VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Friday, September 15, 2006
WANAUME HAWA BWANA

Wakati wa mkutano wa kimataifa wa masuala ya ukimwi hapa Toronto mwezi uliopita, yalikuwepo mambo mengi sana ya kujifunza, kutathmini na kisha kujiuliza wapi tunakwenda. Mojawapo ya mambo ambayo yalikuwa yakiwashangaza wengi na kwa maoni yangu kupoteza kabisa muelekeo wa mkutano wenyewe ni masuala ya haki za wasenge na watu wanaohama kutoka kwenye jinsia moja kwenda nyingine (transgenders).

Kimsingi katika nyakati nyingi mkutano ulikuwa unageuka kutoka kwenye majadiliano ya ugonjwa wa ukimwi,tafiti za tiba nk na kuwa jukwaa la haki za binadamu. Inavyoelekea siku hizi ni vigumu sana kutenganisha siasa,haki za binadamu na ukimwi. Kilichokuwa kinanipa tabu zaidi ni kujaribu kuingia vichwani mwa waalikwa kutoka Afrika ambako masuala haya ya ndoa za jinsia moja,usenge na hata transgenders bado ni ndoto za usiku wa manane. Hivi walikuwa wanajifunza nini? Au ndio mbinu ya kuwaanda "kuiga" sera hizi za kimagharibi au la waitwe "wasioheshimu haki za binadamu"?

Pichani hao ni transgenders. Hao ni wanaume ambao wako njiani kujigeuza kuwa wanawake. Wao husema muumba alifanya kosa.Unasemaje?

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:40 PM | Permalink |


Maoni: 15


  • Tarehe: 10:10:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff,
    Watu hawa mimi hunishangaza sana wanaposema kwamba mungu alikosea.Hilo mimi sikubaliani nalo hata kidogo kwa sababu naamini muumba hakosei.

     
  • Tarehe: 9:18:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mzee wa mshitu

    Ahhhh Kaka hii nakubaliana nawe kuwa ni njama ya kutuambukiza tamaduni za kipuuzi, kwani hakuna maana ya kutumia muda mwingi wa kongamano heshimika la ukimwi kuzungumzia usenge na uhamishaji jinsia.

    Kitu kimoja mimi chanitatiza hapa hivi kweli huyu wa kulia huku ni dume duhh basi kazi!

     
  • Tarehe: 10:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff,
    Bahati mbaya ama nzuri usenge na usagaji upo katika tamaduni zote.kuanzia waarabu,wahindi ,wachina,waafrika ,nk
    Kwangu nafikiri ni maumbile kama ambavyo watu wengine wana miguu mifupi ama mirefu vivyo urijali unatofautiana
    Kwa muda mrefu hata watu wa magharibi wamekuwa wakipinga jambo hilo japo eventually wameanza kuli accept
    Ukienda Kinondoni unaweza kukutana na wasenge wengi labda kama Toronto (yeah right !)
    Na majike dume yamekuwa around for ages too
    Kama mtu hayupo comfortable sioni yeye ananihusu nini kujibadili kuwa vyevyote anavyoyaka!
    Kama tunakubali ama la hiki ni kitu kinakuja kwetu pia kama wanawake kuvaa suruali kulivyokuja !

     
  • Tarehe: 11:04:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Simon Kitururu

    Mambo ya usenge yapo muda mrefu.Unakuta hata kwenye vitabu vya zamani kama biblia yamenukuliwa.Nafikiri hata katika enzi za sodoma na gomora kwa waaminio biblia inasemekana ndio ilikolea. Sasa hivi sayansi ndio inaongeza kasheshe kwa kuwezesha kuwabadili sehemu za siri. Nasikia siku hizi wanataaluma wanaujenga uume vizuri tu.Ingawa na wasiwasi na ufanyaji kazi wake.Ilikuwa kwa wale wanaotaka kuwa wanawake ndio pekee wanatengenezwa.Lakini sayansi inakotupelekwa sitashangaa baadaye wale ma bai sexual watakuwa wanataka watengenezewe sehemu zote iliwajifariji kutokana na tamaa ya siku.

     
  • Tarehe: 12:43:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Anyonymous wa hapo juu;kwa hiyo unakubaliana na dhana kwamba huenda muumba alifanya makosa katika kuwaumba watu hao?

    Kama huamini katika dini hizi za kawaida unadhani nitakuwa nakosea nikisema usenge au usagaji ni "choice" na kujiendekeza na halina uhusiano wa kisayansi wanaposema kwamba kuna watu wamezaliwa hivyo?

    Nakubaliana na wewe kwamba mambo haya yamekuwepo tangu enzi na enzi.

     
  • Tarehe: 2:33:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Hi Jeff,
    Wacha niedelee kuwa anonimous !
    Nadhani Waafrika tunakimbilia sana kumsingizia Mungu katika mambo mengi kwasababu ya uvivu wa kufikiri.Kwa mfano mvua ,vita,umasikini ,life expectance,maradhi,maumbile nk.
    It is better tabia hiyo ife sooner rather than latter.
    Nadhani tunakubaliana kwamba hormones zina play part kubwa sana katika sexuality na kwa kusema hivyo sitafuti mtu wa kumlaumu.
    Kijiji nilichotoka yupo dada mmoja tulikuwa tunamuita dumejike.Huyu dada hajawahi kuvaa sketi ama gauni katika maisha yake yote ana umri wa miaka takriban 45
    Amekuwa na living girl friends kwa muda wote niliomfahamu (usiniulize wanafanyaga nini ) ingawa haikubaliki na wana kijiji
    Wapo wanaosema anazo zote mbili (amezaliwa hivyohiyo sikutafuta kuhakikisha!) huoni kama opereshen ya kumfanya awe mwanaume kamili ingekuwa kama ndoo ya maji jangwani la Sahara ? Sidhani kabisa (Hand on heart) kama alichagua kuwa hivyo
    Ipo mifano miingi ya namna hiyo ,bila kujali kama tutakubalina ama la.
    Nashindwa kusema kama ni nani wa kulaumiwa . Kwani mtoto akizaliwa taahira ama kilema huwa ni nani unamlaumu ?
    It is scientifically proved kama ujuavyo kwamba wapo watu wa namna hii na WANAHITAJI MSAADA WETU.

     
  • Tarehe: 2:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    I couln't agree more with you mr Anonimous !
    Si uweke jina lako kama una uhakika na unachosema ?

     
  • Tarehe: 9:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Sultan Tamba

    Sidhani kama kuna dini inaukubali usenge! Kwa hizi dini ninazozijua mimi sijawahi kusikia! Ni jambo ambalo linakemewa karibu na vitabu vyote. Mungu amempa kila mtu akili ya kuamua anachotaka, hajaumba huyu aende motoni huyu aende kwenye pepo ni akili yako na matendo yako mwenyewe. Sikubaliani kwamba kuna mtu kaumbwa ili awe msenge! Mungu huwa hakosei. Ndiyo maana ukiutumukia usenge kwa muda mrefu ile sehemu inaharibika vibaya na inakuwa haifai kwa matumizi yote yaliyokusudiwa ambayo binaadamu tunayajua.

     
  • Tarehe: 2:43:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    I couldn't agree with both of you, Jeff and Anonymous 18.9.06. Kweli kuna wengine kati ya hao kama huyo mama wa kijijini kwenu, ambao wana uume na uuweke wanahitaji msaada, Mara nyingi watu kama hao wanaangaliwa ni wapi they are more compatible, whether a girl or a boy and then they change accordingly. But my issue right now is that; majority of Gays right now have nothing to do with hormones or multisex, they are just gays because they want to be. which is wrong, sio kwamba tunamkimbilia Mungu kwa ku justify our hoja, ila in the bible and Qur-an both are against this, More over Cultural too. Swali langu kwa Anonymous 18.9.06, Je unakubaliana kuwa it's okay to be Gay just for the sake of being Gay??? kwasababu I can promise you that not all gays are born that way. Kuna shule ya how to be Gay.

     
  • Tarehe: 2:44:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Asante kaka Jeff kwa kuleta haya majadiliano.

     
  • Tarehe: 2:48:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    This comment has been removed by a blog administrator.

     
  • Tarehe: 11:27:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Sasa kuwa anonimous inachanganya !
    Wacha niwe anonimous 1 kwani ndiye niliyeandika hapo juu tarehe 18.09.2006
    Nipo pamoja na wewe kabisa anonimous wa hapo juu, it si almost impossible to draw a line like ,we msenge mkubwa mbona imekuchua miaka yote kuja kufanya operesheni hii ! ama we hauna usenge wowote unazuga tu !
    Nafikiri watu wapo na haki ya kuelimishwa iwezekanavyo na waachiwe waamue wanavyotaka.
    Hata vitabu vya dini haviwashiki mikono watu waende kanisani wala misikitini.
    Vinavyofanya ni kuwaataarifu kwamba ukitenda dhambi Mungu atakuadhibu !!
    Kifupi siungi mkono gays who do it for the sake of it
    Chaguo ni lake

     
  • Tarehe: 11:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff,
    Naomba utengeneze maada ya Utamaduni wa muafrika !
    Ni nini utamaduni wa muafrika?
    Je ni kuvaa kanzu kwenda mskitini ama suti kwenda kanisani ?
    Ni wanawake kuvaa nguo ndefu ama mipasuo ama kutokuvaa kabisa?
    Ni wanaume kutoboa masikio ama kachanja uso ?
    Je utamaduni wa kipare in particular unawekwaje kwenye kundi moja na tamaduni wa kimasai ?
    Ama ni watu wanakuwa wavivu kuanalyse na kutuweka kwenye kundi moja kuuuuubwa
    Ama ni Ile kasumba ya kwamba Afrika ni pori moja kuuuubwa na pamoja na wanyama milima wapo watu pia !
    From my short experience one would struggle kupata utamaduni wa m asia kwani mchina,marabu na mhindi couldnot be more different !
    ama utamaduni wa mzungu kwani muingereza na mkosovo are really different as well
    Kwanini wafikiri kwamba waafrika wote wana tamaduni sawa ?
    Je ni kweli tuna tamaduni sawa ?

     
  • Tarehe: 12:09:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Sikumuelewa mmoja wa anoni wako anasema majike dume huchagua upande walio compatible na ku "ku change accordingly !"
    Labda ni rahisi kusema kuliko kutenda.
    Watu hawa bila opereshen na madawa ya kuwa change kabisa they will always be "somewhere in the middle" na hiyo ina madhara yake.

     
  • Tarehe: 1:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Anoni wa hapo juu uliyeniomba nitengeneze mada ya utamaduni nk.Nitafanya hivyo siku chache zijazo.Kipindi cha nyuma tuliwahi kuwa na mjadala wa muziki wa kizazi kipya.Unaweza kuupata mjadala huo hapa kwenye tovuti hii kwa kutumia searching option upande wa kulia.Ukiandika muziki wa kizazi kipya utapata mjadala huo na mingineyo mingi.Huu wa kwako nitauweka siku si nyingi.

    Tuendelee kuelimishana na ahsanteni sana wasomaji na wachangiaji wote.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker