
Kama unajua kidogo historia ya Canada basi utakuwa pia unajua kwamba hii ni nchi inayoundwa na Wafaransa na Waingereza ukiachia mbali wenye nchi yao asilia ambao wengi tunawajua kama Wahindi wekundu. Mpaka hivi leo bado wafaransa wanataka kujitenga ili waunde nchi yao huru kutoka katika Canada ya sasa.
Pichani hilo ni jiji la Quebec City ambalo linakaliwa zaidi na Wafaransa.Huko lugha ni bonjour tu. Huo mto unaotenganisha jimbo la Ontario na lile la Quebec(Quebec city imo ndani ya Quebec Province) unaitwa Rideau River ambao pembeni yake inaunda Rideau Canal
Quebec, unaonekana ni mji mzuri sana hasa kwa sisi tusiokunywa pombe ambao tuna muda mwingi wa kufanya shughuli zasizokuwa na maana kwa wanywa pombe.
Ulivyopachikwa pembeni ya mto na majengo yaliyoundwa kwa ufundi wa hali ya juu sana. Nadhani mnayafaidi sana hayo majengo ambayo nyumbani hayapo.
Changamoto ni kuyatengeneza hapa nyumbani.