
Kila ijumaa jioni mimi hupata muda wa kukutana na vijana wadogo ambao aidha wao wenyewe wanatokea Afrika au wenye asili ya Afrika.Mojawapo ya shughuli za kitamaduni ambazo huwa tunazifanya ni ngoma. Ngoma bwana huwa kama sala wakati mwingine.Mimi hupenda kusema ngoma ni "meditation" ya kutosha sana kwetu sisi waafrika.Ukiusikiliza mlio wa ngoma kutokea moyoni na sio kichwani basi mwenyewe utaniambia kama kuna dawa ya asili nzuri kuliko hii.
Mtu asiyejua na kuthamini historia na tamaduni zake asilia ni kama meli isiyo na rada.Huishia pembezoni mwa bahari nyeusi.Pichani ni baadhi ya vijana wangu wakiwa wamepozi na ngoma.Ngoma hizi zilitoka pwani ya Afrika ya magharibi.
Zemarcopolo,
ReplyDeleteKwa bahati mbaya sana nina kijana mmoja tu wa kitanzania kwenye kundi hili.Ila mganda huwa unapigwa.Marehemu Hukwe Zawose ndio anatuhamasisha na ngoma za kwetu.
ebwana umenikuna sana na khabari ya kucheza ngoma kila ijumaa kwani mie nafanya hivyo kila siku hiyo hapa dar pale nyumba ya sanaa. na nimeanzisha kampuni kapitoletaz entertainment itayoshughulikia masuala ya ukuzaji sanaa, na makao yangu nahamishia ambassador plaza (zamani gogo hotel) pale morroco. kila ijumaa nataka watu wale sindimba. ngoma kama hiyo nami nnayo chumbani. kanitengezea mbunju wa simba theatre.
ReplyDeleteNi kweli Mh.Jeff huwezi kuzungumzia tamaduni za mwafrika bila kuhusisha vitu muhimu kama vile ngoma.Ngoma inahusishwa na uhai katika jamii ndio maana mbali na burudani ngoma ina maana kubwa sana katika mambo mbali kama vile matibabu.Ili kujua kwa mfano namna ngoma inavyotumica katika matibabu katika africa na Tanzania kwa ujumla jaribu kutembelea(kusoma) kitabu hiki:
ReplyDelete"The Quest For Fruition Through Ngoma: The Political Aspects Of Healing In Southern Africa. Oxford:Kimehaririwa na kuandikwa na James Currey.
Katika kitabu hiki kuna mambo mengi ya kuvutia hasa kutoka katika makabila ya wanyamwezi na wasukuma.Nilipigwa na butwaa kujua kwamba ndani ya makabila ya wanyamwezi na wasukumuma pekee kulikuwa na aina zaidi ya 107 tofauti za ngoma.kwa leo sijui zipo aina ngapi!
Nafikiri mpango alio nao nd.Michuzi ni mzuri sana na ninaamini kwamba kwa njia hiyo utaweza kudumisha utamaduni wa ngoma kwa kiasi kikubwa.