Tarehe: 1:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Reggy's
Tarehe: 5:00:00 PM, Mtoa Maoni:- Simon Kitururu
Tanzania ya sasa hivi si ile tena tuliyoizoea.Inabidi kilasekta ziangaliwe upya.Mimi nahisi polisi kozi zao inabidi ziwe updated kulingana na Mazingira ya sasa.Angalia jinsi majambazi yanavyo fanikiwa kuiba mamilioni kila wakati bila kushikwa. Mambo kama haya yana sababisha majambazi mengine kuona kuwa yanaweza kufanikiwa pia bila kushikwa. Polisi wetu bado wanafunzwa kizamani wakati jamii wanayo ihudumia imebadilika hivyo jasho litatutoka. Hivi nakumbuka wakati wa Nyerere ilikuwa inasemekana Maspy wa kibongo si mchezo.Ile ilikuwa porojo nini! Mbona mavitu yao sisikii tena. Au Ma CID ndio hatuna tena? Maana kama wapo kazi yao ni nini?
Tarehe: 5:31:00 PM, Mtoa Maoni:- boniphace
Jeff masikitiko yangu ni kuwa mtoto wa miaka 3, katekwa sasa wiki mbili na hakuna taarifa zake? Tena kipindi hiki cha njaa anakula nini kweli huyu au ndio analawitiwa kabisa? Tena suala hili kutopewa kipaumbele bila kuzingatia umuhimu wa maisha ya kijana huyu anayeweza kuwa rais huko kesho? Hivi serikali zetu zinajali maisha ya nani hasa na zinaposema wananchi hawawezi kufa kwa njaa wana maana wananchi wapi au kifo kinapata piccha mbaya kinapotokana na njaa tu au hata ujambazi? Kwa nini viongozi wetu wasitoe ahadi ya wananchi kulindwa na kuwaahidi maisha yao kutoraruliwa na majambazi? Tunangoja nini zile NGO zinazotetea haki za akina mama na watoto, zinafanya nini au kwa kuwa kijana huyu anatoka familia duni? Hata hivyo niwapongeze IPP kwa kukubali kuweka kihabari hiki kiduchu ila tuna kazi sasa ya kuongeza habari hii na kukemea suala hili la kutu kama inavyofanyika huku ughaibuni.
Jeff samahani je waweza kutuondolea hii word verification maana inachosha na kupoteza muda wakati wa kuchangia? Naomba kuwasilisha hoja.
Tarehe: 5:38:00 PM, Mtoa Maoni:-
Tarehe: 8:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Jeff Msangi
Tarehe: 4:50:00 AM, Mtoa Maoni:- mwandani
Moyo wangu uko na aliyetekewa nyara mtoto. Hivi mwanangu akiibiwa nitafanya nini...
Tunakwenda wapi, au ndio tumefika wapi? Tunatekeana watoto nyara Tanzania?
Silaha za moto zimezidi, wananchi pamoja na askari walipotoka siku nyingi tu (Ona ujambazi wa gari la fedha ubungo- maaskari nao wamo)- japo wanasema wanajifunga mikanda kukabili hao majambazi. Safari bado ndefu.
Kitururu unasema unasema kweli, inabidi wapandishe madarasa na kubuni mbinu mpya za kukabiliana nao hawa jamaa. Bila kusahau kuchochea watu warudie maadili ya utu.
Maswali hapa lazima yawe mengi. Si kwako tu Jeff, naamini hata kwa polisi. Tukio la namna hii, ni geni sana Tanzania, huwa tunayasikia ughaibuni na Marekani. Unafahamu fika kuwa polisi wetu wengi amesoma tu kozi fupi za CCM (si zadi ya miezi sita) na wachache wameweza kuvuka hapo, hivyo si rahisi kwao kubaini mkitego ya namna hii. Pili, unajua fika kuwa simu zetu hazidhibitiwi na mamlaka yoyote. Naweza leo kununua line nikakupigia siku, kisha nikaitupa nikanunua nyingine nikakupigia vile vile. Hoja ya mnara. Mnara unaweza kuonyesha tu miko Magomeni, Kariakoo, Posta. je utanitafuta mtaa upi, nyumba ipi, chumba kipi? Labda cha kufanya ni kuweka mtego katika ulipaji wa fedha wanazotaka watekaji. Kama ni akaunti ijulikane ya nani? kama ni kuziweka sehemu anayezichukua ajulikane...