VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, April 27, 2006
"MALIZA MBIO"
Leo asubuhi mjomba wangu mmoja amenitumia barua pepe ambayo imenikumbusha mambo kadhaa muhimu sana. Kichwa cha habari cha ujumbe wake kilikuwa "Finish The Race".Nadhani tafsiri rahisi ni "Maliza mbio".Nilipoendelea kusoma nikakuta kwamba mjomba alikuwa ananikumbusha habari ya John Stephen Akhwari iliyoanzia kule Mexico City Oktoba 20 mwaka 1968.

Habari ya
John Stephen Akhwari ni habari ambayo imetumiwa na watu wa kila namna duniani. Masheikh,maaskofu,wana saikolojia,wanasheria,wanazuoni wa kila namna na hata matapeli. Nilipousoma ujumbe ule nikajiuliza swali au maswali..hivi kumaliza mbio maana yake nini? Hapa nilipo mbio zangu ni nini na je nitazimaliza kwa njia gani? Mfano wa Akhwari una uhusiano gani na maisha yetu watanzania hivi sasa? Wangapi wamekata tamaa,walizianza mbio na wala wasiwe na moyo wa kujitoa ambao nahisi mwandishi aliyemuuliza swali ndugu yetu Stephen alikuwa nao? Je suala ni kumaliza mbio au kutokumaliza kamwe bali kuendelea kukimbia? Maisha yetu ya leo yanaturuhusu kumaliza mbio?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 9:09 AM | Permalink |


Maoni: 6


 • Tarehe: 1:01:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff hapo ndipo mimi huwa natamka;
  "Inawezekana, cheza karata yako!"

   
 • Tarehe: 10:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous charahani

  Jeff

  Uncle wako amekusisitizia jambo la maana mno, kuanza na kisha kumalizia ni jambo la msingi sana, lakini tatizo letu binadamu wengi waanzishaji ni wachache sana na wale wanaoweza kumuadudu kuanzisha 'mbio' mpaka kuzimaliza ni wachache sana. Wengi ni aidha waanzishaji tu au wamaliziaji tu, ndiyo maana hatufanikiwi.

   
 • Tarehe: 12:41:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Falsafa kali sana hii. Maneno machache na aya chache lakini vimebeba ujumbe mzito sana. Nionavyo mimi katika mustakabali wa maisha ya binadamu kuanzisha ni kukubwa kuliko kumalizia. Kwa vipi? Wengi wetu huwa-ga tuna hamasa ya kuanzisha vitu vingi lakini hatuvimalizii kwa sababu anuai kama vile kifo na kukata tamaa. Mathalani mtu anaanzisha kampuni ama kujenga nyumba na kutangulia kunako jicho la haki (kufa) kabla kammpuni aliyoianzisha haijaanza kumlipa ama hajaanza kuishi katika nyumba yake mpya hiyo. Wengine kama vile warithi ama wanyanganyi (dhuluma) huja kumalisia kiulaini.

  Waaidha ninachokipata hapa ni kuwa tujipe moyo kumalizia vile vinavyoweza kumaliziwa pasi na kukata tamaa. Ujumbe ulikuna na chapisho hili kwangu ni kuwa "Usikate tamaa katika jambo ulifanyalo ulifikiralo kuwa ni jema na wema wake utakamilika pale utakapolimalizia" Basi na tuyamalizie mema tuliyoyaanzisha kwa manufaa ya watakaotufuata nyuma. Binadamu tusingalikuwa na hamu ya kuanzisha majambo tusingalikuwa hapa tulipo.

  Hivi isingalikuwa mababu zetu kupanda minazi na miembe leo tungevipata wapi. Ingekuwa vipi wazungu wasigalikwenda kunyakuwa watumwa Afrika ili kuja Marekani kujenga mabarabara ambayo leo hata wakina siye pangu pakavu tia mchuzi tunatumia tukiwa huku. Tujiulize basi, bila kujali tutamaliza ama la, nini tunakifanya leo ili ndugu zetu wakitumie tukisha kuwa malighafi ya kutengeneza mafuta ardhini (kaburini). Hapa niwe na upendeleo kidogo; nini tunaifanyia Tanzania ya miaka 100 ijayo?

  Jipe moyo utashinda.

   
 • Tarehe: 5:16:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Mija Shija Sayi

  Jeff Asante!

  Haya ndiyo maneno wakimbiaji tunapaswa kupatiwa kila mara. Kwa upande wangu suala la kukatiza mbio naona ni kosa la jinai kabisa. Kuna kitu kimoja ambacho wengi wetu huwa hatukizingatii tunapoamua kuingia katika mbio, kitu hiki ni 'uandaaji wa akili' hatuiandai akili kikamilifu kwamba..sasa naenda kufanya jambo hili, ugumu wa jambo hili uko hapa na hapa na hapa na hatari hii na hii na hii inaweza ikatokea ghafla bin vuu! wakati nikiendelea na jambo hili sasa je nina uwezo wa kukabiliana na yote haya?

  Jeff mimi ninaamini sana katika kujisikiliza mwenyewe maana hapa ndipo unapojua udhaifu wako uko wapi na ujasiri wako uko wapi, hali hii husaidia sana katika kuchagua lipi la kufanya ambalo una Uhakika utaweza kulimaliza hata kama nini kitatokea. Tatizo kubwa linalotusibu mara nyingi na kutufanya tusimalize mbio ni kuigilizia mambo, unamuona mwenzio anapanda mlima kilimanjaro na wewe unataka kupanda bila ya hata kujiuliza na kujisikiliza kama unaweza matokeo yake misukosuko ikianza kujitokeza unaamua kuokoa maisha yako, lakini mwenzio ataendelea kwa vile aliamua na kujiandaa hasa kiakili.

  MALIZA MBIO ANZA ZINGINE. SUALA LA USHINDI LINAKUJA BAADAYE.

   
 • Tarehe: 4:30:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger tamba

  Hallow!
  Habari kaka, nimefurahi kuingia kwenye blogu yako na hata sijaanza kusoma nimetangulia kuandika maoni. Nimefurahi sana kwa maoni yako kwangu na kwa kweli yamenipa hamasa kubwa. Ni kweli sisi wenye mtandao inabidi tufanye mawasiliano na kutembeleana, hilo ni muhimu sana na nashukuru. Basi nafikiri sasa mtanichoka kwenye blogu zenu, salam kwa wanablogu wenzetu wengine, na nawatembelea pia. Blogu yako ni nzuri na safi sana. Napenda kazi kama hizi.
  Kila la kweri huko kwenye baridi la ajabu.

   
 • Tarehe: 8:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Jeff,

  Kama una access na ubalozi wetu Japan wasiliana nao. Kuna habari ya Mtanzania mwingine laiyefanya mambo kama haya Japan kunako mika ya sitini.

  Niliposoma nikakumbuka habari ya Seth Benjamin Mpinga yule jamaa aliyetembea mapaka akamaliza matembezi akiwa na homa kali kuunga mkono Azimio la Arusha.

  Niliwahi kubadilishana mawazo kule kwa Damija na mwanagazeti tando MK kuhusiana na uzalendo. Nilimulelezea Mtanzania aliyemchapa Iddi Amin siyo huyu wa Bongo fleva na Twanga pepeta. Mtanzania yule alikuwa na hamasa na nchi yake. Huyu wa sasa ni chizi maarifa fulani.

  F MtiMkubwa Tungaraza.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker