Ajali hii ilitokea mwishoni wikiendi mbili zilizopita karibu kabisa na nyumbani kwangu. Kama kuna jambo ambalo polisi wetu wa Tanzania,zima moto na wana vimulimuli (ambulance)wanaweza kujifunza basi ni kujaribu kufika kwenye eneo la tukio haraka iwezekanavyo. Hii huwa inawezesha kuokoa maisha ya watu,kulinda mali za wanaopatwa na ajali(vibaka hata huku wapo aisee) na pia kuweza kupata ushahidi wa haraka na makini kuhusiana na ajali yenyewe. Kwa bahati mbaya pamoja na juhudi zote za waokoa na walinda maisha hawa watu wawili,mtu na mpenzi wake,waliokuwa kwenye hiyo pikipiki walifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali. Hapo binadamu anakuwa hana ujanja,ni mipango ya mungu.
Yote hayo tisa..hivi moto ukitokea charambe au boko, zima moto la pale Upanga litafika saa ngapi?Hivi jiji la Dar-es-salaam lina kituo kimoja tu cha zimamoto?Serikali inaposema inajali usalama wa wananchi wake huwa inazungumzia usalama gani?
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:55 AM | Permalink |