
Kabla kipindi cha baridi kali hakijaanza miti yote hupukutisha majani yake kama unavyoona kwenye picha hii.Msimu huu huitwa Fall.Nadhani hicho ndio ndio kiangazi cha kule kwetu.Tofauti ni kwamba kiangazi chetu hubakiza japo majani machache kwenye miti. Baada ya miti na majani yote kupukutika majira ya baridi kali(Makene anakumbuka baridi ninayoiongelea alipotembelea Canada mwishoni mwa mwaka jana) huanza.Yakiisha huanza majira ya Spring ambayo ndiyo haya tuliyonayo hivi sasa.Hii ndio masika ya kule kwetu.Inakuwa mvua mtindo mmoja.Kwa bahati nzuri au mbaya leo hamna mvua hapa na jua limewaka,mawingu yamefunguka,bluu inaonekana.Nimepiga picha hii mchana wa leo.
Nimeona hiyo Jeff, Ernesto naona naye kakimbilia joto la Tanzania, yupo Arusha sasa. Baridi ile haifai kabisa, mimi siitaki bora nikatinge koti na tai Bongo lakini si vichuguu vya nguo Canada.