Samahani wananchi.. ila ilibidi nirudi mara ya 2 kuweka maoni yangu katika maada hii maana kuna hoja 2 tofauti alizogusia kaka Jeff zote amabazo zimenichoma.
Ya kwanza nishatolea maoni na nii hii ya ushabiki wa kisiasa na mambo ya kudandia behewa la "Kikwete Bomba, Kikwete wahh"
Sasa nije kwenye jinginelo hili.. hili la kuuza nchi. Dah.. yaani kwanza niseme asalale toba yarabi!! Tunaelekea wapi jamani sie!?
Unajua hii habari kwanza ilinikumbusha nini? ,.... FUNGATE LA LOLIONDOOOO. Sijui ni kwanini kina Mgumia walijiuzulu mwaka '93? Kmumbe mamab haya ni ya "kula usikamatwe" ukikamatwa kivyako!!!??
Eti kakak Jwf.. tuna uhakika gani kuwa Ml. Kilimanjaro haumilikiwi na mzungu nao? ..au mbuga ya mikumi.. au ziwa Victoria, ufukwe wetu ktk bahari ya hindi.... au hata Ikulu jamani!!
Maana kwa mwendo huu sitashangaa kusikia kuwa majumba yote ocean road kuanzia kivukoni mpaka Upanaga (ikiwamo Ikulu tukufu) ishanunuliwa. Tunafanya mambo kienyenji mno na kwa kujuana na kuhongana mno Bongo.
Mtaniwia radhi ila ngoja niwe mbinafsi kidogo... mbuga ya Selous imekuwa kwa muda mrefu ikishika nafasi pekee moyoni maana ndio mbunga ya 1 mi kutembelea. Na katika safari zangu za mara kwa mara kupitia reli ya TAZARA nimekuwa nikipita mumoa na kujionea fahari yetu Tanzania. Sasa suala la kuja kuambiwa leo kuwa yote ile ni mali ya mzungu fulani kwa kweli inakuwa ngumu kuafiki.
Yaani ilikuwaje kuwaje mpaka wakauziana mali waliyopigania babu zetu. Yaani damu ya wazee wetu kina Mkwawa na Bushiri ilikwenda bure kumbe!?
Ilikuwaje kuwaje mpaka uozo wote huu ukaliepuka bunge na vyombo vya habari vya mlengo wa mwongozo (mainstream media). Kama isingekuwa blogu na gazeti huria la huria la Tanzania Daima baadhi ya watu kama mie tungekuwa gizani bado juu ya ubaradhuli huu unaotokea chini ya pua za wananchi.
Jamani jamani nalia na TZ yangu.. kwa mwendo huu tutafika kweli. Huu mwendo wa kuuza nchi ni sawa jamani!? Hii si mikataba walifosiwa kuingia wazee wetu kina Mwenye Machemba na kupelekea wengine kama kina Bushiri, Mangi Sina na Mangi Meli kunyongywa?
Ohoooo tusije siku tukasikia machinga wote anzeni mbele Mtwara yote tushaiuza kwa bepari fulani. Maana hapo binasfsi nitaingia msituni!!
Eeeh mola eeen sijui twaipeleka wap nchi yetu hii. Tusaidies wanao.. maana kwa mwendo huu tutakosa kwetu kwa kweli
Jeff niliskia habari za kupitia mikataba na kisha nikasikia habari za mikataba ambayo haiwezi kutazamwa na hata wabunge bali inaweza kuonwa na serikali. Ilinipa swali kuhusu nani serikali na nani huyo serikali anayeinmgia mikataba ya kuuza nchi na anatumwa na nani na anapewa madaraka hayo na nani? Niliandika katika safu jumapili iliyopita lakini kama usemavyo kuna haja ya kuyatunza haya ili siku za siku zifike tuuulizane maana tumezidi kusifiana bila kufanya kazi za wajibu tulioulilia wenyewe! Lingine ni city water...hiki ni kimbembe kipya kwa ndugu Lowassa anayejiandaa pia kuwania urais baada ya Kikwete!