
Mkutano wa 16 wa Ukimwi kwa mwaka 2006 umeanza rasmi jana hapa Toronto,Canada. Zaidi ya washiriki 24,000 kutoka kila pande ya dunia,ikiwemo Tanzania wanashiriki mkutano huu. Ujumbe wa mwaka huu ni kwamba "muda umewadia",wakati wa kuonyesha uwajibikaji kwa vitendo ndio huu. Ninahudhuria baadhi tu ya kongamano nyingi zilizoko kwenye mkutano wote ambao utafanyika kwa takribani wiki moja. Pichani ni jana kwenye uzinduzi rasmi ambapo watu mashuhuri kama Bill Gates na mkewe Melinda, mwanamuziki Alicia Keys, mwigizaji wa sinema wa Hollywood Richard Gere wa Gere Foundation nk walikuwepo. Uzinduzi huu ulifanyikia ndani ya Rogers Centre hapa Toronto. Nimeandika zaidi kuhusu habari hii kwenye blog yangu ya kimombo!
Jeff,
Baada ya kusoma habari za mkutano huo wa Ukimwi nimekutana na habari inayoshangaza wana sayansi kuhusu watu ambao ingawa wana Ukimwi haumwi. Soma hapa:
http://tinyurl.com/zglmm