VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, October 24, 2006
NATAKA CHEZA DOGORI

Nawaona wananipungia. Unaweza dhani wamekuwa punguani. Hawataki kukutana nami uso kwa uso. Wamejaa soni. Wamekunywa yohana mtembezi kupita kiwango. Hawanipendi eti kwa sababu napenda msondo na siishi kutumia Kiswahili. Wanasema maisha yatanipiga chenga siku zote kwa sababu sitaki kujifunza lugha ya wenyewe yaani kizungu. Wananiita msimbo ili wazungu wawaone wao wa maana zaidi.

Wanacheka mavazi yangu eti yana makunyanzi na sio kama yao ya kizungu. Ithibati juu ya hili haionekani. Kwikwi zangu ni juu yao.Wamekubali kuwa watumwa. Natami niwavishe kafani, roho zao zimeshatutoka.

Wanakuwa kama watoto wanaochezea mapulizo. Wanatamani wanilishe punju. Wanashindwa kwa sababu mimi sichezi pungwa kama wao.Wanashindwa wanione wapi. Sina jinsi ya kuweza fikia itifaki nao.

Nalia mimi.

Pichani ni usafiri maarufu jijini Toronto ama subway kwa jina maarufu. Nasikia Dar-es-salaam nayo itakuwa na subway siku si nyingi.Ni kweli?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:52 AM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 3:02:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Kabla maswala ya umeme hayajapata jibu siwezi kuwa na ndoto ya usafiri huu

   
 • Tarehe: 3:28:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Kitururu,
  Nadhani umenena kweli kabisa.Ni dhihaka kuanza kuzingua wananchi na mipango hewa ya subway bila hata ya kuwa na uhakika na umeme.Huwa nashangaa hata mbembe za kuita wawekezaji wakati tunajua umeme hatuna.Ningeshauri raisi asisafiri tena mpaka hali ya umeme itengemae kwa sababu kisingizio kikubwa cha safari zake kimekuwa ni kushawishi wawekezaji.Sasa waje kuwekeza wapi?

   
 • Tarehe: 12:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

  Kaka Jeff,kuwa na SUB WAY bongo.Umeme kaka.Lakini ujenzi wa sub way vijana watapata ajira na kuacha kukaa vijiweni.Kwa mtazamo wangu kabla ya sub way tuanze na kilimo.

   
 • Tarehe: 2:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

  Hiyo treni inapendeza hata kuona picha yake, sijui kama aliyeipanda huwa anatamani kushuka?
  Tunaweza kuwa nayo kama tukiamua, nani alitegemea kama kuna siku tutakaa zaidi ya wiki mbili bila kuwa na wamachinga waliotapakaa ovyoovyo?
  Mipango huleta kitu, Angalia tulivyo na uwezo wa kukodi mitambo ya umeme sasa, raisi akisema anataka kununuliwa dege la kisasa pesa zinapatikana, na mengine mengi tuu!
  Wape nafasi na muda wanaweza.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker