Kwa bahati mbaya au nzuri umeficha jina lako.Sio mbaya kwani huo ni moja ya mitindo huru ya kujielezea.Wakati mimi siandikii gazeti la Mwananchi(huwa nina makala kila jumapili Tanzania Daima) ni wazi kabisa hoja ya vyuo vyetu kuzalisha manamba inaweza kuwa ilitoka kwangu kwa sababu naamini kwamba huo ni ukweli.Ni wazi kwamba vyuo vyetu havimfundishi mwanafunzi kuwa mbunifu ili baadaye aweze kujitegemea,kuanzisha chake,kuwa na ujuzi wa kugundua mambo mapya na sio kubobea kwenye sayansi za kina Newton na Abbot tu.Ndio maana kauli ni kwamba "soma ili upate kazi" kwa maana nyingine soma ukamtumikie mtu,sio usome ili ukajitumikie wewe mwenyewe,ili uboreshe jamii yako.Siku hizi ndio mambo yanazidi kuwa magumu kabisa,mwanafunzi anafanya mtihani wa "alternative to practical".Anasikia kuhusu test tubes wakati hajawahi kuziona.Unategemea huyu anaandaliwa kuwa nani?Chunguza vizuri hao unaosema wanafanya kazi za kuheshimika NASA au Erickson.Chunguza je,walitoka vyuoni kwetu moja kwa moja mpaka huko au walipitia mahali kupigwa msasa?Ahsante kwa mchango wako.
Jeff, hapo Toronto kila siku kuna matamasha ya kitamaduni nini?
Togo wametoka, lakini Ghana wametupa fahari ya kutosha. Nasikia Marekani wamechukizwa kiasi ambacho Joji Kichaka anataka kuiwekea Ghana vikwazo!