VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, November 09, 2006
TUJENGE AJENDA SASA
Siku ya mkutano inazidi kukaribia.Swali ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara ni kwamba ajenda ya mkutano wetu ni nini? Pendekezo la mwanzoni lilikuwa kwamba tutakutana bila ajenda maalumu ili kutoa nafasi kwa wote kushiriki katika kutengeneza ajenda ya mkutano mwingineo. Kwamba tuachane na ukiritimba wa wachache kujifanya machinoo.Ambacho hatukukijua wakati ule ni kwamba inawezekana kabisa tukakutana huku tukiwa tayari na ajenda kibindoni. Tekinolojia bwana....we acha tu!

Kama kawaida,mwenzetu Ndesanjo Macha, ametupatia ufumbuzi wa suala hili. Bonyeza hapa usome ufumbuzi wenyewe na uanze moja kwa moja kushiriki katika uundwaji wa ajenda. Shukrani sana Ndesanjo.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:41 AM | Permalink |


Maoni: 14


 • Tarehe: 4:09:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  NINI MAANA YA DEMOKRASIA? KUFUTA UKWELI NA MAONI YA WATU? INACHEKESHA SANA. ALAFU UNAISHI NCHI ZINAZO HESHIMU DEMOKRASIA!

   
 • Tarehe: 4:42:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Anonymous mwenye details hizi hapa chini.Uhuru na demokrasia una mipaka.Ahsante

  Visitor Detail Unique Visitors

  Visitor ip3-157.champions-centre.hou.ygnition.net

  IP Address: 69.59.14.157

  Date: 10 Nov, Fri, 13:09:53

  Net Speed: Cable/DSL

  Organization: Ygnitio
  Networks

  Browser: Mozilla 1

  Continent: North America

  Operating System: Mac OS X

  Country: United States

  Screen Resolution: Other

  State / Region: Washington

  Screen Color: Other

  City: Seattle

   
 • Tarehe: 12:16:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  MIPAKA GANI? KUULIZA MASWALI? MACHINOO NI NANI? KATIKA SEHEMU ULIYOPO KUNA UHURU NA DEMOKRASIA NA HAKUNA MIPAKA KATIKA KIPENGELE HIKI NINA UHAKIKA UNAJUA HILO ILA UNASHINDWA KUKILI KAMA UMEKOSEA KUITA WENZIO MACHINOO! INAWEZEKANA NA WENGINE WANAKUONA WEWE NDIO MACHINOO, JE UNGEJISIKIAJE KAMA WATU WANGEKUITA HIVYO? NI USTAHARABU KUBAGUA WATU? JE NYIE WACHACHE SIO MACHINOO?

  TUNA MALIZIA KWA KUSEMA KWAMBA UNAWEZA KUWA MTU WA DINI, ELIMU NZURI, MAISHA MAZURI UNAYO LAKINI UKASHINDWA KUWA NA USTAHARABU NA HUU USTAHARABU HAUPATIKANI SHULENI NI MOJA KWA MOJA TOKA DAMUNI. SIO VIZURI KUBAGUA WATU NA KUWAITA MACHINOO.

  FREEDOM OF INFORMATION ACT INA UWEZO WA ATA KUJUA SIRI ZA CIA. NADHANI UNAJUA HILO NA ELIMU ULIYO NAYO SASA MIPAKA IPO WAPI? WEWE KUBALI KUWA UMEKOSEA KWA KUBAGUA WATU ATA KABLA YA HUO MKUTANO HAUJA ANZA.

  BY THE WAY HIZO HABARI HAPO JUU HAKUNA CHOCHOTE ULICHO PATIA SISI TUPO NCHI MOJA NA WEWE SASA FIKIRI.

  TUNAOMBA OMBI LA MSAMAHA TOKA KWAKO KWA KUBAGUA WACHACHE NA KUTUITA MACHINOO NA SIO KUWEKA HIZO HABARI HAPO JUU ATA KAMA UNGEPATIA TUNGE ENDELEA KUOMBA UWEZE KUOMBA MSAMAHA.

  ALUTA CONTINUA

   
 • Tarehe: 12:30:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

  Kaka Jeff,ninaomba kujua maana ya neno Machinoo,na kama kweli kunakubaguwana naona hamna haja ya mimi kuchangia katika mkutano huo.

  Asante.

   
 • Tarehe: 5:01:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger msangimdogo

  Baadhi ya nyakati huwa kuna mambo yanayomfanya mtu kuwaza utimilifu (sio utimamu) wa baadhi ya watu. Hivi kinachojadiliwa hapa mwanzo wake ni upi hasa?

   
 • Tarehe: 6:16:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Mija Shija Sayi

  Hata mimi sielewi kinachoendelea.

   
 • Tarehe: 6:36:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Sijui yameanzia wapi haya. Nilivyomuelewa Jeff ni kuwa anatetea haki ya wanablogu wote kushiriki kupanga ajenda. Jeff alipotoa wazo la mkutano angeweza kuwasiliana na wanablogu wengine wawili, watatu kisha wakapanga ajenda za mkutano kwa kuchukulia kuwa wao ndio wanajua zaidi na wana uwezo na haki ya kuamua ajenda sahihi kwa ajili ya wengine wote. Lakini kwakuwa haoni sababu za wachache kuchukua jukumu hilo kwa mtazamo kuwa wao wanajua sana, basi ndio likaja wazo la wale wote wanaotaka kushiriki kupanga ajenda wapewe uwanja wa kutoa mawazo.

  Sasa sijui kwanini imekuwa kama vile Jeff katukana. Wazo ni rahisi na liko wazi. Lakini inaonekana kama kuna ujumbe wa siri. Kama kuna watu walitaka kuchukua jukumu la kupanga ajenda kwa ajili ya watu wengine, basi watu hao ndio watachukizwa na kauli ya machinoo maana watajisikia kuwa ndio wanazungumziwa.

  Neno machinoo wala halikuwa sehemu kuu ya ujumbe wake. Anachosema ni kuwa tushirikiane kupanga ajenda. Kama kuna anayependa kufanya hivyo basi ashiriki badala ya kuanza kuzozana bila kujua mzozo umeanza wapi. Tushirikiane kufanikisha mkutano wetu.

   
 • Tarehe: 11:15:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Waungwana,
  Haki ya wanablogu wote kupanga na kupendekeza ajenda ndio nilichokuwa nakitetea na nitaendelea kukitetea.

  Pasipokuwa na uhuru huo ndio mwanzo au muendelezo wa nilichokiita ukiritimba na umachinoo.Yaani wachache kuhodhi muelekeo mzima kwa kuona kwamba wao ndio wanajua kila kitu na hivyo kuweka tu mezani mambo ambayo wanataka yajadiliwe(ajenda).Hayo yameshatokea sana katika jamii zetu na bado yanaendelea kutokea.Wachache kuamua maisha ya wengine yaelekee wapi na yawe vipi.Ni haki?

  Ili kuepuka kupita njia hiyo ambayo ndio imeifikisha hata nchi yetu ilipo ndio maana mojawapo ya ajenda kuu za mkutano huu ni kuona ni jinsi gani tunaweza kuanzisha upya ushirikishwaji upya wa wananchi (civil societies)kuamua wapi maisha yao yaelekee kwa kushiriki kikamilifu katika uundaji na utekelezwaji wa sera za nchi nk.Binafsi naamini kwamba blogs zikitumika vizuri,zinaweza kabisa kukidhi haja hiyo.Naamini wengi tunakubaliana katika hili.

  Ni wazi kwamba katika jamii zetu wapo watu watu machinoo(limeundwa kwa kiswahili kutoka katika maneno mawili ya kizungu (much-know).Unapochangia jambo fulani bila kuhodhi muelekeo wa kile kinachojadiliwa au kutendeka,unaposhirikisha na kushiriki na wenzako bega kwa bega (kwa kutumia vyema uhuru na demokrasia) huna sababu ya kujiona au kujihisi machinoo kwa sababu hauhodhi majukumu,muelekeo na hivyo kutobainisha matokeo kabla ya wakati.

  Sasa ili tufike tunakotaka kufika,nawaomba wote tushiriki katika kupanga ajenda.Baadhi ya mapendekezo ambayo yameshatolewa katika ule ukurasa wa ajenda ni mazuri sana,tuendelee kuchangia pale.

  Ukiweka "mapendekezo" ya ajenda sio kwamba umeweka "maamuzi". Moderator ambaye amependekezwa ndio ataweka vizuri mapendekezo yote na kisha kupanga,kwa kuzingatia muda nk,yapi yaanze,yapi yafuate nk.

  Ahsante Ndesanjo kwa kunisaidia katika kuwakilisha nia hii.Kwa yeyote ambaye maneno ukiritimba na machinoo yameakisi kama matusi kwake naomba radhi.

  Shime,tuelekeze nguvu katika maandalizi ya mkutano ambao umebakiza wiki moja tu hivi sasa.Mengi yanaweza kujadiliwa pale.

  Ukurasa wa ajenda ni http://conferences.wikia.com/wiki/Mkutano_Wa_Wanablogu_Wa_Tanzania.Tafadhali changia,weka ajenda.Ahsante.

   
 • Tarehe: 11:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Hamisi Mwinjuma, Glasgow

  jeff na wenzako,
  nyie endeleeni na maandalizi ya mkutano wenu.Huyo anony na luihamu nadhani wao ni machinoo na kuna watu wameshawahi kuwaambia hivyo.ukweli unauma na pia sidhani kama kuna mtu amelazimishwa kushiriki mkutano.Wabongo bwana...wenzenu wanaandaa mambo ya maana nyie kazi yenu kuweka sumu tu.Kaa kwako utulie na ulale

   
 • Tarehe: 12:48:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  TUNASHUKURU KWA KUOMBA RADHI NA HUU NDIO UNAITWA USTAHARABU.

  ALUTA CONTINUA.

   
 • Tarehe: 3:42:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Hamisi Mwinjuma, Glasgow

  Inasikitisha sana kuona kwamba bado tuna watu wagumu sana kuelewa mambo rahisi kama huyo Anony hapo juu.Kama unashindwa kuelewa point rahisi kama hizi utawezaje kutoa mawazo ya maana hata kwenye huo mkutano? Namshauri anyony wa hapo juu asishiriki kabisa mkutano huu.Utawarudisha tu nyuma wenzio.

   
 • Tarehe: 12:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

  Kaka Jeff/Ndesanjo asante kwan kunifungua macho.Tuendelee na Ajenda.

  Asante sana.

   
 • Tarehe: 5:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  nasema kwamba nafsi yangu haijalizika kama nyie mmelizika ni nyie, nataka aondoe kabisa neno machinoo tujue kwamba ameomba radhi ya kweli. ninakuheshimu sana mmiliki wa hii blogu,naomba uondoe hilo neno ili kuweka mambo sawa.

  alamsiki.

   
 • Tarehe: 7:00:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Anony:
  unaweza kutufafanulia kidogo ni jinsi gani mwenye blogu kakosea kwa kutumia hilo neno (ambalo tunapaswa kulitafsiri katika mazingira ya hoja aliyokuwa akiitoa) kiasi cha wewe kutaka aliondoe kabisa? Huenda kuna jambo ambalo unaliona wengine hatulioni. Mimi binafsi ningependa tuendelee kujadili ujumbe wake wa msingi aliokuwa akiutoa alipotumia hilo neno. Lakini kama kuna sababu ya kulijadili hili neno, hakuna ubaya. Ila ingekuwa vyema ukatoa maelezo zaidi ili tuone kwanini kuna umuhimu wa kutumia muda kulijadili. Sijaona maelezo yoyote ya msingi yanayonishawishi kuona kuwa 1. kuna sababu za Jeff kuliondoa 2. kutumia muda kujadili hili suala badala ya hoja kuu aliyokuwa akitoa Jeff (ya kuchangia kuandaa ajenda za mkutano wetu.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker