Friday, September 08, 2006
WANAUME WA BLUU
Wiki chache zilizopita niliwaona hawa jamaa wanaoitwa wanaume wa bluu .Ukisoma historia yao utagundua kwamba walianza jamaa watatu kimchezomchezo tu. Historia yao siwezi kuitofautisha na ile ya jamaa fulani pale jijini Dar ambao hupita baa baada ya baa,mtaa baada ya mtaa,wakiwachekesha watu huku wamejipaka masizi na kuweka vitambi vya matambara,tai za ajabu ajabu nk. Pengine wale tunaweza kuwaita Dark Men, kwa sababu wao wanatumia rangi ya masizi ambayo ni nyeusi.
Tanzania kuna vipaji vingi kupita kiasi. Hili hunipa maswali na aibu ndani ya kichwa changu. Hivi kwanini tunashindwa kuviendeleza vipaji? Hapa naongelea sisi wananchi,wenye nchi, kwa sababu kimsingi serikali imeshashindwa.Miaka zaidi ya arubaini bila muelekeo wa maana katika kuendeleza vipaji vya kisanii hakuna maana nyingine zaidi ya kushindwa. Na je,sisi tuliopo ughaibuni,sisi ambao tunaona jinsi gani vikundi kama hawa wanaume wa bluu wanavyofanya kazi tunashindwa nini kuibua vipaji kama hivyo kutoka nyumbani na kuvitangaza kimataifa?
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:07 PM


|
Permalink |
-
Jeff tupe breaking news za hapo canada (Montreal) tunaona mtu ana fyatua risasi ovyo ovyo ktk Dawson College nini chanzo? tupe habari mzee!! Na amejipiga mwenyewe risasi!! inakuwaje?
13/09/2006 @ 19:03GMT
-
Naufuatilia mkasa huu kwa karibu.Ila kwa hivi sasa inaonyesha kwamba jamaa alikuwa mmojawapo wa hili kundi linalojiita vampires.Yaani wao wanadhani maisha ni kama ushetani hivi na kila wanachokiona kwenye video games wanataka kujaribu in real life.Nyumbani Tanzania hawa tungewaita "machizi".Hapa Canada wanayo majina ya kisayansi.Tovuti yao ni www.vampirefreaks.com na huyu jamaa ambaye mpaka sasa haieleweki kama alijiua mwenyewe au alipigwa risasi na polisi yumo,jina lake halisi ni Kimveer Gill alikuwa ana umri wa miaka 25.Mtu mmoja alikufa palepale na wengine 11 wamelazwa huku wawili hali zao zikielezewa kuwa mbaya.
-
Nina rafiki mmoja hapo Penticton Canada ambaye hata jina anajiita Vampiress. Hata siku moja simuelewi na siwezi kumtembelea katika maisha yangu.Nangoje anipe dondoo kuhusu anafikiria nini kutokana na tukio hili. Urafiki wetu umetokea kwa sababu na ukweli nilikuwa sijawahi kukutana na mtu ambaye hatofautishi real life na fantacy before.Hapa duniani tuna macizi kibao, lakini inasikitisha wakifikia kuathiri na kuua watu wengine wasio fuata uchizi wao
-
Hawa machizi wa namna hii sijapata kuwaelewa hata kidogo, Watu wanaopenda mambo ya kufa kufa tu.
Jeff tupe breaking news za hapo canada (Montreal) tunaona mtu ana fyatua risasi ovyo ovyo ktk Dawson College nini chanzo? tupe habari mzee!! Na amejipiga mwenyewe risasi!! inakuwaje?
13/09/2006 @ 19:03GMT