VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, November 05, 2006
UNGEFANYAJE?

Maandalizi ya mkutano wetu bado yanaendelea. Umuhimu wa kupiga kura yako ili kuchagua muda bado upo na kura yako inahitajika sana. Hivyo bonyeza hapa upige kura yako.

Michezo ya kwenye tarakilishi(computer games) ni mojawapo ya nyanja za maendeleo ya kimtandao ambayo zinazidi kukua kwa kasi sana. Ingawa wanajamii wengi wameishaanza kuihusisha michezo hiyo na mporomoko wa maadili miongoni mwa wanajamii hususani vijana, baadhi ya michezo hiyo ina mafunzo mazuri na pia inaburudisha.(?)

Wiki chache zilizopita,
Shirika La Umoja Wa Mataifa Linaloshughulika na Watoto (UNICEF) lilizindua mchezo wa kwenye tarakilishi unaolenga katika kutoa elimu juu ya ukimwi katika kujikinga na pia kupima. Mchezo huo ambao unapatikana katika lugha ya kiswahili na kiingereza umepewa jina la Ungefanyaje.

Basi kama wewe ni mpenda michezo ya kwenye tarakilishi bonyeza hapa uuone mchezo wenyewe. Mwisho,nini maoni yako kuhusiana na michezo hii ya kwenye tarakilishi? Unadhani njia hii ni muafaka katika kufikisha ujumbe kwa vijana wetu ukizingatia kwamba upatikanaji wa mtandao bado ni adimu?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:30 AM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 2:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

    Kwa mtazamo wangu,kama kweli tunakipenda kiswahili kwanini katika kurasa ya kupigia kura imeandikwa kwa lugha ya kingereza?

     
  • Tarehe: 9:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Luihamu:
    teknolojia tunayotumia imetengenezwa na wazungumza kiingereza. ndio maana nasi tunahitaji kujifunza haya mambo ili tuunde zana zetu.
    Blogpost nayo imeundwa kwa kiingereza ingawa tunaitumia kuandika kwa kiswahili. Hii haionyeshi kuwa hatukipendi kiswahili. Tunatumie barua pepe kwa Yahoo! ambayo nayo imeundwa na wazungumzaji wa kiingereza, haina maana kuwa tunachukia kiswahili ndio maana tunatumia Yahoo!

    Watengenezaji wa ukurasa ule wa kupigia kura wangekuwa wameweka siri ya kanuni ya ujenzi wa zana ile (source code) huenda tungeweza na tungekuwa na haki ya kubadili.

    Ukiona hapo kwenye maoni yako panasema, "Luihamu said..." Kuwepo kwa neno la kiingereza "said" kunamaanisha kuwa hupendi kiswahili?
    ---

    Mkutano wetu: Naomba tuongeze bidii kuamua ajenda na mambo mengine. Inadaiwa kuwa wabongo kiswahili kirefu sana, wakati wa kutenda ukifika, watu wanatokomea. Tunaweza kuwa na kiswahili kirefu na matendo marefu pia, au sio?

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker