VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, April 18, 2006
TUJIFUNZE NA KUFUNZA WENGINE!

Nashawishika kuamini kwamba sote tu-wazima na kwamba hiki kimya kidogo kilichopita ni kwa sababu wengi tulikuwa kwenye mapumziko au heka heka za Pasaka.Ubaya au uzuri wa sikukuu hizi za kidini siku hizi sio za kidini tena.Badala yake ni za kibiashara zaidi.Kwa sababu hiyo upende au usipende zitakuharibia ratiba au mipango yako.

Sijui wangapi bado wanasheherekea sikukuu hizi kwa undani wa imani husika kabisa.Natabiri kwamba ni wachache sana na wanazidi kupungua siku hadi siku.Zamani nimewahi kusikia siku moja kwa mungu ni kama miaka mia hapa duniani.Majuzi nikajiuliza,hivi ikitokea mungu akalala siku moja itakuwaje au ndio inakuwa hivi ilivyo??Au ndio maana anasa na matendo machafu hutawala zaidi siku hizi.Hapo ndipo utakapojiuliza,kama hii ni sikukuu ya kidini,ya ki-imani kwanini polisi wanaongelea kuongezeka kwa ulinzi na doria siku hiyo?Kwanini nyumba za "wenyeji" ziwe adimu kupatikana?Ukiyaangalia mambo kwa mtizamo huu utagundua kwamba tunaishi kwenye dunia iliyochacha kama sio kuoza kabisa.

Nirudi kwenye ninachotaka kuandika hivi leo.Asiyejua historia yake ni kama meli isiyo na mwelekeo.
Ndesanjo, amewahi kuongelea jinsi inavyotia aibu kwamba wakati mwingine inabidi utoke nje ya Afrika ndio uweze kujifunza historia na masuala fulani fulani kuhusu Afrika.Huu ni udhaifu mkubwa sana ambao hatuna budi kuendelea kuupiga vita. Lakini wakati tunaupiga vita udhaifu huo basi sisi tuliopo nje kwa mfano, ni jukumu letu kufikisha nyumbani kwetu lolote jipya tunalojifunza huku.Blogu zinatupa fursa ya pekee katika kufanikisha hilo na ndio maana huwa ni faraja na shangwe kila mara mtu mpya anapoingia kwenye hii jumuia. Hii ndio kusema huna haja ya kuwa na safu yako kila wiki kwenye gazeti kule Tanzania kama vile kina Ndesanjo, Makene, au mimi pale Tanzania Daima (hii tovuti sijui itaisha lini kutengenezwa)ili kuweza kupashana habari,kubadilishana maarifa na umma uliopo nyumbani Tanzania.Blogu zinasomwa sana hivi sasa.

Changamoto hii haishii kwa walio nje tu bali hata wale waliopo nyumbani. Technolojia imetupa fursa ya kwenda sambamba na yeyote yule,popote alipo kwa kutumia mtandao.Unaposoma jambo jipya,mawazo mapya,historia ambayo hukuijua hakikisha unawafikishia wenzako pia. Usikae nacho mwenyewe ukadhani huo ndio werevu. Ukimfundisha au kumuelewesha mwenzio ndio na wewe unazidi kujifunza.

Ni wazi kwamba yapo mengi sana ambayo yamepindishwa kwa makusudi kuhusu historia yetu. Mapindo hayo yametuletea mtindio wa ubongo ambao unaendelea kututafuna kama kansa. Yote mazuri ya kwetu leo hii tunayaona hayafai.Ukweli kwamba historia ya binadamu inaanzia Afrika tunaikataa hata sisi wenyewe. Ndio maana tunaenda kuhiji Mecca na Israel kwa sababu tumeambiwa pale Mlima Kilimanjaro au Ujiji-Kigoma sipo. Dada zetu wanajiwekea kansa kwenye vichwa na nyuso zao kwa imani potofu kwamba vile walivyo sio vizuri. Hawa nadhani hawajiulizi kwamba kama hizo dawa ni nzuri kwa matumizi ya binadamu kwanini utumie gloves kupakia?Kama ngozi ya mikono haiwezi kuhimili,ngozi ya utosi wako na uso wako ndio inaweza?


Ni lazima tujitahidi kubadili hizo fikra...adui yetu ni kupotoshwa kwa historia yetu. Ndio maana ni muhimu sana kuchangia katika kuandika wikipedia. Tuandike upya historia zetu na kama tukipata zilipoandikwa,tukazisoma na kukubaliana kwamba ni sahihi hatuna budi kufikisha ujumbe huo kwa wenzetu,vijana,watoto,wazee,wanaume na wanawake. Ukifuata tovuti hii utakutana na mengi,huu ni mkusanyiko wa historia ndefu ya Afrika.Ukiona yanayokufaa wapatie na wengine tafadhali.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:06 PM | Permalink |


Maoni: 11


 • Tarehe: 7:16:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff safi sana kutukumbusha kuingia katika wikipedia, nadhani kuna haja sasa ya kuandaa makala ya wikipedia ya kiswahili maana Ndesanjo kasaidia sana kuhusu ulimwengu wa Magazeti Tando. Tuna kila sababu ya kila mmoja kufanya nafasi yake kuliko kubaki walalamikaji

   
 • Tarehe: 7:44:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Nianze kuchangia hoja yako kwa kunukuu sehemu hii: 'Ni lazima tujitahidi kubadili hizo fikra'.

  Fikra zetu hakika zimeganda mithili ya matope. Maana ingekuwa mgando wa ice cream basi ingekuwa vema walau twaweza pata desert (kifunga mlo).

  Nilikuwa kwa Michuzi na kukumbana na michango ya wachangiaji kadhaa wakiponda wasanii wetu Bongo kuvaa hereni, kusuka nywele na kurarua miili yao (tatoo). Wengi wetu tumekua tukisahau asili yetu na kuigiza nyingine kwa gharama ya kudharau vyetu na kutukuza vigeni. Ni nani asiyejua kuwa tokea enzi na enzi wamasai, wake kwa waume, wamekuwa wakivaa hereni na kusuka nyele. Ni nani asiyejua kuwa wamakonde wamekuwa wakirarua nyuso zao ama wagogo (ndonya).

  Tanzania hivi sasa kuna ubakaji wa mali ghafi. Ubakaji huu ni wa kutozitumia vema na ama kuzipoteza ama kuwaachia wajanja wajichukulie kiulaini. Matunda mangapi yanaozeana Tanga kwa mfano. Machache yanauzwa kuelekea Abudhabi, Saudi Arabia na kwingineko. Embe moja mathalani laenda tengeneza michupa mi-5 ya juisi na kisha kuja kuuzwa bongo. Nasi tukiona imetoka ughaibuni tunakimbilia na kushangilia kwa gharama ya kudumaza vya viwanda vya kwetu. Hii inaitwa maarufu U-turn production. 'Ni lazima tujitahidi kubadili hizo fikra'

  Dini ndio usiseme. Huko ndio kuna mkanganyiko balaa. Baada ya karne lukuki za kutawaliwa kifikra na kiroho sasa hata nazo hatuzifuati tena. Miaka ya nyuma ilikuwa haba kukuta mfano ndugu zetu wa dini ya kiislamu wakikaa na sisi chini ya miarobaini wakiagiza maji na ile 'iliyowakutanisha Mark Msaki na wanadodoma kule Dodoma'. Leo waambiwa kunako mfungo wa ramadhani 'biashara haiendi'

  Ndugu wangu wa kristo ndio usiseme. Kanisani ni fasheni sio pahala pa kuabudu. Pengine ni pahala pa kwenda kuachunguza girlfriend mpya na kushindana kutoa sadaka. Yametushinda hata majina tu. Niliwahi kuambiwa sehemu fulani kuwa 'Petro' maana yake ni "jiwe/Mwamba". Kama unampenda sana huyo Petro kwa nini basi usimuite mwanao 'Jiwe'au 'Liganga'. Ona sasa leo twafahamika kwa majina ya Boniphace, Grace,Abdul na Rahma. Pengine tungeweza kuwa na majina kama Rehema, Havinitishi, Sijali na Nganenepa, majina ambayo ukiwa nayo unaonekana 'haujasoma'.

  Afadhali ndugu zangu wachaga (waliopo Tanzania)wao walau mara moja kwa mwaka hurundikana maparomokoni mwa mlima K'njaro walau kutoa sadaka. Chetu ni kizazi kilichobakwa na tamaduni za nje.

  Kumbe basi bado tunayonafasi. Ingawaje tumechelewa, masuala mengine yanaweza kutangamana. Kwa nini basi badala ya ndugu zangu wakristo kutafuna divai na kamkate ka ngano wasitafune ulanzi/mbege na muhogo hivi. (muhogo nao naambiwa uliletwa tu Afrika).

  Kwa nini dini zisifundishwe kwa kiswahili, kinyakyusa ama kipare na kuendeshwa kwa lugha hizo badala ya kiarabu na kilatini. Mungu anakusikia ukisema kiarabu sana kuliko kichagga ama kikuyu?

  Alamsik Binuur

   
 • Tarehe: 5:14:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous mtandawazi

  Jeff una mawazo si haba. Ni kweli tumekwepa bara letu kuja kusoma ya Afrika huku. Vyuoni Marekani kuna mafunzo ya Maswla ya Kiafrika eti. Ukichunguza vizuri utapata Mkenya, Mnigeria , Mtanzania n.k.

  Hii ina maana kwamba vyuo vikuu vya Nairobi, Darsalaam au Makerere havina elimu mufti kuhusu Afrika? Tumebakwa kama anavyosema Mwaipopo labda nitaongeza kwamba hatujabakwa tu bali tumetingishwa mimba na manii haramu ya mataifa ya Magharibi. Haya basi matokeo huwa kuzaliwa kwa Wanaharamu ambayo watafanya ngono na wanaume wenzao, watadhamini hizo 'deserts' badala ya mihogo tupandayo, watadhamini juisi kutoka Magharibi badala ya maembe na machungwa tunayokuza n.k.

  Tunahitaji kuamka kama bara Afrika nikidhani.

   
 • Tarehe: 10:05:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

  Hii Nakala ni nzuri sana.

  Maoni yangu--> Kwa ujumla kilichosemwa hapa ni ukweli mtupu sana ya kwamba ktk idadi kubwa ya wa afrika watu wamesahahu walipo toka, BOB MARLEY alisema in this great future you cannot forget your past hakimaanisha ya kwamba ata kama maisha yakoje (mazuri) hauwezi kusahau wapi ulipotoka. Pia kuna mengi alisema ktk Exodus na Redemption song.

  Hapa kilichofanyika ni udanganyifu (psychological manipulation)kwa kutumia TV na vyombo vyote vya habari toka nje.

  Mimi nina muona Binadamu ni mtu complex sana ambapo ni rahisi kua-adopt tabia yoyote kadli muda unavyo kwenda lakini ata kama yuko ivyo Binadamu anaye toka Africa yeye ni rahisi ku-adopt maisha mengine na kusahau maisha ya kwake aliyo kulia.
  Kingine kuhusu Dada zetu kuweka hizo chemical ktk sura zao ni dhana iliyo kaa ktk maisha na ktk akili ya kwamba akiweka Mabutu au bila kutumia vitu vya kuwa mweupe hawezi kuwa mzuri.

  Pia kitu kingine kilichofanya muafrika ama Mtanzania kuweza kusahau wapi alipotoka nadhani ni tatizo la ukoloni, utumwa, na hili tatizo la siku hizi la Mwafrika kutothaminiwa na kuonwa kama si lolote ktk hii dunia (Ubaguzi wa rangi) sasa ktk haya yote kwa mtu wa kawaida akiona haya atajiona yeye sio kitu chochote cha thamani na kuanzia kuweza kuiga na kusahau yale ya nyumbani.

  Kingine inabidi Serikali na wadau wengine wote kuweza kuimiza Vijana wetu kuweza kusoma sana History ya nchi yetu au History ya Afrika kwa ujumla ili ata kizazi kijacho kiweze kujua roots ya mtanzania ama mwafrika ilitoka wapi na sio kila mtu kuweza kubakia kusomea udaktari, Engineering na kozi zingine nyingi tu.Hii isiwe ktk Primary schools au Secondary schools tu bali iwe mpaka ktk Vyuo Vikuu.

  Ktk nchi za wenzetu utakuta kuna mwana History wa kila jambo na hii inawezesha kufikisha kumbukumbu ya mataifa yao kuweza kuendelea na kuota mizizi toka kizazi kimoja mpaka kingine.

  Mwisho, Kuhusu maswala ya dini mimi sitaki niweze kuzungumzia lolote maana kwa nafsi yangu mimi ni mkristo na nina amini Mungu yupo na kufuata na kuamini yale yote maandiko ktk bible, ata kama nina elimu au mafaniakio, maendeleo au utajiri kiasi gani siwezi kukana kuhusu ili swala sababu kuna ishara na dalili zote za ki-science na zisizo za ki-science zinazo onesha hili swala. Ukijiuliza maswali mengi utaona ninayo sema.

  Haya yalikuwa ni Maoni yangu binafsi na sio lazima kuweza kuwa sahihi na wengine.

  Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa.

  Nashukuru,
  ©2006 MK

   
 • Tarehe: 9:06:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Nakubaliana sana nawe kuwa mara nyingi ukiwa mbali na mahala ndio unaweza kupatathmini vilivyo. Kwanza ni vile mtu anapata muda wa kufikiria kutokana na upweke na tamaduni ngeni za ughaibuni.

  Kadhalika ule ukweli kwamba nafasi yako katika macho ya watu wa magharibi inakuwa dhahiri. Pamoja na utandawazi - kwamba Global village is a small world! - unakuta kuna ufa mkubwa wa dhana na mawazo kati yako na wenyeji wa magharibi katika maisha ya kila siku.

  Tatizo ni kwamba siyo rahisi kumfahamisha mtu aelewe kuwa utamaduni wa kimarekani au wa kimagharibi kwa kiasi kikubwa hauna cha kutufundisha juu ya mahusiano ya mtu na mtu - kwani hakuna mahusiano ya jamii ya kawaida, watu hawasabahiani, majirani hawajuani, dharau mtindo mmoja, talaka nje nje, miziki imejaa matusi na kadhalika.

  Ni wajibu wa kila mmoja - walio nje na nyumbani - kufikiria jinsi ya kutukuza utamaduni wetu na kuelimisha umma.

  Utamaduni pekee ndio kisima cha maji yanayotuponya kiu. tukipoteza hicho ndiyo basi, tumekwisha.

   
 • Tarehe: 2:55:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Bwaya

  Mwaipopo umenichekesha sana hasa kwa maneneo haya hasa unaposema fikra zetu zimeganda mithili ya matope!
  Habari kwamba biashara ya kitimoto huwa haiendi nyakati za mifungo, ni mpya kwangu. Nitaanza kuifuatilia.
  Ninachoweza kusema ni kwamba ni lazima sisi kama Waafrika, turejee katika tamaduni zetu. Tukumbuke tulikotoka. Tuache ushamba wa kufikiri kila kinachotoka kwa hawa jamaa wenye pua ndefu ni cha maana. Tuache ujinga wa kufikiri kuwa kujua kimombo ndio kusoma. Jmabo hili ama kwa hakika lina gharama zake maana wengi wetu tumekamatwa kwa namna moja ama nyingine.
  Watu wanamdai mzee JK na Ngoyai kupitia upya mikataba za kizandiki. Nadhani kuna haja ya kuipitia upya hata "mikataba" hii ya dini zetu ambazo, hata kama tunazitetea, tumezibeba kijuu juu!
  Tujikomboe!

   
 • Tarehe: 4:47:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

  DINI NI MKATABA WA MTU BINAFSI NA IMANI YAKE PAMOJA NA MUNGU MSICHEZE NA DINI WALA MUNGU, NA TUZUNGUMZE MENGINE. ULIZA NAFSI YAKO KWANINI UPO KTK HII DUNIA NA NINI MADHUMUNI YA KUWEPO WEWE. MSIJE MKASUBIRI MPAKA SHIDA IKUFIKIE NDIO TUANZE KUTAJA EH MUNGU NISAIDIE, MARA NYINGI SHIDA AU MATATIZO NDIO KIPIMO CHA KUJUA IMANI YA BINADAMU YA KUABUDU MUNGU.NI HAYO TU KWA LEO.

   
 • Tarehe: 11:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger charahani

  Mwaipopo

  Hii pointi imenifurahisha sana "Kwa nini dini zisifundishwe kwa kiswahili, kinyakyusa ama kipare na kuendeshwa kwa lugha hizo badala ya kiarabu na kilatini. Mungu anakusikia ukisema kiarabu sana kuliko kichagga ama kikuyu?"

  Wabongo wengi tunalost kwa sababu hii watoto wetu pengine itafika wakati watabakia njia panda kwasababu hawafahamu kiarabu, hawafahamu kilatini, lakini wanataka kuwasiliana na Mungu wao watafanyaje? kwanini kama ulivyosema mawasiliano kati ya mja na Mungu wake yakarahisishwa kiswahili hata kama ni dini ya kwao.

   
 • Tarehe: 11:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Lyimo

  mbona dini zinafundishwa kwa lugha ya kiswahili na lugha nyingine nyingi tu, Mbona QURAAN ipo ktk lugha nyingi tu, hamjaona kwa lugha ya kiingeraza, punjab, urdu, n.k hamjaona biblia kwa kinyaruanda, kiswahili, kifaransa, kiingereza na luga nyingi tu.Mnataka sasa muabudu sanamu na kuita mungu sababu enzi hizo waafrika twalikuwa tunaabudu hizo dini au wengine uchawi. Msikatae haki ya mungu na hizi dini kuwepo na wengine kuabudu. aisee baba zangu nipeni majibu

   
 • Tarehe: 2:18:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Lyimo nisaidie hili tu. Azana inapigwa kwa lugha gani, mashindano ya Quran tukufu yanakwenda kwa lugha gani. Ukinisaidia hili itakuwa imetosha.

   
 • Tarehe: 5:23:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous lyimo

  aise unajua hizi dini ni za watu sasa utakuta kuna wakiristo, waisilamu, n.k zote zinahabudu mungu. ktk enzi hizo kulikuwa kuna mitume ambapo hao mitume walibarikiwa na kupewa msg ya mungu kwenda kwa binadamu wenzao sasa kama mtume ni kutoka ktk asilia fulani kutokana na mambo ya kidini wanabidi kuiga mfano toka kwake mf.maisha yake n.k binadamu aliye kamilika ni yule ambae anakubali ya kwamba mungu yupo na dini tulizo nazo zinafundisha mafundisho ya mungu.itakuwa vichekesho baba angu kuweza kuishi bila misimamo ktk hii dunia bila kujua mungu yupo na hizi dini ni sahihi. nakuomba baba angu usije kuaraanika kwa kukana hilo.sawa azana yapigwa kwa kiarabu lakini ni kama lugha tu, ndio sababu unaona ata wakiristo wanazungumza lugha yoyote.kusema kiarabu au kiswahili au la si kitu bali ni kuabudu mungu tu. waafrika tulikuwa tunaabudu sanamu na uchawi (vodoo) sasa baba angu unataka tuabudu hayo na kuacha mungu? kwa kweli aise uwezi kuniambia nifate hayo. mwaipopo na wote nawaeshimu sana lakini baba zangu kwa hili mmeteleza kweli.ya mungu tumpe mungu na ya kibadamu tumpe mungu na binadamu.mwache mungu aabudiwe na wache watu waabudu sababu hakuna kitu kilichokufanya wewe kuwapo ktk hii dunia na kufanikiwa zaidi ya mungu.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker