Afrika inateketea, Tanzania inazidi kuyoyoma kutoka kwenye ramani ya ulimwengu. Hivi karibuni itakuwa tena koloni. Koloni lisilo na mtawala. Watazame. Wanarudi kimya kimya. Wananchi wamekata tamaa. Wameamini maneno ya wageni, nyie ni masikini. Hamna mnaloweza kufanya bila msaada wetu. Akili zimetekwa nyara. Tunauana wenyewe kupitia rushwa,ufujaji wa mali, ubadhirifu. Tunapigana kuliko wanyama. Tumechoka,hayo ni maneno ya baadhi yetu. Mwenye nguvu ndio ataishi, hii ndio njia ya maisha yetu.
Kiongozi hajali tena wananchi wake. Anajali zaidi tumbo lake, la familia yake. Anapayuka majukwaani kwa sauti ya radi. Anaongopa bila aibu. Kijasho chembamba kinamtoka pindi tunapouliza maswali magumu, ziko wapi kodi zetu? Anachekacheka huku anashika tumbo lake,akichoka kushika tumbo anashika sharubu zake. Amejaa unafiki, ananuka uroho wa madaraka. Kavalia suti ya marumaru, anamkenulia mtoto aliye tumbo wazi, mtoto mwenye njaa kali.Kinywani kwake kajiwekesha kijiti cha kutoholea vijinyama kutoka kwenye meno. Yeye kashiba.
Huyu tuliyenae ndio mkoloni mpya. Ameshika fimbo,ameshika kisu kikali. Anatukata bila huruma. Anasema maneno yale yale ya mkoloni. Aibu machoni kwake haionekani, achilia mbali moyoni mwake. Anaitwa mtumishi wa umma wakati umma ndio unaomtumikia yeye. Hawezi hata kufunga mkanda kwenye gari lake. Mikoba yake hatuna budi kumbebea. Akitembelea jimbo lake tunatamani tupige deki barabara zote. Kazi yake ni kuweka sahihi mikataba asiyoisoma. Anapata ten percent. Anaua jamii yake. Midomo yake miekundu kama damu, imejaa damu. Maisha ya watu keyachezea. Utumishi huu utumishi gani?
Tafadhali nipatie kikombe cha maji, kiu kimenibana kupita kiasi. Moyo wangu umejaa hasira na huzuni. Najua ninachotakiwa kufanya, bahati mbaya ni kwamba siwezi kukifanya peke yangu. Naomba msaada wako. Simama na mimi nisimame, sote tumzonge adui. Tumpe heshima kama anastahili. Kama anastahili adhabu basi tusisite. Nimechoka.
Nimechoka kuona ndugu zangu wanaishi kizani. Eti wanaishi mijini. Ama kweli dunia hadaa na ulimwengu shujaa.Amani inamsaidia nani eti? Nimechoka kuona mbwa wa Ulaya ana maisha mazuri kuliko binadamu. Nimechoka kusikia mapambio ya kinafiki. Ahadi hizi mpaka lini? Nataka kusimama,naomba tusimame pamoja. Nchi yetu inayoyoma.
Jeff, sisi raia ndiyo tumesababisha hali hii! tunatizama bila kukemea wanayotufanyia na ndiyo sababu wanapata jeuri.
ReplyDeleteHivi kweli wananchi tukimsimamia kidete mbunge wetu kiasi cha kutaka kumpotezea kazi yake kwamba tunataka shule au barabara nzuri jimboni mwetu unadhani hatafanya?
Haya kazi kwetu wananchi, kusimama pamoja na Jeff au kumwacha peke yake tukidhani anajisumbua bure.
Tatizo kubwa nipale ambapo mtu atasubiri kuwa mtu mwingine atafanya. Watu mara nyingi hujaribu kujitoa katika makabiliano ya mambo magumu.Tunajipa moyo kuwa mwingine atafanya. halafu wengi tunadai kuwa maisha ni magumu kiasi kwamba ni vigumu kupata muda wakupigania Taifa wakati tumbo li tupu na shilingi haijulikani itapatikana wapi.Lakini hali halisi inachosha sasa. CHa muhimu ni kuweka wazi mambo ili kuweza kupigania mambo kwa uhakika na mwelekeo utakaotukomboa.
ReplyDeleteNdugu Jeff
ReplyDeleteUsitafute wa kusimama nawe, wewe simama na wengine watasimama. Ukianza kutafuta na wengine wataanza kutafuta sasa paka lini tutatafuta. Umemsikia Kitururu alivyosema? Kila mtu anategemea mwingine afanye. Kwa hiyo cha muhimu wewe simama na ukifanikiwa kusimama na wengine wakiona nao watasimama na kwa msingi huo wengi watasimama na naamini kwa hili wote tutasimama. Basi muda umefika tusiulize maswali mimi na wewe tusimame. Umesimama tayari ndugu Jeff mimi tayari....
Ahsanteni wote hapo juu.Nimeshasimama,tuanze kuweka mikakati wazi.Mwisho umefika.
ReplyDeleteTusimame wote bila kuangalia nyuma.Bila wewe na mimi Tanzania itaangamia, itakuwa nchi ya wageni
ReplyDeletenaungana na wote hapo juu, pamwe na wewe. pia nakupa saluti kwa mistari aali. simama baba. sote na tusimame. play ur part, it can be done - if possible it will be done; if impossible it can be done...
ReplyDeleteRastafarian imejaribu kusema ukweli wa hali halisi Afrika lakini cha kushangaza,watu wanachukulia kama wavuta bangi lakini mambo yanatokea,sisi waafrika tusipokuwa makini tutakiona cha mtema kuni.Binadamu tumebadilika tunauza utu wetu kwa sababu ya tamaa,tusipo simama nakupiga kelele,tutakiona.Jah live.
ReplyDeleteGood piece of work Jeff,
ReplyDeleteSalam zako luihamu !Jah bless us all
ReplyDeletendugu zangu naomba tuchangie mkutano wa wanablogu kutoka Afrika.
ReplyDelete