VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, August 02, 2006
KETI TUZUNGUMZE

Ni kipindi cha joto kali sana hapa Canada na hata hapo kwa jirani Marekani. Jana joto la hapa Toronto na maeneo ya jirani lilifikia nyuzijoto 36! Na kwa sababu ya viwanda na mioshi kama inayotoka kwenye magari basi tunaongelea nyuzijoto zaidi ya 40! Tayari watu kadhaa,hususani wazee,washakata roho kutokana na joto hilo.

Kutokana na hilo,sina budi kujikita zaidi ofisini au nyumbani.Uzururaji hauna budi kupungua. Hapo ndipo ninapopata muda wa kusoma mengi,kujiuliza maradufu,kupiga hesabu za mamilioni bila kuwa na senti mfukoni. Hapo ndipo nikakutana na
makala hii hapa, imeandikwa na Magabe Kibiti (simfahamu). Nikahisi damu inanisisimka, msimamo wangu unajulikana. Lakini nikaona huu unaweza kuwa mjadala mzuri sana ndani ya ulimwengu wetu wa blogu. Ndio maana nauweka hapa, wewe unasemaje kuhusu mtazamo huu? Je,ni kweli kwamba hatuna chetu?

NB: Nimekuwekea picha kama kiburudisho tu, picha hiyo ni kutoka tamasha linaloitwa
Caribana. Inasemekana ndio tamasha kubwa kupita yote hapa Amerika ya Kaskazini linalohusu tamaduni za watu wanaotokea visiwa vya Caribbean.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:36 AM | Permalink |


Maoni: 2


 • Tarehe: 8:24:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Nimeitazama makala. Niko mkutanoni. Tusipoijadili hii makala tutakuwa tumepoteza nafasi muhimu sana ya kuzungumzia masuala kuhusu utamaduni wa Afrika ambayo huwa yanaonekana kuwa ni magumu au hayaeleweki.

   
 • Tarehe: 12:19:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jaduong Metty

  Jeff,

  Nadhani mwandishi wa makala hii yuko "on point". Tatizo letu (nazungumzia WaTz kwa ujumla)tunapenda kubeba mambo kiujumlajumla bila kufanya tathmini. Sipigii debe "relativity" ambayo nayo imezidi sana huku magharibi, bali nadhani waTz wengi hawana uwezo bado wa kuweka vitu kwenye "right context". Matokeo yake "defenders" wa uAfrika mara nyingi wanatoka kapa. Mwandishi amethibitisha hilo. Mfano mzuri ni baadhi ya wabunge wanaopigia kelele mashindano ya urembo. Wanaifanya haya mashindano kama dhana iliyoletwa na akina Lundega in 2000, bila kutazama ukweli kwamba haya majamboz yalikuwepo Tanganyika na Z'bar enzi hizo.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker