VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, August 29, 2006
MAZISHI YA BAADHI YA BLOGU!

Zipo siku ambazo hunipa huzuni sana,zipo siku ambazo hunipa furaha sana,zipo pia siku ambazo sizielewi.Nikihoji kuhusu siku nisizozielewa huwa naambiwa nimechanganyikiwa au naanza kuchanganyikiwa.Wanaosema hivyo wananiambia niwe na furaha au masikitiko tu kama binadamu wengi. Sijui nisikilize la nani.

Leo nipo msibani,namalizia kufukia kaburi.Mchanga wangu ni tekinolojia na bahati nzuri ninaowazika hivi leo wanaweza kufufuka,kama wakipenda. Niliwahi kuisikia
tekinolojia ya bloglines ziku nyingi sana zilizopita. Niliheshimu mantiki yake,niliheshimu pia falsafa ya kuokoa muda iliyotumika. Lakini kwa muda mrefu huo huo sikuona umuhimu wake. Huruma ilinijaa.

Leo nimefikia mwisho.Nimechoka kufungua baadhi ya blogu kwa takribani miezi sita bila kukuta lolote jipya.Ukiwauliza wamiliki wa blogu hizo wanadai wako bize.Walipozianzisha blogu zao waliomba kwa nguvu zote watangazwe,wakaahidi kutoa changamoto kubwa uwanjani,wako wapi? Uhuru usiokuwa na majukumu umerudi tena? Hapana bwana,nimechoka.

Sasa leo,baada ya tafakuri nimeamua kuanza rasmi kutumia tekinolojia ya
bloglines.Kama hujaandika kitu hutonisikia,hutoniona kijiweni kwako.Hata kama umeleta bangi ya Malawi,sitaki. Huu ndio msiba wa leo.Nazizika baadhi ya blogu,zile zisizoandika kitu,zile ambazo nguvu ya soda ilishaisha.Ni ukweli,usikasirike. Naamini kwenye nguvu ya habari,naamini bila nguvu hiyo ambayo wenzetu wazungu wanazidi kukomaa nayo,hatutafika,tutasahaulika.Mtanisamehe ndugu zangu msioweka chochote kipya kwenye blog zenu. Kwaherini kwa sasa,mkitaka kufufuka nitakuja kuondoa saruji.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:44 PM | Permalink |


Maoni: 5


  • Tarehe: 5:57:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff, da! hawa jamaa wa Bloglines naona inabidi wakulipe maana umeelezea vizuri sana kwanini teknolojia kama hiyo ni muhimu. Kwahiyo jamaa watakusikia kwenye bomba tu, sio? Yaani hata kama ni "jani"la Malawi? Je la Iringa?

     
  • Tarehe: 2:22:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mzee wa mshitu

    kaka yaani hapo unakuwa kama vile umegundua 'almasi' ya mwadui , haya mamneno ulosema hakina ni mazito sana nakumbuka kaka ndesanjo aliandika wakati fulani kuwa 'wanaodhani blogu ni upepo wa kupita shauri yao' haya sasa mambo yanawadororea. Usichoke kaka wewe sasa naweza kusema ni nabii wa blogu endelea tu kutuamsha usichoke.

     
  • Tarehe: 4:00:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Naona kwanza ungewashauri hao walio "bize" wazifute blogu zao kama wameshindwa kuziendesha wasiwe kama serikali na shirika la UDA, kumbuka zile siku wanamiliki ikarus kama mia na leo wana isuzu lori/bus kama kumi tuu!, ili wasiotaka kuonekana wabaya wasiwe wanapoteza muda wao kufungua nyumba zisizo na wakaaji badala ya kuingia kwenye harakati zilizo motomoto.
    Waache ngoma wacheze wanaoiweza.

     
  • Tarehe: 9:34:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Hakuna kuchoka,hakuna kulala au hata kusinzia.Tukifanya hivyo tunaonekana tumepoteza muelekeo.Tumepoteza nguvu ya umma.

     
  • Tarehe: 12:06:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger boniphace

    Hakika hapa nanena, sijitupi mchangani
    Nitazidi kuchuana, gazeti tando somani
    Nalia ninapotazama, nyingi zimekimbiani
    Fikra zinanambia, wajibu uko kichwani.

    Waungwana, sina ya kutamka. Nadhani upepo huu unatokana na sababu fulani na kubwa ni hii ya kutotambua kuwa huu ni wajibu tuliojitwisha bila kuomba. Nitashuka na maandishi fulani kwangu, ila tu leo nimesoma gazeti moja likionyesha nafasi ya mmiliki wa gazeti tando hasa wakati wa likizo na mapumziko. YEYE HUKAA LA KOMPYUTA NA KUDODOSA HABARI maana wasomaji hawaendi likizo. Siku njema waungwana.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker