VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, July 16, 2006
DAR ZIPO MBILI?
Kijasho chembamba kinatoka,leo jua limewaka kwelikweli.Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kwamba ukiona jua limewaka namna hiyo ujue malaika aliyeko zamu ya kuwasha na kuzima jua kwa siku hiyo ana roho mbaya sana,au pengine ni mlevi na pombe ya jana bado haijamtoka kichwani hivyo kalala na kusahau kurekebisha mambo. Alah! kumbe malaika nao wako namna hiyo jamani?

Kituo cha mabasi Mwenge, leo kimejaa watu ile mbaya.Naambiwa eti wengi wanaenda downtown kutafuta riziki.Mbona naona kama wameshachelewa?Mchana wote huu jamani,kwani nyie hamuamini kwamba biashara ni asubuhi,jioni mahesabu?Aaa wapi..mbona kanuni za dunia ya leo zinasema biashara jioni,watu wakishatoka makazini?

Leo nimeamua kuchukua njia hii ya kutokea Mwenge baada ya jana kutumia ile ya Ubungo..au barabara ya Morogoro.Waswahili bwana..mpaka niseme Morogoro Road ndio nitaeleweka.Rafiki yangu Ndoga anayeishi huko Uholanzi(nchi ya aina yake hii..ukitaka kuwa bwabwa sawa tu,ukitaka kuuza mwili wako poa tu,ukitaka kula uroda kwenye bustani za jiji twende tu,ukitaka ku..twende tu..ama kweli) kaniambia jambo ambalo sina budi kulithibitisha kwa macho yangu na akili zangu chache.Kasema eti ukielekea mjini kwa kutumia Moro rd na ukitumia hii ya "mzee ruksa" eti utaona jinsi gani Dar ni jiji moja lenye tabaka mbili tofauti.

Labda nianze na nilichokiona jana.Taa ya kijani inawaka,konda anamuamuru dereva akanyage mafuta.Mpiga debe wake anakimbiza gari,hajapewa ujira wake wa kupayuka(hivi ina maana Dar watu wengi hawajui kusoma nini?Sasa kwanini mtu apasue mishipa namna ile?) Duh,karibuni jamaa akanyagwe aisee..hivi kwanini? Naona wananchi kibao pembezoni mwa barabara,naambiwa hawa ni wafanyakazi wa viwanda kama UFI na URAFIKI..ama kweli..kwanini viwanda hivi viwe karibu namna hii na makazi ya watu?Hali ya hewa je?Hapa si ndio Shekilango..pale kwa Lowassa majuzi?Hivi nani karekebishwa? Mara tunafika mahakama ya ndizi...kama huna koo jepesi unaweza rudisha chenji(yaani unaweza tapika).Kwanini ndizi ziuzwe namna ile?Hivi wachaga na wahaya wanajisikiaje wakiona chakula chao kikuu kinadhalilishwa namna hii?

Tunafika Manzese..hii ndio Kibera au Mathare ya Tanzania. Eti kuna mtu anaitwa afisa mipango jiji hapa.Naona kale kanjia ka kuelekea uwanja wa fisi(kama hupajui shauri yako). Hivi vijana wote hawa ni wachuuzi wa mitumba? Mbona basi uwiano ni kila kijana mmoja kwa mtumba mmoja? Naanza kuvuka daraja maarufu la Manzese..naliangalia naona "masela" wameweka chata...Barcelona! Hata sielewi Barcelona na Manzese ina uhusiano gani.Sishangai sana..mbona mbele kidogo ni Manzese Argentina? Maradona..okay.

Naendelea kukata mbuga...Kagera,mwembechai..hali ni zilezile..wazee nje wanacheza bao.Vijana wanajaribu kuchuuza kila wanachoweza..kila tunaposimama wauza maji,nyembe,turi nk wapo madirishani.Survival for the fittest..ushawahi kuiona hiyo senema? Naingia mitaa ya jangwani sasa...ama kweli...naziangalia kwa chabo nyumba za wananchi wenzangu. Maisha.

Leo sasa,gari inakamata Ali Hassan Mwinyi,kondakta kasimama mlangoni,mlango kafunga vizuri kabisa.Ohh kumbe gari hili lina kiyoyozi bwana! Kila abiria amekaa kwenye kiti.Naona watu wana sura tofauti huku.Wengine wanasoma magazeti ya mchana...nachungulia naona kichwa cha habari..kama kawaida..Kikwete na Lowassa kiboko.Sina sababu ya kununua gazeti nadhani,habari ni zile zile.Tofauti na jana naona upande huu watembea kwa miguu ni wachache.Kila kituo naona wakinadada warembo wanasubiri usafiri.Wakiingia kwenye gari,mashalah..manukato! Huku naona ofisi nyeti za kiserikali.Naona taasisi ya kukuzia mitaala(mitaala gani,sijui..mbona mambo ni yale yale?),naona tvt,ooh nyuma tushapita makao makuu ya habari Tanzania(aipipiii)..duh hata chuo cha posta kipo huku...alah..hata tume ya sayansi kumbe?

Mbele nakuta kituo cha mafuta chenye pampu nyingi kupita vyote afrika mashariki..hivi ni kweli? Lakini nyuma tumeshapita majengo mazuri na ya kisasa kabisa hapa Bongo.Hata wazungu(sio kwamba wao ni watu zaidi yetu) nawaona kibao huku.Ndani ya magari mazuri wakati wengi wao "vihiyo" tu. Naona kituo cha polisi..oysterbay! Duh huku watu wanauza maua rozi...huku ni nchi nyingine bwana.ati.Kule kwa jana..thubutu...nani wa kununua maua?Nipo mbuyuni..nakumbuka Kessington Market kule Toronto..jamaa anauza vitu vya anasa..vya watalii.Natamani nishuke..hapana nitashuka siku nyingine.

Nashangaa mahali pako kimya namna hii..sorry nilisahau kwamba hapa ndio Oysterbay penyewe,wanapokaa we... wa nchi hii.Kwa mbali nasikia mbwa anabweka. Fanya fujo uone..naona balozi za nchi za wenyewe zilivyojipanga. Bahari hii hapa...duh beach la Barcelona hili nini?

Las Vegas Casino..wait..hivi nipo wapi?California Dreamer..you must be kidding me! Mbele yangu nauona mtaa wa mabenki..benki zote za nje hizi..Namwambia konda anishushe hapo Delinews..nataka kumsalimia Michuzi. Ama kweli..hivi hii ni Dar moja au mbili?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:21 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 6:18:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Christian Bwaya

    Mimi nafikiri ukichunguza kwa makini sana utagundua kuwa Dar ziko tatu. Na pengine zikawa nne. Hebu endelea kutembea tembea bwana Jeff unaweza kulibaini hilo. Nisizitaje Dar hizo utajionea mwenyewe. Azawaiz karibu sana!

     
  • Tarehe: 10:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    jEFF KAZI NZURI ILA UNAPOONGANISHA SAFARI MOJA KUELEKEA NYINGINE UMESAHAU MTIRIRIKO mzuri wa kututoa barabara ya Manzese na kisha kutuleta tena ya Posta, otherwise ni kazi inayofurahisha utadhani ulikuwepo Bongo. hUU NDIO UBAYA WA bONGO, HAPABADILIKI YAANI UNAWEZA KUKUTA HAYA HAYA BAADA YA MIAKA KUMI NA TANO IJAYO.

     
  • Tarehe: 9:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Malaika kalewa pombe, au pombe ya kienyeji? maana Dar ziko nyingi sana! Hujatuambia jinsi barabara ya Lowassa inavyojengwa kwa kutumia teknologia ya kizamani sana, siamini kama katika karne hii barabara yenye kutumiwa sana iwe na njia moja kwenda na nyingine kurudi, tunatamani kuona "highway".
    Ulipofika manzese kwanini hukukata kushoto au kulia, kwani hukuona watu wengi wanaelekea huko? Umekosa uroda!
    Juzi na jana watu wa ITV walijaribu kuionyesha umma mambo ya uwanja wa fisi ,ambao ulipita karibu yake lakini uliogopa kama wengi kuingia kujionea na kujumuika, kilikuwa ni kioja kikubwa sana kwa wengi.
    Uholanzi kila kitu ni ruksa kuliko alivyokuwa anaturuhusu mzee ruksa, lakini huku pia kuna mambo ambayo hakuna aliyeyaruhusu lakini yanafanyika waziwazi bila serikali kkuingilia.
    Nchi hii ni ya wakulima ,jaribu kuongeza umbali wa safari yako labda kuelea morogoro au rufiji ujionee uwiano wa wafanyabiashara ndogondogo na wakulima.
    Tembea ujionee. Hongera kwa kupanua mijadala.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker