Kama wewe ni mfuatiliaji wa matamasha makubwa ya ngoma duniani basi si ajabu ukawa umewahi kusikia kuhusu tamasha linaloitwa Muhtadi International Drumming Festival. Wenyewe hulinadi tamasha hili kama dunia ya kimataifa inayounganishwa na ngoma. Basi kuanzia leo jioni,kesho na keshokutwa mlio wa ngoma utavuma vilivyo hapa Toronto kwani tamasha hili ndio limewadia tena.
Jina la tamasha hili linatokana na jina la mwanzilishi wake ambaye ni Muhtadi, mzaliwa mweusi wa visiwa vya Trinidad & Tobago aliyehamia hapa Canada mwaka 1974.Yeye ni mmojawapo ya watu waliosema, fanya yote lakini usichezee utamaduni wangu,huo niachie. Lakini hakuishia hapo tu,akasema popote pale ngoma inapochezwa basi nanyi njooni tumcheze mwana pamoja. Ndio mwanzo wa kuwa na ngoma za mataifa mengi namna hii.Nina hamu sana ya kushuhudia ile ngoma kubwa ya kichina. Ukitaka kujua majina na habari za makundi yatakayotupa burudani katika tamasha hili la aina yake basibonyeza hapa. Kama kawaida siwezi kosa tamasha kama hili hivyo nitakuwepo. Pichani ni ngoma ijulikanayo kama dono kutoka Ghana. Ukitaka kuona mapicha zaidi ya tamasha hili mwaka jana bonyeza hapa.
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:40 PM | Permalink |
Jeff,
Lipo jambo tunaloweza kulifanya siku za usoni kuhusiana na tamasha hili. Naomba tuwasiliane.
Vipi? Uliipata barua pepe yangu?
Asante,
F MtiMkubwa Tungaraza.