Friday, September 22, 2006
ZANZIBAR NDANI YA TORONTO!
Siku za nyuma niliwahi kuibandika hii picha hapa ubaoni. Niliahidi kwamba ningali namsaka mmiliki wa sehemu hii ili aeleze kwa kifupi uhusiano wa visiwa vya Zanzibar na hii sehemu ambayo shughuli zake haziendani na maadili ya visiwa vya Zanzibar ambavyo ni sehemu muhimu sana ya nchi yetu ya Tanzania.Ukitoa Zanzibar hakuna tena Tanzania bali Tanganyika. Ukibonyeza juu ya hiyo picha ukasoma maandishi yaliyopo nje utagundua nini naongelea kuhusu shughuli zinazofanyika humo ndani.
Kwa bahati mbaya mpaka hivi leo sijafanikiwa kuonana na mmiliki wa kibanda hii. Nilimuachia simu yangu anipigie lakini naona mpaka leo kimya. Nimeamua kuibandika tena picha hii ili kama kuna ambaye anajua uhusiano wa Zanzibar hii ya Toronto na ile ya Pemba na Unguja atusaidie.Unadhani hii inapotosha watalii wanaotaka kuvitembelea visiwa vya zanzibar au ndio inachangia watalii wengi kumiminikia Zanzibar wakiwa na yao kichwani? Unaweza oanisha habari hii na ile ya majuzi kumhusu Mercury? Isome hapa.Uchunguzi kidogo nilioufanya unaonyesha kwamba hizi Zanzibar ziko nyingi sana huku ughaibuni. Zote zina shughuli zinazoendana.Mfano angalia hapa au hapa Kwanini?Kulikoni?
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:06 AM
|
Permalink |
-
Jeff
Ipo Zanzibar night club nyingine hapo Leicester labda wadau wako watakuwekea picha
Abdul
-
Na hapa ninapoishi palikuwa na kilabu cha dansi - Zanzibar, kimefungwa hivi sasa.
Kitu nachoweza kuwaza haraka haraka ni kuwa Zanzibar ni brand name inayoweza kuuzika.
Hawa watu wanaotumia hilo jina bila kulipa ushuru kwa sababu zao binafsi ambazo mara nyingi hazina uhusiano na tamaduni za kisiwa hicho - wamegundua kuwa hilo jina lina-sound exotic. Kwa hiyo linatia mvuto fulani.
-
Ni sawa alivyosema Mwandani, jina Zanzibar linauzika. Wanasema eti linaleta hisia za kitu "exotic" vile! Karibu kila ninapokwenda lazima nikutane na "Zanzibar."
-
Zanzibar aaahhh Zanzibarrr, kama Ndesanjo na Tungaraza wanavyosema inauzika, hivyo inabidi tufungue kesi ya kudai fidia ya pesa zinazotokana na mauzo ya mvuto wa jina la Zenj labda tutaweza kupata.
-
Kwa mtaji huo wa kuuzika inabidi kwanza tulisajiri hilo jina ili tupate haki miliki yake ndio tuwauzie watu
-
Zanzibar ni mojawapo ya visiwa murua sana duniani.Watu wa magharibi wamekuwa wakivifahamu kabla ya uwepo wetu mimi na wewe.
Kuanzia wareno,Wajerumani,Waingereza,Wachina ,Waarabu na Wahindi wamekuwa wakifanya biashara na visiwa hivi kwa miongo mingi.
Kama umefika Zanzibar utaona ni nini naongelea!
Hainishangazi kusikia kuna sehemu mahali duniani wanatumia jina hili
Labda siku moja wabongo watajifunza kwenda holidays kama huko ulaya na kuanza kuja Zanzibar (karibuni sana)
Jeff
Ipo Zanzibar night club nyingine hapo Leicester labda wadau wako watakuwekea picha
Abdul