VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, October 16, 2006
UNATAKA KUSIMAMA NAMI?
Afrika inateketea, Tanzania inazidi kuyoyoma kutoka kwenye ramani ya ulimwengu. Hivi karibuni itakuwa tena koloni. Koloni lisilo na mtawala. Watazame. Wanarudi kimya kimya. Wananchi wamekata tamaa. Wameamini maneno ya wageni, nyie ni masikini. Hamna mnaloweza kufanya bila msaada wetu. Akili zimetekwa nyara. Tunauana wenyewe kupitia rushwa,ufujaji wa mali, ubadhirifu. Tunapigana kuliko wanyama. Tumechoka,hayo ni maneno ya baadhi yetu. Mwenye nguvu ndio ataishi, hii ndio njia ya maisha yetu.

Kiongozi hajali tena wananchi wake. Anajali zaidi tumbo lake, la familia yake. Anapayuka majukwaani kwa sauti ya radi. Anaongopa bila aibu. Kijasho chembamba kinamtoka pindi tunapouliza maswali magumu, ziko wapi kodi zetu? Anachekacheka huku anashika tumbo lake,akichoka kushika tumbo anashika sharubu zake. Amejaa unafiki, ananuka uroho wa madaraka. Kavalia suti ya marumaru, anamkenulia mtoto aliye tumbo wazi, mtoto mwenye njaa kali.Kinywani kwake kajiwekesha kijiti cha kutoholea vijinyama kutoka kwenye meno. Yeye kashiba.

Huyu tuliyenae ndio mkoloni mpya. Ameshika fimbo,ameshika kisu kikali. Anatukata bila huruma. Anasema maneno yale yale ya mkoloni. Aibu machoni kwake haionekani, achilia mbali moyoni mwake. Anaitwa mtumishi wa umma wakati umma ndio unaomtumikia yeye. Hawezi hata kufunga mkanda kwenye gari lake. Mikoba yake hatuna budi kumbebea. Akitembelea jimbo lake tunatamani tupige deki barabara zote. Kazi yake ni kuweka sahihi mikataba asiyoisoma. Anapata ten percent. Anaua jamii yake. Midomo yake miekundu kama damu, imejaa damu. Maisha ya watu keyachezea. Utumishi huu utumishi gani?

Tafadhali nipatie kikombe cha maji, kiu kimenibana kupita kiasi. Moyo wangu umejaa hasira na huzuni. Najua ninachotakiwa kufanya, bahati mbaya ni kwamba siwezi kukifanya peke yangu. Naomba msaada wako. Simama na mimi nisimame, sote tumzonge adui. Tumpe heshima kama anastahili. Kama anastahili adhabu basi tusisite. Nimechoka.

Nimechoka kuona ndugu zangu wanaishi kizani. Eti wanaishi mijini. Ama kweli dunia hadaa na ulimwengu shujaa.Amani inamsaidia nani eti? Nimechoka kuona mbwa wa Ulaya ana maisha mazuri kuliko binadamu. Nimechoka kusikia mapambio ya kinafiki. Ahadi hizi mpaka lini? Nataka kusimama,naomba tusimame pamoja. Nchi yetu inayoyoma.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:01 PM | Permalink |


Maoni: 10


 • Tarehe: 4:40:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Mija Shija Sayi

  Jeff, sisi raia ndiyo tumesababisha hali hii! tunatizama bila kukemea wanayotufanyia na ndiyo sababu wanapata jeuri.

  Hivi kweli wananchi tukimsimamia kidete mbunge wetu kiasi cha kutaka kumpotezea kazi yake kwamba tunataka shule au barabara nzuri jimboni mwetu unadhani hatafanya?

  Haya kazi kwetu wananchi, kusimama pamoja na Jeff au kumwacha peke yake tukidhani anajisumbua bure.

   
 • Tarehe: 4:38:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Tatizo kubwa nipale ambapo mtu atasubiri kuwa mtu mwingine atafanya. Watu mara nyingi hujaribu kujitoa katika makabiliano ya mambo magumu.Tunajipa moyo kuwa mwingine atafanya. halafu wengi tunadai kuwa maisha ni magumu kiasi kwamba ni vigumu kupata muda wakupigania Taifa wakati tumbo li tupu na shilingi haijulikani itapatikana wapi.Lakini hali halisi inachosha sasa. CHa muhimu ni kuweka wazi mambo ili kuweza kupigania mambo kwa uhakika na mwelekeo utakaotukomboa.

   
 • Tarehe: 5:17:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Halifa Mjengwa

  Ndugu Jeff
  Usitafute wa kusimama nawe, wewe simama na wengine watasimama. Ukianza kutafuta na wengine wataanza kutafuta sasa paka lini tutatafuta. Umemsikia Kitururu alivyosema? Kila mtu anategemea mwingine afanye. Kwa hiyo cha muhimu wewe simama na ukifanikiwa kusimama na wengine wakiona nao watasimama na kwa msingi huo wengi watasimama na naamini kwa hili wote tutasimama. Basi muda umefika tusiulize maswali mimi na wewe tusimame. Umesimama tayari ndugu Jeff mimi tayari....

   
 • Tarehe: 8:42:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ahsanteni wote hapo juu.Nimeshasimama,tuanze kuweka mikakati wazi.Mwisho umefika.

   
 • Tarehe: 3:25:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

  Tusimame wote bila kuangalia nyuma.Bila wewe na mimi Tanzania itaangamia, itakuwa nchi ya wageni

   
 • Tarehe: 3:32:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Michuzi

  naungana na wote hapo juu, pamwe na wewe. pia nakupa saluti kwa mistari aali. simama baba. sote na tusimame. play ur part, it can be done - if possible it will be done; if impossible it can be done...

   
 • Tarehe: 11:34:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

  Rastafarian imejaribu kusema ukweli wa hali halisi Afrika lakini cha kushangaza,watu wanachukulia kama wavuta bangi lakini mambo yanatokea,sisi waafrika tusipokuwa makini tutakiona cha mtema kuni.Binadamu tumebadilika tunauza utu wetu kwa sababu ya tamaa,tusipo simama nakupiga kelele,tutakiona.Jah live.

   
 • Tarehe: 4:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Good piece of work Jeff,

   
 • Tarehe: 4:43:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Salam zako luihamu !Jah bless us all

   
 • Tarehe: 11:41:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

  ndugu zangu naomba tuchangie mkutano wa wanablogu kutoka Afrika.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker