VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, September 02, 2006
INA MAANA GANI?

Hiki ni kisa cha kweli.Mchana wa leo,saa za hapa Toronto,nikiwa katika mihangaiko yangu ya kawaida mwishoni mwa wiki nimekutana na dada huyu pichani.Yeye anatokea visiwa vya St.Vincent(mojawapo ya visiwa vya Carribean).Dada huyu aliponiona nimening'iniza kamera begani akanisihi nimpige picha.Kichwani nilitegemea angetoa ushungi wake ili picha iwe maridhawa zaidi au sura yake ionekane.La hasha,alijitega vizuri kabisa na kuniambia "haya piga".Nikampiga picha na kumuahidi kumtumia baadaye kwenye barua pepe yake.Nishafanya hivyo.
Baada ya hapo nikajishtukia nimejawa na maswali kadha wa kadha.Hivi ina maana gani kupiga picha na hata sura yako isionekane? Hivi huyu naweza kumfananisha na wale watu wanaopenda kutoa maoni kwa kutumia kivuli cha anyonymous? Hivi ina maana gani kutoa maoni kwa kutumia kivuli cha anyonymous huku ukiandika kama vile mwenye blog atakutambua? Rafiki yangu
Michuzi ni victim wa watu wa kivuli hiki.Kwa bahati mbaya wengi huvuka hata mipaka na kufurumusha matusi.Hivi ina maana gani? Hivi ni kweli Tanzania ina watu waoga kiasi hicho au ni kweli kwamba Tanzania haiheshimu uhuru wa kujielezea mpaka watu waogope kuweka maoni yao kwa uhuru,bila kujificha?Si 9/12 huwa ni sikukuu ya uhuru?
Kwa namna moja au nyingine,huwa naelewa,kwa mbali lakini,utoaji wa maoni kwa kivuli cha anyonymous.Naelewa suala la uoga,kutokujiamini au kuwa kwenye witness protectionism acts.Lakini wakati huo huo huwa nashangaa,hivi kama tutashindwa kutumia nguvu ya umma,kama blog,kujielezea,bila kujificha,tutasukuma vipi gurudumu la maendeleo?

Bado nasaka majibu kutoka kwa huyu mwanadada kwamba ina maana gani au inasaidia nini kupiga picha yake huku akiwa ameficha uso?Niambieni wenzangu.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:57 PM | Permalink |


Maoni: 11


  • Tarehe: 7:38:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Simon Kitururu

    Mimi sioni kuwa tatizo kwa watu kujificha identity.Naamini ni haki ya kila mtu kusaidia kimawazo bila kujulikana.Nisichopenda ni kwamba watu wakiwa wanatukana wakati wanajificha. Mimi ningependa mtu anitukane face to face.

     
  • Tarehe: 9:30:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Simon,
    Hata mimi najaribu kukubaliana na utoaji wa maoni bila identity rasmi.Tatizo langu ni kwamba kama tunataka kujenga civil society mpya ni muhimu kujuana,kutambuana juu ya misimamo yetu na hata hulka zetu.Mambo hayo tunaweza kuyajua kwa kujaribu kutoa maoni bila kujificha labda pawe na ulazima sana wa kufanya hivyo.Kutumia kivuli cha anyonymous na kutukana nadhani sio ustaarabu kabisa.

     
  • Tarehe: 6:26:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Unajua Jeff, nimekuwa natazama sana watu wanaotoa maoni wakiwa wamejificha nyuma ya mbuyu au nyuma ya banda la kuku. Basi katika kutazama tazama sijaona hata wakati mmoja maoni ambayo unaweza kusema kuwa mtu huyo alikuwa na haki ya kujificha ili kutekeleza haki yake ya kujieleza. Kunaweza kukawa na mazingira ambayo sio vyema mtu kujitambulisha. Lakini mazingira hayo hayajajitokeza katika blogu zetu. Mazingira hayo ni kama vile hofu ya kutiwa matatani kwa kusema ukweli au kufichua uovu. Inawezekana mtu akawa tayari kufichua uovu ila kwasababu za kiuchumi, kisiasa, na kisheria akawa hayuko tayari kujulikana. Hii huwa inatokea hasa nchi zenye udikteta uliokomaa ila katika viwanja vyetu ya majadiliano, elimu, na burudani haijatokea. Wanaotoa maoni huku wamejificha unakuta wanatoa maoni kuhusu mambo ya ajabu ajabu na kutukana na kushushiana utu. Watu hawa hawakosekani kwenye jamii yoyote ile. Watakuwepo. Tuwaelimishe, wako watakaoelimika na wengine watabaki walivyo. Sisi tuendelee kwenda mbele.

    Kama Jeff ulivyosema, kama kuna ulazima wa kutoa maoni ukiwa umebena nyuma ya choo, basi watu wafanye hivyo. Ila sio kujibana nyuma ya choo kwakuwa mambo unayosema unaogopa watu wakijua ni wewe umeyasema kwani watakudharau.

     
  • Tarehe: 4:46:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    kwa maoni yangu, mie sina neno na mtu kuficha identity yake, na uzoefu (wangu) umeonesha kwamba wengi wanajiona huru wakiwa nyuma ya choo, hasa wale wenye kuosha vinywa kwa matusi na kashfa.

    kuna wakati nilijaribu kuruhusu members tu, nikakuta maoni yanapungua, maana aidha wengi hawana blog ama hawajui namna ya kufungua blog ama ni wavivu na juu ya yote nahisi wanaogopa kujulikana kama ndesanjo ulivyonena.

    nashangaa blog yangu imepata umaarufu kwa kuwa na comments za udaku. yaani kuna mtu kanitumia barua pepe na kunihoji kwa nini nimeacha kuweka picha za masupastaa wa bongo ili wachambuliwe. nikajihisi kama shigongo wa blog, jambo ambalo lanichanganya sana.

    hivi dawa ni nini? kuwaacha watu waoshe vinywa wapendavyo ama tuhamasishe wengi wafungue blog na kujitaja bila kificho?

    nilijaribu pia kufanya mchujo wa post nikakuta ni kibarua kigumu, maana penye post zaidi ya 100 kwa siku inabidi uache kazi ufanye kazi.

    naomba kutoa hoja.

     
  • Tarehe: 8:17:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Sijui kama niko sahihi, Msanii wa kwaito anayenivutia anaitwa Mzekezeke cha ajabu wengi , isipokuwa wanaomjua kabla hajaanza kuimba, hawajawahi kuona sura yake yeye kila siku anavaa "mask" kuficha sura yake walipomuuliza akawauliza wao, hivi hamuoni wasanii wengine walivyopotoka siku hizi? Hiyo lugha yao ya yoo yooh! na vaa yao na matusi waliojaza, sitaki wanizoee sana wasije kuniambukiza vitu hivi?
    Ungemuuliza huyo dada kwanini hataki watu waone sura yake.

     
  • Tarehe: 2:34:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Hi there. Mimi nakubaliana sana na mtu kutoa maoni yake bila kujulikana. Sababu ni nyingi lakini ningependa kusema kwamba wakati mwengine unaweza kutoa maoni ya muhimu sana lakini watu wasichukue maanani kwasababau wakaangalia nani kasema, au wakona ni muhimu kwasababu nani kasema. Mimi naona as long as you have a point na unasaidia jamii it doesn't matter who you are as long as your points is taken. Sasa kuhusu Michuzi kwa kweli wale wanaotukana wanatukana tuu just because. Na huyo dada ana lake jambo...

     
  • Tarehe: 8:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Michuzi,
    Sioni kama kuna sababu ya kuchuja maoni maana utapoteza muda wako bure. Pia sioni sababu ya kuweka kizingiti ili kila anayetoa maoni awe amejisajili kwenye huduma ya blogger, hii itazuia mtu anayetaka kutoa maoni harakaharaka bila kulazimishwa kuanza kujisajili wakati ambapo hana nia ya kuwa na blogu.

    Jambo tunaloweza kufanya kwa maoni yangu ni kuwaacha na sisi tuendelee na kazi zetu na majukumu yetu ya kuendeleza uwanja huu wa habari, sanaa, maarifa, elimu, na burudani. Tuwaache watajichuja wenyewe. Michuzi, kamata kamera yako wala usiwafikirie tena kuanzia leo hata milele. Huenda wanapata afya wanapojificha nyuma ya choo ili kuonyesha uwezo wao wa matusi na kashfa. Waache. Sisi tuendelee. Tunajua tunafanya nini. Blogu yako inagusa watu wengi sana, hawa wachache wala wasitukoseshe usingizi. Faida za picha unazotupa ni kubwa mno ukilinganisha na hasara ya kuwa na maoni ya ajabuajabu.

     
  • Tarehe: 2:47:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Ahsante Ndesanjo kwa sio tu maoni bali njia na muelekeo juu ya utoaji maoni.
    Nadhani kufanya unachotakiwa kufanya ndio la msingi sana.Tuendelee.

     
  • Tarehe: 9:03:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    nakumbuka nilipokuwa naanza kazi (ya uandishi) nilihamanika na kwenda huku nalia kwa bosi wangu reggie mhango baada ya jamaa kuniandikia barua kuwa naboronga, sijui kuoiga picha wala kuandika, hivyo niache nitafute kazi ingine. iliniuma na kunisumbua sana, hasa kwa kuwa barua hiyo ilichapishwa kwenye gazeti letu wenyewe!

    "Sasa unalia nini", alinijibu reggie, ambaye baadaye nikaja kumaizi kuwa ndiye aliyeruhusu barua hiyo ya kuniponda ichapishwe. "Wenzio wamefanya kazi miaka zaidi ya kumi na hawajapata kutumiwa barua ya aina yoyote.

    "Sikiliza Michuzi; furahi kwamba kuna mtu kaona kazi yako na kaamua kukaa na kukuponda. Hii inaonesha watu wanakusoma na kazi zako wanaziheshimu na hii ndio njia yao ya kukupa changamoto..." alimalizia.

    Toka siku hiyo kiasi cha miaka 15 ilopita, sijawahi kukatishwa tamaa na jambo lolote, hususan watu hawa ambao nawaita nzi wa kizungu (wa chooni). Ndo maana nakubaliana na wewe kwamba sintoweka vizingiti wala mchujo wala kususa endapo ntatukanwa mimi ama mtu yeyote.

    Hivyo Ndesanjo kwa vile wewe ndiye mbatizaji wangu kwenye blogu nakuahidi mbele ya baraza hili la kaka Jeff kwamba ALUTA KONTINYUAAAA!

    kesho ntakuwa bagamoyo kwenye tamasha la sanaa nambako JK atakuwa mgeni rasmi siku ya ufunguzi jumatatu. tegemeeni mengi na wengi toka huko.

     
  • Tarehe: 10:38:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jamani kaka ndosanjo wengine hatuna utaalamu mwingi kwenye mambo haya ya matumizi ya kompyuta sasa mkituwekea vizuwizi vya kujiandikisha kutoa maoni itakua tabu jamani,Ila tuhimizane tu kuepuka matumizi ya lugha chafu,na masengenyano.Najifunza mengi niingiapo kwenye bloog hizi

     
  • Tarehe: 3:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    wakina mama wote wange vaa hivi UKIMWI ungepungua

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker