Dunia imejaa majaribu,dunia tambara bovu,maisha yanataka moyo, hujafa hujaumbika.Misemo ni mingi na inaweza ikajaza nyumba. Kwa mara ya kwanza nimeiona habari hii kwenye blogu ya Michuzi.Nikaamua kuifuatilia zaidi.Matokeo yake ni haya hapa. Pichani ni ndugu zetu ambao hivi sasa wanasakwa.Cha msingi.Tusiwahukumu kabla mahakama haijafanya kazi yake ingawa ni wazi kwamba habari hizi hazileti picha nzuri kwa jamii yetu,nchi yetu ya Tanzania.Jamani,kulikoni?






Kaka haka kahabari kametanuka sasa si kwamba ni kadogo tena ni kakubwa mnoo na kanatisha kukajadili sana. Hii ndiyo picha hasa ya Afrika huku ughaibuni? Nini tunafanya na nini wamefanya hawa ndugu zetu? Je kunahitajika kuwalinda hasa walioko nyumbani wasitiwe nguvuni kweli hasa baada ya kuingia katika tuhuma kama hizi? Hapa ndipo wakati hasa wa kucheza karata yako kila jambo lawezekana kama uko makini!