VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, October 31, 2006
MKUTANO WA KWANZA WA WANABLOG WA KITANZANIA!

Kama unasoma habari hii nina uhakika kwamba wewe ni mfuatiliaji wa karibu wa masuala ya Tanzania, ya kitanzania na watanzania nyumbani Tanzania na popote tulipo ulimwenguni.Pia nadhani sitokosea sana kama wewe ni mmojawapo wa watanzania waliotapakaa sehemu mbalimbali za dunia na ambao tayari wanaendesha au kumiliki chombo kipya cha mawasiliano ya umma yaani blog( jina mbadala la kiswahili bado lina mjadala kidogo)

Isitoshe nina uhakika kwamba umeshajionea au kuona jinsi ambavyo nchi yetu inasonga mbele au kurudi nyuma. Kutegemea na jinsi unavyoona wewe inawezekana unafurahia au unashikwa na hasira, unakata tamaa na wala usijue la kufanya(mimi ni mmojawapo).

Binafsi naiona hasira ya wananchi kutoka kila kona,hasira ambayo wakati mwingine inafanya hata uwezo wa watu kufikiri kwa nia ya kupata ufumbuzi inapotea. Huwa sishangai wananchi wakimimina matusi tu kwa mfano pale kwa
Michuzi.Hawa watu sio vichaa,ni hasira ndio inawaongoza.

Ukweli mwepesi ni kwamba nguvu ya siasa katika kuleta mabadiliko ya kijamii nchini Tanzania haitii imani tena. Kuna kitu kinamiss. Miaka zaidi ya arobaini inatosha kukupa picha halisi.

Katika kujaribu kuangalia jinsi gani tunaweza kushiriki katika maendeleo halisi ya nchi yetu ni wazi kwamba nguvu ya wananchi, nguvu ya umma, ambayo nadhani bado haijatumika ipasavyo, inahitajika kuliko wakati mwingine wowote. Katika nchi zilizoendelea taasisi za kijamii (civil societies) ndizo zimekuwa chachu muhimu ya maendeleo yao. Kwa bahati mbaya za kwetu hazina uhai.

Kufumba na kufumbua, imejitokeza nyenzo muhimu sana ya kuunda upya nguvu hii ya umma. Nguvu hii inaitwa blogu. Ziada ya nguvu hii ni kwamba sio tu inaweza kutumika kama chombo muhimu cha nguvu ya umma bali pia inatoa burudani, inaelimisha, inajenga uzalendo, inaamsha fikra na ikitumika vizuri inaweza kabisa kuandika katiba mpya! Haishangazi basi kuona kwamba wanasiasa maarufu duniani,maraisi, mawaziri,wabunge,washika dau chungu mbovu wanamiliki blog pia. Ushahidi upo wazi kwamba wanasiasa na viongozi wetu wa Tanzania ni wasomaji wazuri wa blogu za watanzania.Ujumbe muhimu unawafikia na hivyo kuathiri uundaji wa sera mbalimbali.

Lakini ni muhimu sana ieleweke kwamba blogu sio uwanja wa siasa. Blogu hivi sasa ni jamii.Jamii ina watu wa kila aina. Ndio maana hata blogu za kitanzania sio zote zinazojadili masuala ya kisiasa peke yake. Ukweli ni kwamba wanablogu wengi wa kitanzania (nikiwemo mimi) sio wanasiasa hata kidogo. Ni watu tu wenye mapenzi na nchi yao na wanaotamani kuona nchi yao ikipiga hatua. Hivyo basi watatumia njia kadhaa kama sanaa, siasa, elimu nk kuhakikisha ujumbe muhimu unawafikia walengwa.

Ingawa idadi ya blogu za kitanzania (za lugha kadhaa za kiafrika, kizungu na kwa wingi kiswahili) zimekuwa zikiongezeka kila mara na hata kuushangaza ulimwengu wa blogsphere, hatujapata nafasi ya “kukutana”. Nia imekuwepo, sababu zimekuwepo, mipango ya muda na jinsi ya kukutana ndio imekuwa migumu. Habari njema ni kwamba sasa tunaweza kukutana kwa kutumia tekinolojia hizi hizi za mitandao ambazo zimetuwezesha baadhi yetu kufahamiana bila hata kuwahi kukutana!

Kikubwa kilichobaki ni sisi wenyewe kuamua lini tunataka tukutane, saa ngapi (tukizingatia uwepo wetu katika maeneo mbalimbali ya dunia, upatikanaji wa mtandao kwa wale wanaotumia migahawa ya mtandao nk) Mwenzetu Ndesanjo Macha amejitolea kutambulisha na kuunda mitabendi rahisi ambazo zitawezesha kukutana kwetu. Atatoa maelekezo zaidi tukishakubaliana kukutana.

Nimeweza kuwafikia baadhi yenu na wengi mmependekeza kwamba tunaweza kukutana siku ya Jumamosi, Tarehe 18 Novemba, 2006 kuanzia Saa Sita Kamili Mchana kwa saa za Tanzania. Sasa ili kuwa na demokrasia kamili ni muhimu kama nyote mtatoa maoni yenu hapa na kusema kama mnadhani tarehe hiyo hapo juu, siku, muda na saa ni muafaka ili maandalizi mengine yaendelee.

Nia kuu ya mkutano huu ni kukutana. Hapatakuwa na ajenda maalumu. Ajenda ya kikao kitakachofuata baada ya hiki itaundwa na washiriki wote ili kuondoa tabia ya “wachache” kuunda ajenda wanazozitaka wenyewe.

Wasiokuwa na blogu pia wanakaribishwa sana katika mkutano huu.

Naomba kuwasilisha!




 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:42 PM | Permalink |


Maoni: 28


  • Tarehe: 4:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Mjengwa

    Jeff!
    Nakushukuru sana kwa taarifa hii.Mimi nadhani tarehe inayopendekezwa ni muafaka.

     
  • Tarehe: 4:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

    Wazo zuri kaka, naunga mkono tarehe,muda na siku iliyopendekezwa.

     
  • Tarehe: 6:14:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    niko tayari, endelea kutufahamisha muda ukiwadia.

     
  • Tarehe: 7:32:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

    Muda na Tarehe nitakuwa Moshi,itakuwa vigunu sana,pia ningependa kuchangia maoni wakati huo.

     
  • Tarehe: 7:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Ahsanteni wachangiaji,wanafamilia.Tafadhali endeleeni kusambaza ujumbe huu ili taarifa iwafikie wanablog wote na hata wale wasio na blog ambao wangependa kushiriki mkutano huu.

     
  • Tarehe: 8:28:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Simon Kitururu

    Niko pamoja nanyi katika tarehe hii

     
  • Tarehe: 9:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jaduong Metty

    Nadhani huu ni wakati muafaka.

     
  • Tarehe: 3:51:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff, shukrani kwa kuchukua jukumu hili la kutusukuma ili tuweze kukutana na kubadilishana mawazo jinsi gani tunaweza kutumia teknolojia hii kwa faida ya taifa na bara letu.

    Kuna wimbo mmoja unasema, "Now that we have found love, what are we going to do with it?"
    Tunaweza kubadili maneno hayo na kusema, "Now that we have found blogs, what are we going to do with them?

    Au, "Now that we can own the media, what are we going to do?

    Naona mkutano huu hasa utakuwa unauliza swali hilo.
    Ninapandisha taarifa kuhusu mitabendi ya mkutano huo hivi sasa.

     
  • Tarehe: 7:05:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Sultan Tamba

    Ni wazo zuri, naliunga mkono, na tarehe iliyopendekezwa na siku pia naunga mkono, naahidi nitashiriki.

     
  • Tarehe: 7:27:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

    Kaka,Jeff nitashiriki lakini naomba topic kama umeziandaa,nivizuri kutupa changamoto na kujiandaa.

     
  • Tarehe: 7:42:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Luihamu,
    Nadhani kama umemwelewa Jeff vizuri ni kwamba hakuna suala la watu fulani kuandaa mada kwa ajili ya watu wengine. Moja ya jukumu la mkutano huu ndio kuandaa basi mada kwa ajili ya mkutano utakaofuata.

     
  • Tarehe: 1:31:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Ahsante Ndesanjo kwa kunisaidia kwa swali alilokuwa ameuliza Luihamu.

    Kwa wengineo wote,
    Ndesanjo ameshapandisha pale kwake maelekezo muhimu ya jinsi gani tutaweza kukutana katika tarehe ambayo tutafikia muafaka nayo.Tafadhali tembelea www.jikomboe.com usome maelekezo yale ambayo yapo chini ya kichwa cha habari SHIRIKI KUPANGA MKUTANO WA WANABLOGU WA TANZANIA.
    Ahsanteni sana.

     
  • Tarehe: 4:10:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Mija Shija Sayi

    Jeff na wanablogu,

    Naomba tusogeze muda wa kuanza, mnaonaje ikiwa saa nane kwa saa za Tanzania?

     
  • Tarehe: 5:31:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    jeff!

    asante kwa wazo hili. niko nanyi katika hili, na naomba nihesabike katika koram, na hata kama nitashindwa kuhudhuria, naomba niseme niko pamoja na wote, na mawazo yote nitayaheshimu na kuyaafiki. wazo la da mija naomba tuliangalie kwa macho mawili, kwani saa sita wengi twabeba zege. ila usichoke kutafuta muda muafaka, kwani nitajihisi kutindikiwa nikikosa.

    nawaomba wanablogu wote wawafahamishe wengine, hata kama hawana blogu kama ulivyosema, umuhimu wa mkutano huu wa kwanza

     
  • Tarehe: 5:57:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

    Siku na saa ni muafaka. Tuombe uzima tufike na tunaisubiria hiyo siku kwa hamu.

    Nashukuru.

     
  • Tarehe: 5:59:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MK

    Samahani Damija sikuona comm.. yako, Wahusika wa huu mkutano tunaomba muliangalie ombi la dada yetu.

    Nashukuru.

     
  • Tarehe: 4:40:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Rama Msangi

    Kwa tulioko Tanzania tumetizama na tatizo la umeme au tumeshajiridhisha kuwa limeisha sasa!!

    Tutakuwa pamoja kwa wale ambao tutabahatika kuwepo siku husika na muda, ni vyema siku tatu kabla tukafikia muafaka rasmi na kutoa tamko la mambo ambayo tutayajadili, muda muafaka (maana kuna wameomba usogezwe, na huenda wakaomba wengine urudi nyuma) na mambo kama hayo

     
  • Tarehe: 5:06:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Da Mija,
    Inawezekana saa nane ikawa ni muda muafaka kwa wengi. Lakini ili kujua hilo, itabidi basi watu waweke alama ya vema katika kalenda ile ya kupanga ili tuweze kujua ni watu wangapi wanaweza kuwa na muda saa nane na wangapi wanaweza kuhudhuria saa sita. Hii ndio itakua njia rahisi. Kwa mfano, iwapo watu kumi na tano wataweza kuhudhuria saa nane, na watu sita saa sita, basi tutasema mkutano ni saa nane. Lakini tutajuaje? Lazima kwanza watu waweke alama pale kwenye ukurasa wa kalenda kuonyesha saa ambayo ni muafaka kwao.

     
  • Tarehe: 6:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Gallus

    Ni wazo zuri sana, nampongeza aliyeliibua licha ya kwamba limechelewa... siku na muda ni muafaka sana, naahidi nitashirki, Asante,

     
  • Tarehe: 6:57:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Gallus

    Saa sita naona ni muafaka zaidi kusema kweli!

     
  • Tarehe: 7:03:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Naungana na da Mija, saa nane ni muafaka. Kalenda iko wapi wazee. Nitashiriki. Salaam.

     
  • Tarehe: 4:19:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Paul,
    Kama unaulizia kuhusu kalenda ya kupiga kura kuchagua saa ya kukutana,inapatikana pale kwa Ndesanjo (jikomboe.com) au katika kiungo nilichotoa katika post hiyo hapo juu.

     
  • Tarehe: 12:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

    Wanabloggu naomba kama inawezekana tusogeze tarehe nyuma au baadya ya tarehe 18 iliyopendekezwa.Tarehe 18 nitakuwa safiri shughuli za serikali na ningependa kuchangia maoni katika mkutano huu.Kwanini tusisogeze tarehe nyuma?Kama haitawezekana itakuwa vizuri nipitie mliyo pendekeza katika mkutano huo.

     
  • Tarehe: 5:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Wna Blogg. Wazo zuri na nafikiri wengi watafika siku hiyo. Ila huu muda jamani mbona kama mapema kidogo? Kama ingelikuwa saa 8 mchana nafikiri ni bora kwa sababu Africa na Europe ni mchana, na USa ni asubuhi. Labda tu balaa kwa walio Australia na Asia. Lakini hata kwao nafikikiri ni heri kwenda kulala saa tisa kuliko kuamka saa 10 alfajiri kwa watu waliko USA/Canada. Hakuna muda mzuri sana kwa kila mtu lakini ndiyo demokrasia.

     
  • Tarehe: 11:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    HABARI

    MIMI NAITWA YONA MARO EMAIL YANGU NI yonamaro@hotmail.com na simu yangu ni 0784360204 MIMI MWENYEWE NIKO DAR ES SALAAM HUWA NACHANGIA KATIKA BLOGU LAKINI SANA KATIKA FORUMS NA KUANDIKA HADITHI KIDOGO BASI TUTAFUTANE MUDA HUO MIMI NITAKUWA SINA KAZI

    AHSANTE

     
  • Tarehe: 5:48:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mzee wa mshitu

    Yess huraa ni idea nzuri sana, muda nadhani ni muafaka tukutane tu siku hiyo!!

     
  • Tarehe: 9:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Hector Mongi

    Juhudi zimeonekana. Siku za mwishoni mwa wiki ni muafaka na haswa ikizingatiwa hali ya umeme hapa nyumbani. Angalau Jumamosi na Jumapili maeneo mengi yanapata umeme ingawa sio wa uhakika sana. Natoa maoni haya nikizingatia kuwa ukumbi wa mkutano utakuwa huku huku kwenye mtandao.

     
  • Tarehe: 12:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger bongozite

    Mie kwa bahati mbaya nilikosa mkutano huu. Lakini jitihada zote za kuwaendeleza watanzania ni za kupongeza.

    Tusirudi nyuma ni kusonga mbele tu.

    Tengo Kilumanga

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker