
Ulimwengu wa biashara siku hizi unaenda sambamba na ubunifu mkubwa wa jinsi ya kutangaza bidhaa au huduma kwa jamii. Haishangazi basi kusikia kwamba mabilioni ya fedha hutumika katika nyanja hiyo muhimu ya kujitangaza.
Ukweli ni kwamba yapo matangazo ambayo yanavutia kiasi kwamba unaweza kununua usichokihitaji (commercials makes you buy what you do not need).Kuna umuhimu sana wa kujiuliza je hiki kitu ninachotaka kukinunua nakihitaji au nakitaka tu?
Majuzi katika pita pita yangu jijini Toronto,nimekuta hiki kigari kilichozungukwa na asasi za jikoni kimeanikwa juani.Unadhani nini kinauzwa hapa? Hicho kigari au hivyo vyombo?
sisi watu weusi ndio tunaongoza kwa kukamatwa na haya matangazo.Mtu yupo radhi alale kwenye gari kisa tu ni gari la thamani,hana nyumba wala pango.Wenzetu weupe wananunua mara nyingi what they need na sio what they want.Tujifunze na sisi.