VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, November 23, 2006
MPAKA WAKATI MWINGINE....MATOKEO YAMETOKA!
Matokeo ya raundi ya kwanza kuelekea mwisho wa tuzo za Blog bora nchini Canada yametoka. Kama mnavyojua blog yangu ya kimombo African Perspective kwa mara ya kwanza ilikuwa imeteuliwa kuwania tuzo hizo katika kundi la blog bora za kitamaduni.

Kwa bahati mbaya blog hiyo haikuweza kuchaguliwa kwenda raundi ya pili ya mchuano huo. Unaweza kutizama matokeo kwa kubonyeza hapa.Je,hilo linakushangaza? Mimi binafsi limenishangaza lakini sina budi kukubali kushindwa ili niwe mshindani (wakati mwingine labda). Asiyekubali kushindwa........

Ninachojua hivi sasa ni kwamba wengi wenu mlinipigia kura. Idadi ya barua pepe,simu,ujumbe mfupi wa simu za mkononi nk zilitosha kabisa kunionyesha jinsi gani mlinipa kura zenu.Kwa hilo sina budi kuwapeni shukrani zangu za dhati.Ahsanteni sana sana.Kilichotokea upande wa pili,baada ya kura zenu kuhesabiwa sikijui na wala huenda nisije kijua milele.Tekinolojia bwana,zina mambo yake!

Kwa wale ambao,kwa sababu moja au nyingine,hamkuweza kupiga kura wakati huu,tutajaribu tena wakati mwingine,inshallah.Nitaendelea kuandika kwa kutumia hizi lugha mbili,kiswahili na kule African Perspective,kwa kiingereza.

Sasa kwa sababu siku zote huwa inaudhi kushindwa, kumpigia kura mtu wako kisha asishinde, nimeona nikupe burudani kidogo na wimbo huu hapa chini wa hayati Bob Marley unaoitwa Three Little Birds(Ndege watatu wadogo).Ahsanteni sana.


 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:20 PM | Permalink |


Maoni: 6


 • Tarehe: 2:22:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Mimi kwa mtazamo wangu bado wewe ni mshindi.Mimi nilizipitia zile blogu zote zilizokuwa zinashindana chini ya utamaduni .Na ya kwako bado inaendelea kuwa iliyo mshindi kwangu.

   
 • Tarehe: 8:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Jeff,

  Waliwahi kumshindanisha Maradona na Pele nani mchezaji wa karne? Akashinda maradona! Kwa hiyo usishangae. Kura zetu ulizipata!Hongera kwa pale ulipofikia.

  F MtiMkubwa Tungaraza.

   
 • Tarehe: 5:47:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

  Sina la kusema ila tu Nabii robert nesta marley kasema.long live jahrastafarian.

   
 • Tarehe: 4:24:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Wimbo umeshanifanya ni "Feel-Good" Asante Kaka.

   
 • Tarehe: 1:44:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Bwaya

  Nilizipitia blogu ulizoshindanishwa nazo. Hayo matokeo hayana uhusiano wowote na hali halisi.

  Nakupongeza kwa kupeperusha bendera ya Uafrika kikamilifu. Mimi naamini umeshinda mpaka hapo.

  Kazi ndio kwanza umeianza. Mwendo ni mbele kwa mbele.

  Naandika kukupongeza kaka. Hongera!

   
 • Tarehe: 4:48:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Maggid Mjengwa

  Jeff!
  Pamoja na matokeo hayo bado binafsi nakupa pongezi nyingi kwa ushindi unaotokana na kazi yako nzuri,
  Iko siku.
  /maggid

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker