VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, May 17, 2006
HII NDIO TANZANIA KWELI?
Kwa takribani wiki moja na zaidi sasa nimekuwa nikifuatilia kisa kimoja cha kusikitisha sana.Kisa hiki ni cha kutekwa nyara mtoto mdogo wa miaka mitatu ajulikanaye kama Humudy Abubakar huko Dar. Kwa bahati mbaya sina viungo vyote vya habari hii zaidi ya hiki cha leo ambacho kimetoa habari kwamba wateka nyara sasa wamekata mawasiliano hali ambayo inafanya juhudi za kumuokoa mtoto Humudy Abubakari zizidi kuwa ngumu.

Kuporomoka kwa maadili miongoni mwa jamii zetu ni suala lenye historia ndefu sana.Biashara za utumwa na ujio wa ukoloni bado ni vidonda ndugu ndani ya mioyo ya wengi wetu. Maswali kama ni kwanini nasi tumefikia mahali kama hapa tulipofikia ambapo badala ya mtu kutafuta riziki yake kwa kufanya kazi anaona ni kheri eteke mtoto wa mtu kisha adai kiasi chochote cha hela yanakuwa hayana msingi tena.Tunajua kwanini tumefika hapa tulipo.Kila mtu,kwa nafasi yake analo la kujiuliza mwenyewe kwamba anachangia vipi kuboresha au kuyazika maadili yetu mema ambayo kila kukicha yanazidi kuwa na mushkeli? Zamani matukio kama haya ya utekaji nyara wanadamu wenzetu kwa minajili ya kujipatia hela tulikuwa tunayaona au kuyasikia tu kutoka kwa wenzetu kama sio kupitia sinema za Hollywood. Ni dhahiri kwamba hali si shwari tena.Kuwaachia watoto wakacheze kama watoto wanaokulia kwenye "nchi yenye amani" yaelekea kuwa kitendawili kipya hivi karibuni.

Habari hii haitii simanzi peke yake bali inazidi kuumiza linapokuja suala la mchango wa jeshi la polisi na hata vyombo vya habari katika kufuatilia masuala kama haya. Kwa jinsi nilivyokuwa nafuatilia suala hili inaonekana kwamba vyombo vya habari (vingi havikuliongelea kabisa tukio hili la aina yake) havikulipa tukio hili kipaumbele.Ni habari iliyoandikwa kama kujazia kurasa hivi.
Polisi nao sijui nini wanafanya kwa kweli.Naomba nielimishwe jamani kuhusu "intelligence"Hivi kweli mtu anateka mtoto,anapiga na kupigiwa simu mara chungu mbovu na polisi wanashindwa kabisa kujua alipo?Ninavyojua mimi hizi simu za mikononi zote zinafanya kazi kwa kutumia mawasiliano yaliyounganishwa kutoka kwenye mnara mmoja mpaka mwingine (repeaters).Ukinipigia simu kutokea eneo fulani ni rahisi sana kwa polisi kujua uko wapi?Nini kinashindikana kumuokoa mtoto huyu ambaye waroho wa utajiri usiokuwa na jasho wapo njiani kukatisha maisha yake? Mitego ya polisi iko wapi?
Nina maswali mengi sana kichwani kwangu. Tukio hili linazua maswali mengi kupita kiasi.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 4:04 PM | Permalink |


Maoni: 6


  • Tarehe: 1:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Reggy's

    Maswali hapa lazima yawe mengi. Si kwako tu Jeff, naamini hata kwa polisi. Tukio la namna hii, ni geni sana Tanzania, huwa tunayasikia ughaibuni na Marekani. Unafahamu fika kuwa polisi wetu wengi amesoma tu kozi fupi za CCM (si zadi ya miezi sita) na wachache wameweza kuvuka hapo, hivyo si rahisi kwao kubaini mkitego ya namna hii. Pili, unajua fika kuwa simu zetu hazidhibitiwi na mamlaka yoyote. Naweza leo kununua line nikakupigia siku, kisha nikaitupa nikanunua nyingine nikakupigia vile vile. Hoja ya mnara. Mnara unaweza kuonyesha tu miko Magomeni, Kariakoo, Posta. je utanitafuta mtaa upi, nyumba ipi, chumba kipi? Labda cha kufanya ni kuweka mtego katika ulipaji wa fedha wanazotaka watekaji. Kama ni akaunti ijulikane ya nani? kama ni kuziweka sehemu anayezichukua ajulikane...

     
  • Tarehe: 5:00:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Simon Kitururu

    Tanzania ya sasa hivi si ile tena tuliyoizoea.Inabidi kilasekta ziangaliwe upya.Mimi nahisi polisi kozi zao inabidi ziwe updated kulingana na Mazingira ya sasa.Angalia jinsi majambazi yanavyo fanikiwa kuiba mamilioni kila wakati bila kushikwa. Mambo kama haya yana sababisha majambazi mengine kuona kuwa yanaweza kufanikiwa pia bila kushikwa. Polisi wetu bado wanafunzwa kizamani wakati jamii wanayo ihudumia imebadilika hivyo jasho litatutoka. Hivi nakumbuka wakati wa Nyerere ilikuwa inasemekana Maspy wa kibongo si mchezo.Ile ilikuwa porojo nini! Mbona mavitu yao sisikii tena. Au Ma CID ndio hatuna tena? Maana kama wapo kazi yao ni nini?

     
  • Tarehe: 5:31:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Jeff masikitiko yangu ni kuwa mtoto wa miaka 3, katekwa sasa wiki mbili na hakuna taarifa zake? Tena kipindi hiki cha njaa anakula nini kweli huyu au ndio analawitiwa kabisa? Tena suala hili kutopewa kipaumbele bila kuzingatia umuhimu wa maisha ya kijana huyu anayeweza kuwa rais huko kesho? Hivi serikali zetu zinajali maisha ya nani hasa na zinaposema wananchi hawawezi kufa kwa njaa wana maana wananchi wapi au kifo kinapata piccha mbaya kinapotokana na njaa tu au hata ujambazi? Kwa nini viongozi wetu wasitoe ahadi ya wananchi kulindwa na kuwaahidi maisha yao kutoraruliwa na majambazi? Tunangoja nini zile NGO zinazotetea haki za akina mama na watoto, zinafanya nini au kwa kuwa kijana huyu anatoka familia duni? Hata hivyo niwapongeze IPP kwa kukubali kuweka kihabari hiki kiduchu ila tuna kazi sasa ya kuongeza habari hii na kukemea suala hili la kutu kama inavyofanyika huku ughaibuni.

    Jeff samahani je waweza kutuondolea hii word verification maana inachosha na kupoteza muda wakati wa kuchangia? Naomba kuwasilisha hoja.

     
  • Tarehe: 5:38:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    wacha word verification ina ondoa spams, ukitaka maoni yasiyo eleweka ondoa spams.

    spams zina uzi sana na ukizipata ni vigumu kuondoa sababu unaweza kupata maoni 100 kwa siku.

     
  • Tarehe: 8:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Pole Makene kwa hiyo word verification.Hata mimi mwenyewe ninapoandika maoni kama ninavyofanya hivi sasa ni lazima niiweke.Inaudhi wakati mwingine lakini kama alivyosema anonymous hapo juu inasaidia sana kuondoa spams.Labda soon tutapata ufumbuzi mwingine.

     
  • Tarehe: 4:50:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Moyo wangu uko na aliyetekewa nyara mtoto. Hivi mwanangu akiibiwa nitafanya nini...

    Tunakwenda wapi, au ndio tumefika wapi? Tunatekeana watoto nyara Tanzania?

    Silaha za moto zimezidi, wananchi pamoja na askari walipotoka siku nyingi tu (Ona ujambazi wa gari la fedha ubungo- maaskari nao wamo)- japo wanasema wanajifunga mikanda kukabili hao majambazi. Safari bado ndefu.

    Kitururu unasema unasema kweli, inabidi wapandishe madarasa na kubuni mbinu mpya za kukabiliana nao hawa jamaa. Bila kusahau kuchochea watu warudie maadili ya utu.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker