
Mwaka huu kongamano la kimataifa la ukimwi linatarajiwa kufanyikia hapa Toronto,Canada. Ninatarajia kushiriki kikamilifu. Kuanzia ijumaa iliyopita nimekuwa nikihudhuria kongamano zingine ndogo ndogo za kijamii...hususani za watu weusi wanaotokea Afrika na wale wa visiwa vya Caribean hapa Ontario. Kongamano hili limefanyikia kwenye hoteli ya Ramada hapa Toronto(pichani kulia)...picha za ndani ya kongamano na vyombo vya habari vilikuwa marufuku ndio maana picha niliyoambulia ni hii ya nje.
Ni wazi kwamba vita dhidi ya ugonjwa huu bado haimthamini vilivyo mtu mweusi. Hapo ndipo tumekuwa tukiongelea kujikomboa sisi wenyewe,kusaidiana sisi wenyewe na pia kuacha kutegemea "huruma" za wenzetu. Chini kabisa ya moyo wangu naamini tunaweza.Tunachotakiwa kufanya,hapa ughaibuni na hata kule nyumbani ni kusema hapa,imetosha. Tuachane na tabia ya kutegemea na kusubiri mpaka tusaidiwe basi ndio na sisi tuonyeshe kwamba tunaweza.
Maswali ambayo ninajiuliza hivi sasa kabla ya mwezi wa nane ni kwamba nini kitabadilika baada ya mkutano kama huu unaokuja ambao maandalizi yake hugharimu mabilioni ya dola ambazo zingeenda kwenye elimu na uwezeshwaji kuhusiana na mbinu za kupambana na ugonjwa huu? Nafasi za wewe kushiriki kwenye kongamano hili nadhani bado zipo. Angalia kwenye tovuti hii hapa uone kama utaweza shiriki nasi hapa. Ukikubaliwa, malazi na usafiri wa kwenda kwenye mkutano niachie mimi.
Mwisho je unamkumbuka Philly Bongole Lutaaya? Tunao bado watu maarufu wenye moyo kama wa huyu bwana?
Jeff namkumbuka Phili Lutaya na kibao kile moto moto I was Born in Africa. Kama kuna mtu anaweza kuniweka kwenye mtandao au kunisaidia nikipate jamani anisaidie maana lile rege lilinikuna sana nyakati hizo na kila nikirejea maneno kama Iwas born to dance, dance music and singo songs, au music is a topic today na mengine yaani namkumbuka sna shujaa huyu wa Uganda. Huyu nikifananisha na Tanzania katika Muziki namuweka kundi la Kalikawe na lile songi la Nichakwizuka! Yaani we acha tu, watu ufa muziki hubaki na kuishi milele.