VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, December 03, 2006
SAIDIA WATOTO WA AMANI

Wiki iliyopita,kupitia kitabu changu cha wageni, nilipata ujumbe kutoka kwa mwanadada Valerie Johnson(30) ambaye ni mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalojulikana kama Amani Children's Home (Nyumba ya Watoto ya Amani) lenye makao yake kule Moshi,Tanzania.

Ujumbe wa Valerie kimsingi ulikuwa umeelekezwa kwa jumuia nzima ya wanablog wa kitanzania popote tulipo duniani.Nia ni kuomba kuungwa mkono kwa kile anachokifanya nchini Tanzania kujaribu kunusuru maisha ya watoto wa mitaani na wale ambao wamejikuta ni yatima baada ya wazazi wao kuchukuliwa na ugonjwa hatari wa ukimwi.Misaada mbalimbali ya hali na mali ndio vitakavyofanikisha maendeleo ya taasisi kama hii ya Amani.

Ni wazi kwamba tatizo la watoto wa mitaani na yatima linazidi kushamiri siku baada ya siku.Huu ni ukweli ambao hatuwezi wala hatupaswi kujaribu kuupa kisogo.Kwa bahati mbaya sera za kiserikali juu ya tatizo hili zimegeuka kuwa "bubu".Haishangazi kuona kwamba matatizo kama haya yameachiwa taasisi zisizo za kiserikali pekee jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa jamii ya leo,kesho na keshokutwa.

Wakati tukiendelea kushiriki katika kuiamsha serikali kuhusiana na sera zake kuhusu jamii ya watoto yatima na wa mitaani, tunaweza kuanza kujitolea kusaidia taasisi kama hii ya Amani.Kwa habari zaidi juu ya kituo hiki cha Amani tembelea tovuti yao kwa kubonyeza hapa. Pale utaweza kujisomea mengi kuhusiana na kituo hiki ambacho kina umri wa miaka takribani mitano sasa.Unaweza pia kupata mawasiliano na kituo hicho.Kumbuka kutoa ni moyo na sio utajiri.

NB:Pichani ni baadhi ya watoto wa nyumba ya Amani na ni kwa idhini ya Valerie Johnson
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 9:54 AM | Permalink |


Maoni: 5


  • Tarehe: 2:07:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Ndesanjo Macha

    Tumekupata Jeff. Nitatazama kazi zao kwa undani zaidi ili kujua ni vipi mtu anaweza kuwaunga mkono.

     
  • Tarehe: 9:58:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Innocent Kasyate

    Jeff mie niko Moshi nitakitafuta hiki kituo nipate kuona kwa macho yangu kinachofanyika pale.

     
  • Tarehe: 10:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Innocent,
    Hilo ni wazo la maana.Tafadhali watembelee kisha utoe muhtasari wako.

     
  • Tarehe: 5:11:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Rama Msangi

    Hapa ndipo tunapojikuta tukikubaliana kuwa kuna sehemu jamii inatutambua sisi wana blogi na inatutegemea pia.Inno nadhani ukishakitembelea utatueleza kile ulichokiona na si ajabu kutueleza pia namna nzuri ya kuweza kuwasaidia ndugu zetu hao

     
  • Tarehe: 4:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    watoto anaosaidiwa wasiwe kwa ubaguzi bali waangaliwe wenye vigezo sitahili kwani inaonyesha bado kuna watoto wengi sana mitaani waishio katika mazingilamagumu sana. na selikari iunge mkono kusaidia taasisi zisizo za kselikari kupunguza idadi ya watoto waishio katika mazingira magumu.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker