Friday, November 03, 2006
TUKUTANE SAA NGAPI?
La mgambo limelia,kuna jambo.Jambo lenyewe ni mkutano wetu wa kwanza wa wanablogu,wachangiaji,wasomaji,wananchi, mimi na wewe.Shukrani nyingi kwa wote ambao wameitikia wito huu kwa haraka na kwa moyo wote. Hii inaonyesha kwamba inawezekana na tunaweza!
Mpaka hivi sasa nadhani wote tumekubaliana na tarehe iliyopendekezwa ya 18 November,2006. Kikubwa kinachobaki ni kuamua muda wa mkutano. Kutokana na sababu mbalimbali kama mahali, upatikanaji wa umeme(hii inatia hasira) nk imeonekana ni wazo zuri kama "demokrasia" ya kura itatumika. Hatuna budi kutenda tunachohubiri,demokrasia.
Hivyo basi, mwenzetu Ndesanjo Macha, mwanamapinduzi ya tekinolojia, kwa kutumia tekinolojia ijulikanayo kama Doodle, ameturahisishia jinsi ya kuendesha zoezi hilo la kuchagua muda ambao wengi watakuwa wameuchagua. Tafadhali bonyeza hapa uchague muda mzuri wa mkutano.Ukifika pale kumbuka kwamba tarehe ambayo mpaka hivi sasa imeonekana kushinda zingine zote ni 18 Novemba,2006. Mida inayopigiwa kura ni saa sita au saa nane mchana kwa saa za Tanzania.
Naomba radhi kama kuna usumbufu wowote.Kumbuka tu kwamba hii ni mara yetu ya kwanza na tuna mengi ya kujifunza kwa sababu safari ndio kwanza tunaianza. Pia kama hujasoma bado alichoandika Ndesanjo kuhusu tekinolojia tutakayotumia, mitabendi, nk basi bonyeza hapa. Usisahau kumpa habari hizi mwenzako ambaye unadhani hajazipata bado.
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:25 AM
|
Permalink |
-
Nami nimefafanua kidogo pale kwangu kuwa nilikosea nikaweka tarehe mbalimbali. Nimefuta na kuonyesha kuwa tarehe ya novemba 18, saa sita au saa nane na kuwa zile tarehe nyingine watu waziache tu kama vile hazipo pale. Muhimu ni watu kuweka majina yao pale ili kura zihesabike.
-
Ahsante Ndesanjo kwa ufafanuzi.Nimeona kura zimeanza kuingia.Walinzi wa makbrasha ya kura wapo?
-
Kura tutazisafirisha kwa baiskeli kwenda wilayani! Yatakayotokea huku katikati ya njia usiniulize!
-
Ningependa tupate ufafanuzi wa uhakika kuhusu saa za upatikanaji wa umeme wa "kijiko" Tanzania. Je ni kweli kuwa umeme utapatikana saa moja ya usiku na sio mchana siku hiyo ya tarehe 18 Novemba?
-
Mzee Ndesanjo umeme unapatikana saa moja usiku,siku za karibuni wamekuwa wakiwasha na kukata muda wowote,kwahiyo basi naomba kama inawezekana tukutane siku hiyo lakini tubadilishe muda,iwekuanzia saa moja usiku.Jah Live.
-
Mimi tarehe 18 ni sawa kabisa. Lakini kama mkibadilisha, iwe Jumamosi au Jumapili ndio napatikana mchana. Asante sana Jeff wazo zuri
-
Mimi tarehe 18 ni sawa kabisa. Lakini kama mkibadilisha, iwe Jumamosi au Jumapili ndio napatikana mchana. Asante sana Jeff wazo zuri
-
Ratiba ya umeme nadhani kwa wakati huu imekuwa si ya uhakika sana, sababu wamekuwa wakiendelea kupunguza makali ya mgao, tatizo ni kuwa hawana ratiba ya kueleweka, yaani wanawasha na kukata wakati wowote. Nadhani hali ndio imekuwa mbaya sana kuliko hata wakati wa mgao wenyewe ulipotangazwa rasmi sababu kipindi kile ilikuwa inajulikana wazi kuwa muda fulani hadi muda fulani ndio muda wa mgao. sasa kwa sasa hujui watawasha muda gani na kukata muda gani, kwahiyo tukubaliane tu kuwa iwe wakati huo, kwa wale watakaobahatika, maana hata ambao hawatabahatika, bado watashiriki kupata taarifa.
Hoja hapa ni kuona namna tunaweza kujenga jamii ya mtandaoni ambayo itakuwa na mchango katika kuamsha au kuyeyusha mawazo mgando ambayo yangali vichwani mwa jamii, na kama tunakubaliana katika hili, tutakubaliana pia kuwa ujenzi wa jamii ya namna hii sio suala la siku moja bali mchakato wa muda mrefu sana. Ninachomaanisha hapa ni kuwa kwa wale ambao watakosa kikao hicho, naamini watakuwa na nafasi ya kutoa michango yao kupitia blogs mbalimbali na yakasomwa pia, na hata wanaweza au niseme tunaweza kuamua kuitisha mkutano mwingine wakati wowote ule tukitaka.
-
nashauri tuangalie kadiri muda unavyokaribia ndio tuamue saa, pengine tanesco watabadili mgao, hapa nilipo saa sita ya nyumbani ndiyo sawa, saa moja ya jioni itakuwa minara ya saa tisa hivi za usiku. Tanesco wakigangamala haidhuru tutakesha kusubiri kikao.
-
kaka Msengi, maoni hayo hapo chini, nimemtumia Kaka Ndesanjo!!
Kaka Ndesanjo na wanaharakati wote wa blogu za kiswahili, nimesoma haraka hakara juu ya taarifa za mkutano wa wanablogu wa Tanzania, nilikuwa safari ya mkoa wa morogoro maeneo ya vijijini kwa takriban mwezi na nusu hivi, sasa jana usiku nimerudi na leo katika pita pita yangu nimekutana na taarifa hiyo. Kwa kweli nakubalinana na wazo la kufanya mkutano huo kuwa tarehe 18/11 kuanzia saa sita mchana na ikiwezekana mpaka saa 9 alasiri. Nilitamani sana kupiga kura lakini naona niko nje ya wakati, si mbaya pia.
Napongeza sana wazo la mkutano huo!!!
Nami nimefafanua kidogo pale kwangu kuwa nilikosea nikaweka tarehe mbalimbali. Nimefuta na kuonyesha kuwa tarehe ya novemba 18, saa sita au saa nane na kuwa zile tarehe nyingine watu waziache tu kama vile hazipo pale. Muhimu ni watu kuweka majina yao pale ili kura zihesabike.