VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, July 27, 2006
HII NI NJAA,TAMAA AU UKWELI NA MUHIMU?
Nimekutana na habari hii leo asubuhi, nimeshindwa niseme nini,niongee na nani,nimlaumu nani au hata nimpige nani konde. Hivi kwanini lakini,kwanini kwa jina la Tanzania ambayo si mali ya mtu mmoja bali wananchi wote,wakuzaliwa na wakuletwa toka bara hindi na kokote duniani?

Alichokifanya huyu ni tofauti na kile alichowahi kukifanya Emil Muta? Inabidi serikali iunde sheria mpya ya matumizi ya jina la nchi kwa faida binafsi? Hivi kwanini jamani?Hebu nisaidieni kwa mawazo hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 9:51 AM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 8:49:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff nikupe pole sana kwanza! Sasa niingie katika hoja hivi ni nani anaandika ukweli kuhusu Afrika? Hizi ni makala tatu mfululizo nilizowahi kuziandika nyumbani gazeti la Mwananchi.

  Je Tanzania inalingana na nchi za magharibi? Je namna hospitali za nchi tajiri na vyyombo vilivyomo hufanana na vya Tanzania? Je wakati vinatupwa ni aibu kuviomba ili vipelekwe katika jamii inayovihitaji? Nini maana ya mitumba?

  Jeff, suala si kutumia jina la Tanzania au kudanganya ili kupata misaada. Wenye imani kama zangu tusiopenda misaada kabla ya kufanya nguvu zetu tupo kundi lingine lakini pia wenye kudhani misaaada pekee ndiyo itaweza kunusuru nchi zetu unadhani wafanye nini kuvutia misaada hiyo? Na wanapozungumza masuala yaliyo wazi na kweli je wanadhalilisha? Ni kweli serikali yetu inafanya vema katika afya? Jeff nikuulize wewe...nini maana ya kila kiongozi kwenda kusaka matibabu Ulaya? Je kama mambo yanaendelea huko wanafata nini ughaibuni na siku hizi wanajisifu kabisa kutoa taarifa hizo magazetini? Je hawa hawayapaki matope mataifa ya Afrika kuonyesha namna wasivyoweza hata kuebndeleza husuma za afya katika nchi zao na badala yake wao kutumia madaraka yao kutafuta tiba bora nje?

  Swali lingine kwa sasa ni hizi NGO je tunasoama proposal wanazoandika zina madudu mangapi? Pita kwa Mwandani na kisha soma maongezi na mheshimiwa mgeni utabaini nini nazungumza. Nitue kwa msemo wa Kiswahili usemao, "Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio" Tujadili na tucheze karata zetu kila jambo linawezekana.

   
 • Tarehe: 3:20:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Jeff samahani lakini naona serikali yetu haifanyi kazi vizuri, kama tunaweza kuomba misaada kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu kwa nini tusifanye hivyo? Angalia Israil, unafikiri pesa zote wanazotumia kuendeleza nchi zinatokana na mapato ya nchi yao tu? Mimi naona Tz ikiwa na watu wengi zaidi kama hawa atleast tutapiga hatua. Huyu dada amepata fursa kusaidia jamii ktk sekta anayofanya kazi. Kwa kweli mimi nampongeza kwa ujasiri wake. Harambeee

   
 • Tarehe: 11:10:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Katika proposal ya hao watanzania imeandikwa:

  ”People there commonly live in mud huts and, in many rural areas, without electricity. Running water is a luxury,”

  There are so many problems’ in her homeland, she said. ”Poor infrastructure, poor housing, poor utilities. No clean water. Poor schools, it’s just overwhelming,’

  Katika mistari hiyo kuna ukweli. Hawa watu wamechukua hatua kuomba misaada. Pengine kitu kinacholeta tatizo ni manipulation katika lugha iliyotumiwa kuomba msaada.

  Pengine pia kwa kushindwa kwetu tulioko ughaibuni katika nchi hiyo husika kufanya harambee na kukusanya kipato kuweza kujisaidia kabla ya kuomba wafadhili ambao kutokana na stereotypes wametumia lugha ya kudhalilisha. lugha ambayo inafanya kazi ukiwa unaomba. baniani m'baya kiatu chake dawa.

  Kama watu wangejumuika na kukusanya kipato kusaidia wangekuwa na ownership ya namna fulani ambayo ingesisitiza uwajibikaji katika huo mradi wa vitanda. lakini kama mimi binafsi na mke wangu tufanya jambo ownership inakwenda kwetu, chances are tunaweza kufanya tutakavyo.

  Nimewahi kufanya kazi katika sehemu inayosaidia wakimbizi wanaongia ughaibuni. Ndugu zangu wa kutoka Afrika saa nyingine hata wakijua kimombo huwa wana-act kama hawajui, ikesha husema mengi mengineyo si ya kweli ili kuwafanya wafadhili wamwage pesa na misaada. Manipulation. Manipulation inayoendeleza taswira ya mwafrika kama mtu aliyeshindwa kabisa kujisaidia.

  hasira inabaki pale pale kwa kushindwa kwetu kushirikiana na kufanya mambo ya maana.

  NB: Suala la Israeli pengine ni la kisiasa zaidi geopolitics fulani. China pia ni nchi ambayo imekuwa ikipokea sana misaada kwa sababu hizo hizo za kisiasa.

   
 • Tarehe: 5:38:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Jeff hiyo mijamaa mitatu hapo juu imenisemea. Kwan za habari za sikunyingi.

  Manipulation kama alivyosema mwandani hatitakiwi na pengine ipigwe vita. Lakini kama lengo hasa ni kufikisha misaada kunakohusika natamka hadharani kuwa Mungu awazidishie moyo wa huruma ndugu hawa.

  Wakina Oweya ndio wale watanzania wasiokumbuka kwao na kukaa kwao nje kumefanya wasahau walikotoka. Kwa muda mchache niliokaaga Marakani niligundua kuwa wao huita spedi spedi na sio kijikokikubwa. Maneno waliyotumia katika kupeleka ujumbe ndio hasa sahii kwa hali halisi iliyopo Kajunjumele na kwingineko Tanzania.

  Jana Radio One walikuwa na habari ya mrundikano wa wagonjwa katika Muhimbili hata wengine kulala wawili-wawili na wengine chini kabisa. Je huyo Oweyo analalamika nini kuwa tunadhalilishwa. Sio hali halisi hii.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker