Majira ya summer ndio yashaanza kupiga hodi. Jana joto lilikuwa nyuzi joto 25,leo ni nyuzi joto 31.Hii ina maana kwamba leo hapa Toronto pana joto kuliko Dar-es-salaam. Joto la hapa linakuwa baya zaidi kwa sababu ya kinachoitwa na wanasayansi "humidity".Ukizingatia pia kwamba hapa hakuna "upepo wa bahari unaonukia"(hivi ule pale nyuma ya Aga Khan hospital na Kigamboni ni upepo unaonukia au unaonuka?) basi kajoto ka kukera huwa kanazidi kupamba moto.
Lakini kwa jinsi yeyote ile wenzetu hujua sana kufurahia majira haya.Mtu unatamani wikiendi isiishe.Kila kona ya jiji ni midundo ya ngoma,muziki na pia makelele ya kilevi nk.Nyama choma na masanga ndio usiseme.Ndio raha au karaha ya summer.Huu ndio ule wakati wa "licenced to walk naked".Utaona chuchu na makalio mpaka uchoke.Utahisi watu wote wametoroka "Mirembe".
Jambo moja ambalo nimetokea kulipenda sana wakati huu wa summer ni kuhudhuria sherehe za wahindi wekundu(wenye nchi asilia) zinazoitwa pow wow .Mimi huzipenda sherehe hizi kwa sababu nyingi zikiwemo zile za kuutukuza utamaduni wao. Ni sherehe poa sana hizi na nazisubiri kwa hamu mwaka huu. Pichani ni mwaka jana nilipohudhuria pow wow katika mojawapo ya kambi wanazokaa hawa wahindi wekundu. Wazungu wamewapora jamaa nchi yao.
Jeff umenikuna roho ulipouliza kuwa upepo wa Dar unanuka ama unanukia. Ni mchanganyiko wa kunukia na kunika. Kwa mbaali kuna kaharufu ka samaki. Mengineyo ni uvundo anuai. Si mnajua bado hatujafanikiwa katika maji taka.