
Kuna nyakati huwa nazikumbuka sana enzi zile za kushinda vijiweni na kwenye vigenge vya hapa na pale tukidanganyana na kuuziana nyeti zisizokuwa na unyeti wowote.Enzi zile ambapo tulikuwa tukikutana "maskani" tukapigishana stori juu ya raha ya kupata msuba na jinsi unavyoweza kukuliwaza kutokana na mawazo uliyonayo ya kukosa kazi. Unajua Tanzania imekuwa na recession ya kudumu kwa muda mrefu sana na ndio maana vijiwe havikauki. Bado nakumbuka jinsi tulivyokuwa tukipanga madili na kuweka mezani kabisa jinsi tutakavyogawana mapato. Tukapigishana hadithi za kununua Mercedez Benz Convertible wakati hata baiskeli ya miguu mitatu hatuna!
Lakini kali zaidi ni lile la baadhi ya "wajuaji" walivyokuwa wakipakaza na kueneza "ukweli" wa wakati huo kwamba eti yule mwanamuziki wa Marekani aliyekuwa anaitwa Marvin Gaye alichapwa risasi(aliuawa) na baba yake mzazi kwa sababu alikuwa msenge. Hukuwahi kusikia hivyo wewe?Basi kijiwe chenu kilikuwa hakina mabingwa wa kuleta hadithi za Ulaya na Marekani. Hizo ni zile enzi ambazo njia pekee ya kwenda "mamtoni"ilikuwa kuzamia meli,potelea mbali yanayoweza kukukumba mbele ya safari. Enzi zile wafagizi na wapishi katika meli za nje wanaotokea mitaani kwetu tuliwabatiza "zungu la unga".
Unajua kama hadithi/kashfa ile ya Marvin Gaye ilitungwa ili kila mtu aogope ushoga kama ukoma basi ilifanikiwa sana.Kampeni za namna ile naweza nikaziunga mkono.Najua hata wewe unazo hadithi/visa kutoka maskani kwenu. Kwanini basi tusikumbushane hapa kwenye blogu? Hebu tukumbushane ENZI ZILE.....
enzi nzikumbukazo mimi ni za akina dj (marehemu) kalikali na neagre jay pale ymca , dj john peter pantelakisna dj (marehemu) choggy sly kule silversands, dj gerry kotto na dj seydou mbowe na dj emperor (huyu joseph kusaga bosi wa clouds fm) akiwa motel agip.
enzi hizo sexual healing ya mavingei ilikuwa balaa kama zilivyokuwa dont stop til yu geti inafu ya maikojackson. mtindo tawala enzi hizo ulikuwa break dance na nakumbuka wimbo wa 'u cant stop us now, dancing' sie tulikuwa tunaimba: maiko jekson njoo, sitaki...kama hutaki nenda...