Tuesday, April 04, 2006
PENZI NA BALOZI:Unafuatilia haya ya Uganda?
Kama unafuatilia habari za ki-afrika mashariki si ajabu ukawa umeshasikia sokomoko/gogoro la uhusiano wa kibalozi linaloendelea hivi sasa kati ya Rwanda na Uganda. Kuna mwambata wa ubalozi kafumaniwa na mke wa mtu huko kisha "akadhalilishwa". Lakini je unajua kwamba mwanamke aliyekuwa "akizini" ni mtanzania mwenzetu,dada yetu?Soma zaidi hapa.
Najaribu kuangalia hili suala la "diplomatic immunity" kwa makini zaidi sasa.Hivi hii kinga ya kibalozi haina mipaka hata kwenye masuala ya ugoni?Yaani ukifumaniwa na mke wa mtu kisha ukatoa kitambulisho chako cha kibalozi uachwe uambae zako? Na je masuala ya vyumbani mwa watu yanaweza yakatikisa mahusiano mazima ya kisiasa,kijamii na hata kiuchumi? Tanzania nayo iingilie kati kwamba raia wake anahojiwa katika vituo vya polisi kwa "kula raha zake"(nje ya ndoa lakini)??
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:28 PM


|
Permalink |
-
Jeff nilipita hapa kwa haraka na pia nilikikuta kisa hiki huko nyuma na hawa jamaa wanaonyesha kuwa huyu binti yetu ni mchezo wake ili kutafuta kupanda kimaisha au vipi! Lakini huenda kuna zaidi ya hilo maana hapa panatisha kiasi ngoja niishie hapa nishushe pumzi hili fumanizi yaani acha tu sijui nicheke huku natamani kulia hivi.
-
Jeff,
Jaribu kutafiti kisa cha ugomvi kati ya Besigye na Museveni.... Afrika tuna njia ndefu kuelekea kinachoitwa 'maendeleo' Mungu ibariki Afrika.
Londo
-
Hii maneno inatisha babake. Kama alivyosema Makene inaonekana kadada haka ni chu** Mkononi. kakamchanganya mkatoliki wa watu hata akakaoa. Kumbe hajatulia-tulia na mapepe. kuna habari kuwa watutsi popote walipo 'hawanyimani' hata iwe vipi. Na hako kadada kanaweza kuwa katutsi ka namna fulani. si unajua tena walivyosambaa huko maziwa makubwa, sorry makuu.
lakini hoja yako hapa ni diplomatic immunity. Inawezekana inatumiwa vibaya na 'dioplomats'. Kweli imekua inakera hata baa anataka apunguziwe bei ya ulabu kisa diplomatic immunity. Kama ina-abusiwa yafaa imulikwe na jicho kali kuliko kurunzi la mark msaki. Isije siku moja wakazusha kuwa watoto wa madiplomats ndio tu wenye haki ya kuchukuwa totoz bomba na sie tuliotoka kajunjumele tule-ge kwa macho tu.
-
Lakini hapa Jeff
Hawa watu wana visasi vya muda mrefu, na uhusiano wa kidiplomasia kama anavyosema makene na Mwaipopo ni wa kuwindana. Suala la kula ngoma wala siyo big issue mpaka likaingia katika mvutano kiasi hicho.
Hebu kumbukeni mvutano uliopo kati ya Kagame na Museveni halafu na washikaji waliopo pembeni yao, suala kila mmoja hamuamini mwenzi anaona kama vile anachunguzwa.
Jeff nilipita hapa kwa haraka na pia nilikikuta kisa hiki huko nyuma na hawa jamaa wanaonyesha kuwa huyu binti yetu ni mchezo wake ili kutafuta kupanda kimaisha au vipi! Lakini huenda kuna zaidi ya hilo maana hapa panatisha kiasi ngoja niishie hapa nishushe pumzi hili fumanizi yaani acha tu sijui nicheke huku natamani kulia hivi.