VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, December 17, 2006
MWANABLOG,UNAWEZA KUSHITAKIWA?
Tulipokutana tarehe 18 mwezi uliopita na kuweka historia mpya katika ulimwengu wa blog za kitanzania, mojawapo ya yaliyokubaliwa na kupitishwa na wajumbe karibuni wote kama sio wote kabisa ilikuwa ni suala la nidhamu katika lugha na maandishi tunayoyatumia,utafiti makini wa kile tunachoandika , kutunza heshima na utu wa binadamu wenzetu (wale tunaoandika habari juu yao) na matumizi muafaka wa kazi za watu wengine yakiwemo maandishi,video, picha nk.

Masuala hayo hapo juu na mengineyo mengi yamekuwa yakiongelewa mara kwa mara kuhusiana na tekinolojia hizi za kisasa zinazoruhusu uandishi wa raia ambao unasemekana kuwa wenye uhuru kuliko ambavyo imeshawahi kutokea.Masuala ya sheria, haki za binadamu, muelekeo wa tekinolojia hizi, matumizi yake kama vimulika vya jamii,faida na hasara za blogs huwa ni ajenda zisizoonekana kuwa na mpaka.Mijadala mbalimbali bado inaendelea.

Hivi karibuni nimejaribu kufanya uchunguzi kidogo tu kuona nini kimeshatokea baina ya kile ninachoweza kukiita mapambano baina ya mkono wa sheria na blogs. Kesi moja ambayo imeanza kuvutia wengi huku Marekani ya Kaskazini ni
hii hapa inayohusu matumizi ya picha zilizopigwa na watu wengine bila kutaja wazi chanzo(source) chake. Zaidi ya kesi hiyo maswali kama haya hapa chini ni muhimu kuyazingatia kama wewe ni mwanablog na mkereketwa wa uhuru huu wa upashanaji habari nk.

Je unaweza shitakiwa kwa maoni ambayo wasomaji wako wameacha kwenye blog yako?
Soma kesi hii.

Je ukiweka kiungo cha; kwa mfano video ya matusi unaweza shitakiwa? Soma hapa pia

Je nini kinaweza kutokea endapo wanafunzi wataacha maoni ya aina fulani kwenye blog na wakuu wao wa shule wakayapitia? Unadhani jambo kama
hili hapa ni sawa?

Tuwe makini.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:17 PM | Permalink |


Maoni: 6


 • Tarehe: 8:39:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

  Ahsante jeff,
  Haya mabo ni moja yaliyozungumzia katika mkutano wa GV.Mwanblogu wa wa iraq Salam na Preetam waliongeeea swala hili kuhusu kublogu bila kutumia jina halisi.Alisema kuwa kuna wanablogu katika nchi fulani hasa zenye matatizo ya kisiasa hawaitaji kujulikana majina yao wanapokwa wakiblogu,pamoja na kwamba kuna teknolojia mabayo ainweza kukufichua wewe ni nani na upo wapi.

  Ndesanjo hapa naomab utufanunulie masuala ya kisheria katika huu uandishi wa kiraia

   
 • Tarehe: 2:02:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger John Mwaipopo

  Jeff,
  Ingawaje haya masuala yanawataalamu wake, kama wakina Michuzi na Makene, na masomo yao ya Media Law and Ethics, ni wakati sasa tukumbuke tu kublog ni teknolojia huria. Basi Huria Isiwe Holela. Kushitakiwa yawezekana kabisa.

   
 • Tarehe: 9:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Bwaya

  Jeff,

  Asante kwa kutukumbusha jambo hili muhimu.

  Tusijejikuta tunakuwa waandishi huria walioparaganyika. Sheria zinazotawala mambo haya ziwe wazi tusijejitia kitanzi bila kujua.

   
 • Tarehe: 5:39:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Michuzi

  Jeff!

  maneno bomba. ila mbona umekuwa mvivu/bize sana siku hizi? hii ngoma ina mwezi sasa hujapiga ingine. kulikoni?

   
 • Tarehe: 6:05:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Jeff, mada muhimu sana kwetu. Ngoja nami nikae chini niandike kidogo juu ya hili. Nakubali kuwa uhuru usije ukawa holela. Uhuru na wajibu vinakwenda sambamba. Na kama ulivyosema lazima kuwa macho, mtu asidhani kuwa blogu ziko juu ya sheria kama alivyo rais wa Tanzania!

   
 • Tarehe: 7:37:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Duh Jeff! umepotelea wapi?

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker