VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, January 15, 2007
MGOGORO WA DARFUR-TUMLAUMU NANI?

Bara letu la Afrika limeshuhudia majanga makubwa kila mara. Imefikia mahali kila janga,hangaiko la binadamu na mengineyo yamepewa sura ya "Afrika". Bara letu limekuwa ndio kisima na kiini cha kila aina ya uharamia. Haikunishangaza wakati Katrina ilipogonga kuta za New Orleans kule Marekani na serikali ya Marekani kushindwa kuwahudumia wananchi wake, walalamikaji walisikika wakisema "ah, itakuwaje jamani,hapa sio Afrika bwana,ni Marekani"!Maneno yale yalimaanisha pengine ni sawa kwa majanga kama haya kutokea huko Afrika na sio kwingineko.Ingawa janga la Tsunami lilifika pia Afrika, kuua watu na pia kuharibu mali nk hakuna aliyetaka kusikiliza wala kuwasaidia walioathirika. Lakini unakumbuka nguvu iliyopelekwa huko Banda Acheh?Unadhani ni kwanini?

Mifano ya migogoro ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo imewahi kulikumba bara letu la Afrika na bado inalikumba ipo mingi na ina sababu nyingi.Wanazuoni,wanahistoria,wachumi,walimu,wanafunzi na wengi wanaohusika wanayo maswali na majibu kedekede kuhusu kwanini Afrika,kwanini sisi?Majibu mengi huzua maswali zaidi.

Mgogoro wa Darfur ni mfano hai wa migogoro mingi iliyopo barani mwetu. Mgogoro huu wa Darfur ambao eti kiini chake ni ubaguzi, ungali unaendelea,ungali unakatisha maisha ya maelfu na ni mfano mzuri wa jinsi gani sisi waafrika tunavyojiweka katika ramani ya ulimwengu. Ni nani alaumiwe kuhusiana na mgogoro wa Darfur? Jibu rahisi ni kwamba viongozi wetu na wengineo wenye uchu wa madaraka. Hawa ndio wanavipa faida viwanda vya silaha vya magharibi na kutoka nchi za Asia kama China,Japan nk.Viongozi wetu ndio wanaotia sahihi mikataba ya silaha za maangamizi badala ya kutia sahihi masuala ya kiuchumi na maendeleo.

Ni kwanini viongozi wetu hawajiulizi maswali kama nini mchango wa nchi kama Uchina katika migogoro yetu barani Afrika? Viongozi wetu wanapoikumbatia China kama mwambata mkuu wa biashara wanajua wanafanya nini? Hivi ni kwanini hakuna anayesema wazi kwamba China ilikuwa na mchango mkubwa sana katika mauaji ya halaiki ya Rwanda kwasababu mapanga yaliyotumika yalikuwa yametengenezwa Uchina? Endapo China ingeuliza mapanga yote haya ya nini na kusitisha "order" ile nini kingetokea? Ni nani anayeuzia silaha wanamgambo wa janjaweed? Kwanini huyo asiwe ni adui yetu mkubwa? Nini viongozi wetu wa bara la Afrika wanafanya ili kutokomeza vita visivyokwisha barani Afrika?

Kimsingi, siamini kama kuna kitu kinachoitwa jamii ya kimataifa.Kilichopo ni mataifa yanayoshindana ulimwenguni. Marekani, China,Japan, Canada,Uingereza, Urusi,Italy nk si washirika wa chochote bali washindani. Sasa kama wao kwa wao wanashindana,inakuwaje viongozi wetu wanadhani au kuhadaika kwamba baadhi ya nchi nilizozitaja hapo juu na nyinginezo nyingi ni marafiki zetu? Kwanini wasitazame kwa makini historia? Nani washauri wao?

Viongozi wetu wa Afrika lazima watambue hilo na kuunda jamii yao wenyewe ambayo itaongozwa na kulindwa na wao wenyewe wakishirikiana na wananchi(sisi). Lazima pawe na nia ya pamoja ya kukomesha mauaji holela na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu tunaoushuhudia hivi leo. Lazima tujilaumu sisi wenyewe kwanza.Lazima tukasirike na kuamua kutokuwa wanyonge na masoko ya silaha holela,madawa ya kulevya,madawa yasiyokuwa na viwango na mengineyo.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:36 PM | Permalink |


Maoni: 6


 • Tarehe: 11:45:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Boniphace Makene

  Jeff salam za mwaka 2007, pili nichangie sasa, nitatumia mfano wa Tanzania. Kupata muungano wa mawazo na misimamo katika Afrika inahitaji kuwa na viongozi vichaa. Hivi unapokuwa na kiongozi anatoka CUba kwenye NAM kisha anaenda kukumbatiana na George Bush nini ishara yake? Hii si picha nyinginev ya Afrika? Vipi kuhusu nchi kupelela vikosi Lebanon, je Majeshi ya Afrika na nchi hizi haziwezi kukaa na kutumia rasilimali za ndani kukomesha mauaji hayo? Nini mchango wa ndani uliowekwa kwa ajili ya Darfur? Je, siku zote tutegemee nguvu kutoka nje wakati tunaoharibu mambo ni sisi wenyewe? Na, je hatuna uwezo hata wa kutatua mambo yanayiotuhusu sisi kwa sisi hadi tupewe faranga na wanaoyasababisha? Nani adui wa kweli na rafiki katika Bara hili? Tuna kazi ya kwenda.

   
 • Tarehe: 2:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

  Inasikitisha sana mambo haya kuendelezwa!.
  Hatujui Mheshimiwa wetu Kikwete akikutana na Al Bashir huwa wanaongea nini? Kile tunachotaka sisi amwambie au kuna kingine anachomwambia?
  Leo nimesikia ati Sudani, anayekumbatia na kulea mauaji ya Darfur anasubiri kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Afrika! kichekesho, kittuko na vilevile ni udhalilishaji. Sijui hawa maraisi wa afrika kusini mwa sahara wanakubali vipi watu wanaoua watu wa asili yao kwa dhana ya ubaguzi leo wanakuwa viongozi wenu!je wakikuangamizeni wote mtasema nini au mtalalamika kwa nchi za magharibi wakupeni msaada.
  Sitegemei kama Sudani watapewa hicho kiti kabla ya suluhu ya darfur kufanyika.

   
 • Tarehe: 10:07:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Makene,
  Kheri ya 2007 pia.Maswali yako ni halisi kabisa.Inashangaza sana kuona tunaowaita "viongozi" wanaonyesha kuwa ndio wanahitaji zaidi kuongozwa!

  Mloyi,hilo la Sudan kutaka kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Afrika(tamthilia)linashangaza lakini linawezekana kabisa barani Afrika.Tusubiri tuone.

   
 • Tarehe: 2:26:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Sudan kutokana na mafuta yake imewafanya wachina waangalie pembeni. Inaweza kutumia ndoano ya mafuta ukasikia nchi kibao tu za Afrika zikasapoti Sudan kuchukua uongozi. Si unakumbuka hata Idi Amini alikuwa kiongozi katika kipindi ambacho watu hasa viongozi walijua anafanya nini Uganda?

   
 • Tarehe: 5:35:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Happy new year Jeff na wasomaji wako,
  Nimepokea taarifa za JK kuja hapa UK kwa furaha, bahati mbaya sana sikuweza kwenda kumuona .
  Kilichonihuzunisha ni taarifa kwamba aliitwa na Tony ili wajadiline kuhusu zile rada mbovu walizotuuzia !
  Lord forbid us !
  Hawa watu wataendelea kutufanya hivi hadi lini ?
  Hope justice will follow its course hasa kwavile michoro hiyo inaonekana ilimhusisha kuanzia Tony hadi Ben
  Be blessed

   
 • Tarehe: 7:57:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Hawa wasudani naona walikosea kutaka kuwa na idea za PanArab nation.

  Kwanza ukiwaangalia waarabu wa Sudani na wale tunaowaona Lebanoni au Iraki utaiona tofauti. Nashangaa sana kumuona mwanasfalsafa wa Pan Arab kama Al Turabi... mweusi kuliko mimi tofauti ni kuwa yeye hupendelea kuvaa kiremba.

  Anyway, hawa jamaa na ka-imperialism kao kwa watu wa ndani ya mipaka yao katashindwa.

  Indonesia walijaribu kuwa na kamfumo kama ka Sudani kwa East Timor, Aceh na West papua, matokeo yake wenyewe wanarudisha majeshi.

  Hata sasa Sudani inaweza kutengemaa wakiondoa dhana potofu kwamba kuna waarabu sana na watwana wanaoweza kutengwatengwa. Wote ni waafrika, wagawane sawa mapesa ya mafuta na walioko kwenye mavumbi Dafur nao wapewe angalau vizahanati na mafao mengine mengine.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker