
Kila ijumaa jioni mimi hupata muda wa kukutana na vijana wadogo ambao aidha wao wenyewe wanatokea Afrika au wenye asili ya Afrika.Mojawapo ya shughuli za kitamaduni ambazo huwa tunazifanya ni ngoma. Ngoma bwana huwa kama sala wakati mwingine.Mimi hupenda kusema ngoma ni "meditation" ya kutosha sana kwetu sisi waafrika.Ukiusikiliza mlio wa ngoma kutokea moyoni na sio kichwani basi mwenyewe utaniambia kama kuna dawa ya asili nzuri kuliko hii.
Mtu asiyejua na kuthamini historia na tamaduni zake asilia ni kama meli isiyo na rada.Huishia pembezoni mwa bahari nyeusi.Pichani ni baadhi ya vijana wangu wakiwa wamepozi na ngoma.Ngoma hizi zilitoka pwani ya Afrika ya magharibi.
Zemarcopolo,
Kwa bahati mbaya sana nina kijana mmoja tu wa kitanzania kwenye kundi hili.Ila mganda huwa unapigwa.Marehemu Hukwe Zawose ndio anatuhamasisha na ngoma za kwetu.