Wednesday, October 04, 2006
KAZI NI KAZI?
Waafrika au niseme watanzania tunao msemo unaosema kazi ni kazi, ili mradi mkono uende kinywani. Nadhani wazee wetu walipoutunga msemo huu walimaanisha tusichague kazi,tufanye kazi yeyote iliyopo mbele yetu. Nadhani nitakuwa sijakosea nikisema msemo huu ni mzuri na kama wengi wetu tungeuzingatia basi pengine yale makundi ya vijiweni kila kukicha yangepungua.
Unadhani msemo huu unazingatiwa? Nipe maoni yako. Pichani ni jamaa akiwa kazini jijini Toronto. Anatangaza bidhaa kwa ajili ya watoto huku akiwasaidia kupuliza maputo yao.Kazi ni kazi? Hebu malizia kwa kusoma makala hii hapa.
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:09 PM
|
Permalink |
-
Kwa mtazamo wangu wa Tanzania, kazi ni kazi ni msemo tu. Nakumbuka tokea shule ya msingi ilikuwa ujanja kukimbia kazi. Utakuta asilimia kubwa ya hata waliotaka kuwa viongozi, moja ya motisha ilikuwa kurahisisha kazi. Angali hata maoni katika haya ma blogu.Ni kawaida kukandia kazi kama za ufagizi, kulelea wazee na zinginezo. Mimi nahisi hili ni baadhi ya jambo ambalo liko katika ubongo wa Mtanzania ambalo bila kubadilika safari ya maendeleao itaendelea kuwa ndefu sana.
-
Naam Jeff!
Ingawa ni kweli kwamba kazi ni kazi, lakini si uwongo kwamba kazi zingine kweli ni kazi, chukulia mfano ujambazi. jee nikipora mkono hauendi kinywani? na hapo sizungumzii bastola na ngeta, nazungumzia pia rushwa, utapeli na uozo mwingine kama huo. hapa nakumbuka maneno ya Che Mkapa ya: Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe...
-
Simon,
Umenifanya nifikirie,kumbe suala hili lina ile ile mirija ya utumwa wa akili sio?
Michuzi,
Labda tuseme kazi halali,yaani ile isiyovunja sheria na taratibu za nchi husika.
-
Kazi ni kazi, katika kiungo ulichoweka kuhusu machina kuwa machinga tanzania... Wale ndio wanavyoenda kama wajinga wajinga, ukishtuka unakuta wanamiliki kila kitu.
Nenda kokote utakuta wamejenga China-town...