VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, October 28, 2006
UTALII WA MJINI

Utalii ni nyanja ambayo inaziingizia serikali za miji,majiji,vijiji,kata,wilaya nk kipato kikubwa kutokana na mapato yatokanayo na shughuli nzima ya utalii. Kama unavyoweza kuona katika picha hiyo hapo juu, gari hilo la manjano ni moja ya magari mengi jijini Toronto yanayofanya kazi ya kutembeza watalii. Jina maarufu la magari hayo ni "sight seeing vehicles".Toronto ni makao makuu ya serikali ya jimbo la Ontario na ndio jiji maarufu zaidi kushinda yote nchini Canada na inawezekana ndio linaongoza kwa shughuli za kibiashara na hivyo kuwa "commercial city headquarters"

Wakati utalii ukizifaidisha nchi chungu mbovu duniani, Tanzania bado inazembea sana kuhusu utalii. Wananchi wanaoishi kwenye "visima" vya utalii nchini Tanzania bado hali za maisha yao ni duni sana. Utalii wa ndani bado ni wa kusadikika huku nchi za jirani kama Kenya zikiendelea kufaidi "visima" vya utalii vilivyopo Tanzania kwa mfano mlima Kilimanjaro,mbuga za wanyama za Serengeti,Ngorongoro,Manyara nk kwa sababu watalii wengi hutua kwanza nchini Kenya na kisha kuingia mikataba na makampuni ya utalii ya Kenya kwa minajili ya kuwapeleka vilipo "visima" hivyo. Kampuni hizi za Kenya hazifanyi kosa lolote, zinatumia nafasi zinazojitokeza ambazo zingeweza kutokuwepo endapo wizara yetu ya utalii kwa kushirikiana na bodi ya utalii zingekuwa na mikakati endelevu kuhakikisha watalii wanatua Tanzania kwanza. Njia pekee ni matangazo na sio vipeperushi vinavyopigwa vumbi katika balozi zetu mbalimbali duniani.

Lingine ni ukweli kwamba serikali ya Tanzania kupitia wizara ya utalii imeshindwa kabisa kuyahifadhi,kuyatengeneza maeneo ya kihistoria ambayo ni maarufu duniani kwa kuleta wataliii. Mfano mzuri ni kama vile Bagamoyo. Kama uliwahi kutembelea Bagamoyo utakuwa uliona sehemu ambayo bado ina minyororo waliyofungwa mababu zetu enzi hizo za biashara ya utumwa. Nasikia alama kama zile za kihistoria ambazo zingekuwa chanzo kizuri sana cha utalii zinatokomea taratibu kama bado hazijauzwa kwa "wawekezaji" ambao hawana uchungu na historia yetu hata kidogo.Hawana sababu ya kuwa nayo.


Kuna tofauti gani kati ya Bagamoyo na Gore Island nchini Senegal sehemu ambayo kwa mwaka hushuhudia maelfu ya watalii? Watalii wangapi wanaenda mkoani Iringa kutembelea ngome ya Mkwawa? Wangapi wangemiminika huko kama ingekuwa ni sehemu iliyotengenezwa vizuri kwa minajili ya utalii? Utalii sio kutembelea mbuga za wanyama tu. Watu wengi hupenda kutembelea maeneo ya kihistoria(nikiwemo mimi). Tuamke sasa!
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 4:44 PM | Permalink |


Maoni: 3


 • Tarehe: 9:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

  Kaka Jeff, Naona unaota kitu ambacho kipo mbali sana na sisi, Huoni kwamba hata usafiri wa kutupeleka kazini ili tutumiwe kwa kipato kidogo hapa ni tatizo? Na haya mawaya ya umeme yanayonin'ginia ovyo itakuwaje na hilo 'basi la ghorofa liendalo ulaya' sasa wewe unataka tuanze na kuwatembeza "wazungu" mijini! itawezekana hiyo?
  Mabasi hayo ya 'topless' nimeyaona South Afrika, muulize indya anayaona bado ingawa amekuwa kimya sana siku hizi, yanapendeza sana. Fikiria ukifanya 'bethdei' yako ndani humo huku mkitembezwa mjini inakuwa furaha kubwa sana.
  Inabidi tujipange upya ili tuwakarimu wageni wetu vizuri.

   
 • Tarehe: 9:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Bwana Jeff, Blog yako safi, inavutia sana. Hongera mzee.Kuhusu huu utalii wa mjini hasa katika nchi zilizoendelea kama Canada, nchi zetu zinatakiwa zijifunze nazo. Kwa watanzania kama nyinyi mnaomiliki blog, ingekuwa ni bora kama mngekuwa mnaweka link mbalimbali kuhusu nchi mnazohishi hata wale walio nyumbani waweze kujifunza nao. Maana yangu ni kwamba kuna watu hawajui Ontario, au majimbo ya Canada, na habari nyinginezo kuhusu Canada ambazo labda kwa njia moja au nyingine zinaweza kuwasaidia watu waliobaki bongo waweze kupiga hatua.

   
 • Tarehe: 5:49:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Anyon,
  Nakubaliana kabisa na wewe.Nitakuwa najitahidi nisisahau kuweka links muhimu.Binafsi nimekuwa nikijifunza mengi kwa kufuata links kama hizo unazozizungumzia.Nashukuru sana kwa kunitembelea na kunikumbusha.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker