Tuesday, May 23, 2006

JAMANI WATANZANIA!

Dunia imejaa majaribu,dunia tambara bovu,maisha yanataka moyo, hujafa hujaumbika.Misemo ni mingi na inaweza ikajaza nyumba. Kwa mara ya kwanza nimeiona habari hii kwenye blogu ya Michuzi.Nikaamua kuifuatilia zaidi.Matokeo yake ni haya hapa. Pichani ni ndugu zetu ambao hivi sasa wanasakwa.

Cha msingi.Tusiwahukumu kabla mahakama haijafanya kazi yake ingawa ni wazi kwamba habari hizi hazileti picha nzuri kwa jamii yetu,nchi yetu ya Tanzania.Jamani,kulikoni?

4 comments:

  1. Kaka haka kahabari kametanuka sasa si kwamba ni kadogo tena ni kakubwa mnoo na kanatisha kukajadili sana. Hii ndiyo picha hasa ya Afrika huku ughaibuni? Nini tunafanya na nini wamefanya hawa ndugu zetu? Je kunahitajika kuwalinda hasa walioko nyumbani wasitiwe nguvuni kweli hasa baada ya kuingia katika tuhuma kama hizi? Hapa ndipo wakati hasa wa kucheza karata yako kila jambo lawezekana kama uko makini!

    ReplyDelete
  2. Kama kesi hii angepelekewa mwanafalsafa Yesu Mnazareti, bila shaka angewashushua wamarekani kwa kuwaaambia.."kama hamjawahi kuiibia Afrika na muwanyooshee vidole vijana hawa.."

    Jeff nina swali hapa, hivi hizi nchi zinazojiita zimeendelea zinatoa wapi malighafi za kutengenezea kompyuta zao?

    Siwatetei kina Njaidi lakini ukweli utabaki pale pale, nchi za magharibi ndiyo zinazosababisha umasikini Afrika. Leo hii wanaijeria wamefikia tabia waliyonayo kutokana na hayohayo ya kuibiwa malighafi zao.

    Naona umefika wakati sasa kwa Bara la Afrika kulinda mali zake kama wao wanavyozilinda zao na tena tuwe makini na hila zao za kutuchonganisha wenyewe kwa wenyewe ambazo hutuchukulia muda mwingi kupigana huku wenyewe wakiondoka na mali za Afrika.

    ReplyDelete
  3. DaMija,
    Ni kweli kwamba bara letu la Afrika linaibiwa utajiri mwingi sana na hawa wenzetu.Lakini nadhani tunaweza kuwa na njia nzuri zaidi ya kulinda vyetu na kufaidi sisi wenyewe.Wenzetu wanakuja na mikataba ambayo sisi bila kujua/au kwa tamaa za wachache wetu malighafi zetu zinachukuliwa.Wanatudanganya kwamba vyetu si bora bali vyao na mambo chungu mbovu.Hatuwezi kuanzisha mapambano nao kwa kuwa "vibaka".Matokeo ya mtindo huu ni kama haya ya kina Njaidi.

    ReplyDelete
  4. Anonymous2:26:00 PM

    Ni kweli kabisa kama laivyosema jeff hapo chini sio sahihi hata kidogo kupambana kwa njia ya vibaka kisa eti hawa mabepari nao wanaaibia africa, angalia wao wanavyoiba sio kijinga na kipumbavu kama haop vijana walivyofanya na hata hivyo hao vijana hawajaiba kwa maslahi ya taifa waliiba kwa maslahi ya mifuko yao iweje leo waonekane wamefanya la maana

    ReplyDelete