
Dunia inawayawaya. Msemo huu nimewahi kuusikia na kuukubali katika kamusi yangu.Kwa bahati mbaya sikumbuki vizuri niliusikia wapi.Kumbukumbu ya mbali inanionyesha kwamba niliwahi kuusikia kwenye masuala ya "injili".Enzi zile nilipokuwa sijajua kwamba dini sio uhuru bali inaweza kuwa utumwa wa aina yake.
Kuna jambo ambalo nimekuwa nalitamani na nitaendelea kulitamani sana.Sio jingine bali la kuona siku moja viongozi/kiongozi wa nchi yeyote duniani w/anasimama imara dhidi ya Marekani.Hapo ndio nishawahi kuhoji akili za viongozi wa yale mataifa yanayounda lile kundi la G8.Kwamba inakuwaje na wao wanabakia kuwa walalamikaji dhidi ya Marekani badala ya kuwa wepesi(uwezi wanao) wa kuiambia Marekani,imetosha?
Hivi sasa kuna kiongozi mmoja (kwa bahati mbaya au nzuri yeye hatokei katika lile kundi la G8).Huyu si mwingine bali Mahmoud Ahmadinejad,raisi wa Iran(pichani). Majuzi amefanya jambo ambalo limenifurahisha sana.Amemuandikia barua George W.Bush (Ndesanjo humuita George Kichaka). Kilichonifurahisha sio barua tu bali yale yaliyomo kwenye barua hiyo. Unadhani dunia ingekuwaje kama kungekuwa na viongozi kumi tu wenye msimamo wa aina hii dhidi ya Marekani? Kumbuka ufedhuli wa Marekani unaathiri dunia nzima. Isome barua yenyewe hapa(samahani kwa wasiotumia kiingereza)
Mwisho nimetegua kitendawili cha ile nyumba yenye bendera ya Tanzania nje. Jibu lipo kwenye comments za ile picha.
Barua hii nitaisoma leo usiku nikishiba ugali na maharage.
Lakini natanguliza msemo huu: "Ni heri kufa ukiwa umesimama kidete kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti".