Tarehe: 11:53:00 AM, Mtoa Maoni:- MICHUZI BLOG
Tarehe: 8:14:00 AM, Mtoa Maoni:- mwandani
Kumbe Choggy keshatutoka! huku kupitwa na wakati kubaya. Mungu amrehemu.
Hata mimi nilisikia hicho kisa cha Mavingei.
Kikao kwenye gogo vivu mjomba magirini ndio yalikuwa yakitawala, kila mtu alikuwa na filingi za kujimbinjua. kitu kibaya zaidi kilikuwa kuwazikiliza wale masela pale lebanoni (magogoni), wakitoa stori za bichi la siria, bichi la misri, na mitemba ya manta laini, mo mac momack... Magirini ya kuzamia na kujificha kwenye hachi za meli, jinsi ya kuongea na kapteni akupe u-deki boi...
nilikkuwa naijua meli na namba za hachi hata bila kuikwea hiyo meli.
Mambo ya kijiweni hayajakwisha hivi karibuni tu pale bichi la Bombay niliwaona watoto wa kibongo wanapiga stori kama hizo, na wanafanya mabo kama yale ya stori za vijiweni, kuna yanki nilikutana naye ndio kwanza atoke bongo baada ya kuwekwa mazabe New jersey, akadanganya kuwa yeye ni muavori kosti, walipomshusha uwanja wa ndege kulikuwa na machafuko ilibidi aililie bongo, kufika nairobi akatoa kitu kidogo mara tu akajimbinjua bombay tulipokutana.
Recession, vijiwe vipo mpaka leo ndugu yangu.
Tarehe: 8:24:00 AM, Mtoa Maoni:-
MASELA KIJIWENI
Ali Master: Ndiyo babu yangu!
Hapo mitaa ya Instambuli hapo. Hapo babu yangu makabalee mpaka asubuhi. Humo mitoto ya Kimanga, Kizungu, inacheza na bikini tu. Likikuzimia linakufuata lenyewe " yu wanti go endi mi?" Usipapatikie maanake inaweza kuja zali nyingine hevi zaidi we unampa " Ai teli afta taimu"
Paulo Mtanga: Aaah hiyo mitoto ya kimtoni wala haimaindi atakuambia tu "no sweti, ai weiti yu" Hapo Istambuli siyo poti mchezo. Hapo kila kitu; drai poti, auti anka, taneli kila kitu maanake. Meli zinaingia poti kwa trafiki laiti kama magari yanavyovuka daraja la Kajima. Siyo mchezo poti liko openi twenti foo awazi.
Ali Master: Huko wiki moja mtu unatuna, moningi unapata uji uliopikwa kwa unga wa keki halafu umetiwa mapande ya siagi. Lanchi unakula poki na viazi vya kuponda, saladi, glasi ya maziwa. Jioni unapata bifu la kukaanga tena ile mipande hevi (anaonyesha kipimo cha kiganja cha mkono wake) na chipsi pembeni juisi.
Paulo Mtanga: Wiki!? Hiyo menyu siku mbili tu unaumuka, mashavu utafikiri unapuliza moto! Ukijiangalia kwenye kioo wewe mwenyewe hujitambui. Hilo menu Bongo mawaziri hawaipati, fanya mchezo nini?
Ali Master: Subutuuu! Hiyo misosi iliyopimwa na imepikwa na shefu aliyesomea kwa madigrii ya upishi. Mawaziri menyu kama hiyo wanaiskia kwenye bomba. Chakula unapikiwa na boi katoka shamba. Ukurutu kibao mikononi. Akisonga ugali matone ya jasho yanatiririkia ndani ya sufuria. Nyumba nzima kipindupindu. Kwani unafikiri Ostabei hamna kipindupindu? Dooo, basi huko ndiyo kipindupindu ndiyo kwao lakini wanafanya siri.
Mshikaji mwingine yuko bangi nyingiii anasikiliza kwa makini.Ghadhabu za kujikata zinamwingia kama homa ya malaria. Inamtoka " No sweti safari lazima.Sasa hivi nikimalizia misheni yangu fulani nachukua simeni buku. Mkoba n'nao, vasinesheni kadi nayo n'nayo. Nasubiri Selebresheni an'tumie kidogodogo toka Kopenihajeni. Nikamilishe dokumenti zote niingie Beira au Msa.."
Ali Master: Kwa nini usipige bboda la Sudani? Sasa hivi Beira na Msa vyuma havikamatiki. Chawa (Stolowei) wengi ile mbaya. Meli ikitoka poti inaingia auti anka siku tatu hata wiki kuanika chawa! Jamani mchango wa lanchi.
Wanachangachanga wanapata pesa ya kutosha kula kodrai kwa mama n'tilie(ukoko wa chini wa wali)Wanaondoka kijiweni kwenda kula kodrai.
F MtiMkubwa Tungaraza.
Tarehe: 11:58:00 AM, Mtoa Maoni:- Jeff Msangi
Tarehe: 1:58:00 PM, Mtoa Maoni:- John Mwaipopo
enzi nzikumbukazo mimi ni za akina dj (marehemu) kalikali na neagre jay pale ymca , dj john peter pantelakisna dj (marehemu) choggy sly kule silversands, dj gerry kotto na dj seydou mbowe na dj emperor (huyu joseph kusaga bosi wa clouds fm) akiwa motel agip.
enzi hizo sexual healing ya mavingei ilikuwa balaa kama zilivyokuwa dont stop til yu geti inafu ya maikojackson. mtindo tawala enzi hizo ulikuwa break dance na nakumbuka wimbo wa 'u cant stop us now, dancing' sie tulikuwa tunaimba: maiko jekson njoo, sitaki...kama hutaki nenda...