
Ukitembelea Paris- Ufaransa ni wazi kwamba utapenda kutembelea na hata kupiga picha kwenye mnara ujulikanao kama Eiffel(Eiffel Tower) .Ukifanya safari za jiji la New York si ajabu ukapenda kwenda kushuhudia ule mnara wa uhuru(Statue of Liberty). Vile vile ukitembelea jiji la Toronto,hapa Canada nina uhakika utapenda kuutembelea huu mnara ujulikanao kama CN (CN Tower) (pichani). Inasemekana kwamba huu ndio mnara mrefu kupita yote duniani ambao umesimama dede. Uliwahi pia mnamo mwaka 1995 kuingizwa katika yale maajabu saba ya kisasa ya dunia.Unaweza kusoma zaidi juu ya mnara huu hapa.
Majuzi nimesikia kwamba huko Chicago-Marekani na Tokyo-Japana inajengwa minara ambayo huenda mmojawao ukachukua nafasi ya CN Tower ambao ndio sahihi ya jiji la Toronto.Nilipiga picha hii wikiendi iliyopita.
Asante Jeff, kwa taarifa za kina juu ya minara ya duania. Umenikumbusha mnara wa uhuru pale mnazi mmoja Dar na ule wa Arusha, nashindwa hata kufananisha.
ReplyDeleteJeff na Reginald
ReplyDeleteMsisahau kuwa Tanzania ni ule pale askari Monument ambao kuna askari kama yule wa kule Moshi ambapo tunaelezwa ndugu zake Msangi wa kutoka pale Kisumundu walikuwa wakitupa mikungu ya ndizi na kukimbia zao.
Hebu angalieni wenzetu wanavyotukuza vyao haishangazi kwamba siku moja ile minara ya pale Mnazi mmoja (wa uhuru) na mingineyo kukuta imebomolewa halafu kikasimikwa kitu cha ajabu ajabu.
Charahani:Afadhali kiwe kitu kingine chochote. Unaweza kuta wamejenga ama baa ama gesti.
ReplyDeletejohn umenikumbusha warsha ya bagamoyo ya wadau wa muziki ambao mojawapo ya maazimio ni kuzindua 'orofea' zilizokuwepo kila wialaya kwa ajili ya kutumiwa na jamii ya mahali husika kama vile muziki, kwaya, maigizo n.k. nakumbuka pale tukuyu siku ya sikukuu jamaa alikuwa-ga anapiga ngoma na filimbi orofea ya polisilaini, na kutuchaji thumni kiingilio.
ReplyDeletesasa hii minara yote iliyoko dar na kwingineko, mingi ni ya mkioloni, ukiondoa wa saa dar, na wa azimio la arusha arusha, na sijui wapi. jeff asante kwa habari na picha. nadhani umeng'amua kuwa mineno mitupu nayo ikizidi inaboaga. hongera sana, nadhani wengine wataiga mfano, hasa we mwaipopo.
Hii habari ya minara kuna wakati nilikuwa nafuatilia sana. Kwanini binadamu tunapenda minara? Je kuna uhusiano wa upenzi wetu wa minara na ile hadithi ya wayahudi ya mnara wa babeli? Nyumba za wachagga za asili, ingawa hazina mnara, umbo lake, pale kwenye paa, liko kama mnara. Makanisani unakuta minara. Misikiti unakuta minara. Majengo ya bunge unakuta minara. Makumbusho ya kitaifa katika nchi mbalimbali yanatumia minara.
ReplyDeleteAsante kwa picha, Jeff!
Ndesanjo,
ReplyDeleteUmenifanya nifikiri vivyo hivyo. Kwamba inawezekana kuna jambo limejificha katika upenzi wa minara. Labda ipo sababu ya sisi wanadamu kupenda minara. Minara kila mahali! Siku hizi hadi majengo ya Bunge ni minara. Ukipata majibu nitafurahi kusikia siri yake. Nimependa kufuatilia minara.