VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, April 03, 2006
BUNGE LA ONTARIO

Hili ndio jengo la Bunge la jimbo la Ontario ninaloishi.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:51 PM | Permalink |


Maoni: 12


 • Tarehe: 6:33:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Jeff, unajua jambo moja ambalo hawa wakoloni huwa wananifurahisha ni tabia yao ya kupenda kutunza majengo ya zamani zile (ama kuyatunza kama yalivyo au kujenga mengine yenye ramani/michoro kama hayo ya zamani) ili kutunza urithi na historia yao. Sisi kule nyumbani majengo ya zamani tunayaona kuwa yatuwekea kiwingu, tunayabomoa haraka sana ili kujenga majengo ya vioo tupu. Utaona miji kama London ni miji ilitapakaa majengo ya miaka na miaka, majengo yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye riwaya za akina Dickens au Shakespeare.

   
 • Tarehe: 6:44:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Jeff, naona umetoa ule ufito wa juu wa kwenye blogu yako (asante Vijimamboz kwa maarufi uliyogawia wengine). Lakini tatizo ni kuwa ule ufito nimekuwa (labda na wengine pia) kutafuta habari ulizoandika huko nyuma (pia kwenye blogu za wengine). Kwenye ule ufito kuna kile kisehemu kinakuwezesha kusaka habari zilizoko ndani ya blogu unayoisoma (search this blog). Kwa mfano, nilikuwa nasaka habari ambazo Michuzi kaandika na akakutaja kwa ajili ya makala yangu ile kuhusu maadili. Nilichofanya ni kuandika jina lako pale kwenye ufito wa blogu yake.

  Kwahiyo nadhani kama utaamua kuondoa ule ufito na kuzuia uwezo wa mtu kusaka habari fulani ndani ya blogu yako (ukichukulia kuwa bado blogger haina maudhui) utakuwa unatupa kazi ya ziada. Ambacho unachoweza kufanya ni kuweka kidude cha kusaka habari, labda sehemu nyingine na sio kwenye ufito. Ngoja nitaingia blogger kutazama jinsi ambavyo hii inaweza kufanyika. Au yeyote anayefahamu asaidie. Sijui kama wengine mnatumia ule ufito kusaka habari za nyuma. Mimi ninautumia sana, ukitolewa utakuwa kama umenikata miguu nishindwe kutembea kila kona ya blogu yako.

   
 • Tarehe: 8:04:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger charahani

  Anachosema Ndesanjo ni kweli

  Hapa kwetu kila sehemu yenye maudhui ya kikale kale imebomolewa na kisha kuwekwa vijengo vya 'kizungu'. Hii ina maana kwamba muda si mrefu tutapoteza utambulisho wetu tutabakia labda na majengo mawili au matatu ya St. Joseph na Azania Front kwingine kote kwaheri.

  Hii ni noma tunazidiwa hata na wenzetu Wazanzibari ile beit el jaib ni kivutio tosha kwa watu wasioijua wanatoka mbali kufika hapo.

  Ina maana we Msangi unaishi ndani ya hili jengo la Bunge, hebu nitoe ushamba inakuwakuwaje au kwa sababu ni jengo la ghorofa nyingi tumezoea kwetu hapa jengo kama hilo linakuwa limejaa ofisi tupu.

   
 • Tarehe: 8:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ndesanjo,
  Utunzaji wa majengo ya kale ni mojawapo ya tabia ambazo ni nzuri kuziiga.Historia ni shule nzuri sana na vitambulisho kama majengo na vinginenvyo ni mihimili mizuri sana.
  Sikuwa na habari kwamba ile mini search engine pale juu ilikuwa inatumika kwa mtindo huo..kama sitopata namna nyingine ya jinsi ya kutafuta malighafi katika hii blogu yangu basi nitairudisha kama mwanzo ili nisikukate miguu Ndesanjo.Pole kwa usumbufu.
  CHARAHANI...samahani kwa kupindisha kiswahili kidogo.Nilikuwa nina maana ninaishi jimbo la Ontario na sio ndani ya jengo la Bunge.Humo hakai mtu..ni kama ulivyosema..ni ofisi kwa wingi tu.

   
 • Tarehe: 12:19:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

  Nashukuru Muheshimiwa Ndesanjo kwa maoni yako lakini watu wengi walikuwa wakiniuliza kuhusu hiyo search box maana mtu unashindwa kuweka baadhi ya vitu fulani juu ya page yako.Alafu watu wengi ina wakera sana!

  Kuhusu kutafuta habari mbona kuna section ya Archives ambayo inaonesha nakara zote zilizopita.Sasa kama mtu unataka nakara zilizo pita click hapo na utaziona.

  Nimeamua kugundua hizo code kwa kuwapa watu uhuru wa kuweka vitu kama tarehe (karenda), saa na n.k kama unavyo ona page yangu ilivyo.

  Nashukuru Muheshimiwa kwa Maoni yako.
  ©2006 MK

   
 • Tarehe: 12:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Michuzi

  ndesanjo, ni kweli. ila lile kanisa la kule kilema lenye umri wa miaka 100 bado lipo, nakuhakikishia. hata la pale bagamoyo pia lipo. asante jeff kwa picha

   
 • Tarehe: 12:37:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Michuzi

  ndesanjo, ni kweli. ila lile kanisa la kule kilema lenye umri wa miaka 100 bado lipo, nakuhakikishia. hata la pale bagamoyo pia lipo. asante jeff kwa picha

   
 • Tarehe: 1:55:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  MK,
  Tatizo la Archive ni moja. Ngoja nikupe mfano. Majuzi nilikuwa natafuta picha na habari aliyotupa Mwandani iliyosema: Tanzania Business Community. Sasa ukiwa hukumbuki tarehe na mwezi ambao aliandika habari hiyo ukienda kwenye "archive" hutatumia muda mrefu sana kuipata. Ukitazama "archive" ya blogu ya Jeff utaona ina tarehe, miezi, na mwaka. Je habari aliyoandika ambayo hukumbuki mwezi na mwaka utaipata vipi? Utakuwa kama mtu anatembea kizani.
  Jaribu kwenda kwa mwandani: http://mwandani.blogspot.com
  kisha nenda pale kwenye ufito wa juu. Andika maneno haya: tanzania business community kisha bonyeza kwenye "search this blog" utaona unaipata habari hiyo mara. Lakini kwa kupitia kwenye "archive" ni vipi utaipata habari hiyo kwa muda mfupi hivyo?

  Nadhani kama mtu anataka kuweka vitu pale juu au hapendi ufito ule anaweza kubadili. Ila nilitaka tu kusema kuwa ufito ule unatusaidia wasomaji kwa kiasi fulani.

  Halafu kuna kile kibendera pale kwenye ufito ambacho kazi yake ni kutoa taarifa kwa blogu ambazo zinatumiwa labda kinyume cha sheria au maadili. Kinaweza kuwa hakina kazi kubwa kwenye blogu zetu kwa sasa, ila kimesaidia kwenye matukio fulani fulani. Ila hili sio kubwa kwangu kama uwezo wa kupata mambo yaliyoandikwa huko nyuma kwa urahisi bila kuanza kubuni mwezi na tarehe ambayo habari hiyo iliandikwa.

   
 • Tarehe: 2:55:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Duh!Nimepata tabu ya kutafuta nilipoweka vijiko kwenye kabati langu mwenyewe,
  Ndesanjo sina budi kukubaliana na wewe kwa sasa kwamba inakuwa ngumu sana kutafuta "zilipendwa" katika mtindo huu.
  MK itabidi turudi tena darasani.

   
 • Tarehe: 10:23:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

  Jeff nimefanikiwa kutengeneza code nyingine hizi nadhani mtazipenda maana zinaondoa NavBar na kukuwekea kibox kidogo ambacho wewe ndio utachagua wapi kikae ktk site yako ambacho unaweza kusearch kila kitu. bonyeza hapa ukazisome.

  Nashukuru,
  ©2006 MK

   
 • Tarehe: 11:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  MK,
  Juhudi zako zinatia moyo sana.Usichoke tafadhali.Nimejaribu kufuata maelekezo yako.Nilifanikiwa kuiweka hiyo blog search kama ya kwenye blogu yako.Kwa bahati mbaya nilipopreview ikawa imefanya picha yangu kwenda chini kabisa.Hili liliwahi kunitokea siku za nyuma.Ndesanjo atakumbuka jinsi nilivyokereka mpaka nikachukua template nyingine.Una ushauri wowote? Sitaki kuiweka pale juu kama alivyofanya Miruko.

   
 • Tarehe: 6:11:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

  Jeff nimekutumia e-mail kupitia jeffmsangi@sympatico.ca kuhusu maelekezo ya kufanya ambayo yatafanya search box ikae mahali pazuri bila matatizo yoyote.

  Naomba isome kidogo na ufuate maelekezo. Nakutakia kazi njema.

  Nashukuru,
  ©2006 MK

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker