Tekinolojia inakua kwa kasi sana. Huu ni msemo mpya,wa kizazi hiki ambacho wengine tunakiita cha .com. Mwanablog mwenzetu Ndesanjo Macha ni mmojawapo ya wanablog ambao wamejikita sana katika kuhakikisha kwamba habari za tekinolojia mpya,hususani kwenye ulimwengu wa habari na mawasiliano hazitupiti. Kila mara unapopitia tovuti yake utakuta ameweka habari zenye mtizamo huo wa tekinolojia.Kwa mfano habari hii na nyinginezo nyingi.
Naamini kwamba wengi hupitia tovuti kama hii ya Ndesanjo na nyinginezo nyingi kwa minajili ya kupata habari za tekinolojia. Mojawapo ni watu kutoka kule Columbus,Ohio (nakumbuka Ndesanjo aliwahi kuishi Ohio) Hawa wameikumbatia tekinolojia ya podcast kwa kasi ya aina yake. Radio Butiama inayoendeshwa na Deus Gunza aliyeko huko Columbus,Ohio ni mfano mzuri wa tekinolojia hii.Ukitaka kusikiliza baadhi ya matangazo yake yakiwemo mahojiano na watu kama mwanamuziki Cosmas Chidumule au mpiga picha maarufu,mwanablog mwenzetu Issa Michuzi bonyeza hapa. Kwa kujua zaidi jinsi gani tekinolojia hii ya podcast inavyofanya kazi bonyeza hapa.
Hii ni babu kubwa mzee.Mimi bado sijaifanyiakazi, lakini naifuatilia kila siku. Lakini kwako Mzee jeff na kwa Mzee Ndesa napitia kila siku. Si muda mrefu utastukia tu navyotumia teki hii.
Asante kwa changa moto za kila siku