VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, July 02, 2006
TEKINOLOJIA INAPOWEZESHA!
Mara nyingi sana Ndesanjo amekuwa akielezea na kunadi jinsi ambavyo tekinolojia inazidi kuiunda upya dunia yetu. Jinsi ambavyo tekinolojia inazidi kuwa tishio kwa wale ambao ni wakoloni wa hata habari pia. Tekinolojia za habari kama hizi za blogu, tunazoandikamo masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwa matarajio ya kujenga na wakati mwingine hata kubomoa ni nyanja inayokua kwa kasi sana na mfano mzuri wa mapinduzi haya. Habari ni haki na ni nguvu pia.

Kwa wiki kadhaa hapa Canada pamekuwepo na malumbano makali sana kuhusu imam mmoja wa huko Uingereza anayeitwa
Shaykh Riyadh Ul Haq.Baadhi ya vikundi vya kidini na hata kijamii hapa Canada viliiomba serikali kutomkubalia huyu bwana kuja Canada ambako alikuwa amealikwa aje kutoa mihadhara kadhaa kwenye mkutano wa vijana wa kiislamu ambao unaendelea hapa Canada. Mkutano huo umeandaliwa na The Islamic Foundation ya hapa maeneo ya Toronto.Hoja zao ni kwamba jamaa anatoa mihadhara inalenga katika kujenga chuki miongoni mwa wanajamii nk nk. Jamaa wa uhamiaji waliridhiana na maombi ya wanajamii hao na hivyo kumzuia jamaa asipande kabisa ndege kwa minajili ya kuja Toronto.

Sasa kilichotokea ni kwamba jamaa amehutubia mkutano huo kwa kutumia tekinolojia,akiwa huko huko ofisini kwake Uingereza huku vijana wakimsikiliza kwa utulivu wa aina yake.Leo hii anaendelea kuhutubia mkutano huu na hata pia kuwa na wakati wa maswali na majibu na vijana hao.Upo hapo?Soma zaidi
hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:38 AM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 5:46:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

    Ninafuatilia kwa undani habari na kisa kizima cha shehe huyu. Asante kwa kutuonyesha jinsi ambavyo teknolojia inabadili dunia kama tunavyoijua leo hii. Jambo la msingi ni kuwa watu wenye nia njema hawatakiwi kulala au kuiponda teknolojia pale inapotumiwa vibaya bali kutazama ni jinsi gani nia zetu njema zinaweza kuwezeshwa, kukuzwa, na kusambazwa na teknolojia mpya.

     
  • Tarehe: 3:52:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

    Hii teknolojia inabidi watu wenye nia njema waendelee kuitumia kwasababu kunawatu wenye nia mbovu wanakuja juu ile mbaya. Huwa nawasoma sana watu wa White pride kama hawa:http://finalsolution88.com/ na kila siku naona wanazidi kutumia teknolojia mpya kujipa nguvu.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker