VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, January 17, 2007
TOVUTI YA "UHURU"....MMMH!


Waingereza wanao msemo usemao "Beauty is in the eyes of the beholder".Maana halisi ya msemo huo ni ukweli usiopingika.Lakini pia kuna wakati umma mzima unaweza kukubaliana kwamba kitu au jambo fulani sio kizuri. Upo hata wakati binadamu fulani fulani hukubali kwamba wao ni "wabaya" aidha wa sura au roho. Nadhani unakumbuka kwamba Tanzania iliwahi kuandika historia kwa kuwa na mashindano ya "watu wabaya".Kama ilivyotegemewa wanaume ndio waliojitokeza. Mpaka leo hii sijawahi kukutana na mwanamke aliyekiri kwamba yeye ni "mbaya".Natumaini ushawahi pia kusikia mtu akijitapa kwamba yeye ana roho "mbaya".Watu wengi walishikwa na mshangao pindi shindano lile la aina yake la Tanzania lilipotangazwa.

Mshangao haukuishia kwenye kujitokeza kwa wingi kwa washiriki wa shindano la kumtafuta mtu mbaya kupita wote bali lilinoga pale baadhi ya washiriki walipopinga matokeo. Walisema ah yule aliyeshinda bwana kapendelewa,mimi ndio mtu mbaya kushinda wote!Yule mzuri kabisa. Bado sijasahau jinsi ambavyo mshindi wa shindano lile la "mtu mbaya" kushinda wote (nakumbuka aliitwa Masoud kama sikosei) alipoanza kufuatwa fuatwa na vimwana wa kila aina wakitaka penzi lake(au hela zake?) Kama wote tulikubaliana na uamuzi wa majaji kwamba Masoud alikuwa ni mbaya kuliko washiriki wengine kama Mzee Jangala,Remmy Ongala na wengineo inatokana na msemo wa hapo juu kwamba beauty is in the eyes of the beholder.

Tukiachana na uzuri au ubaya wa wanadamu(wengine wanasema ni dhambi kukosoa kazi ya mungu), siku hizi si ajabu ushasikia zawadi zikitolewa kwa tovuti bora za mwaka katika nyanja mbalimbali. Best designed websites huwa ni mojawapo ya kipengele ninachokipenda sana. Hivi karibuni nimesikia kwamba kuna tuzo zinaandaliwa kwa ajili ya tovuti (sio blogs ingawa kiufundi blogs ni tovuti) mbalimbali za kitanzania.Keti chini usubiri.

Wakati maandalizi yanaendelea naomba leo niseme wazi kwamba,kwa mtizamo wangu, tovuti ya gazeti la uhuru la Tanzania,mojawapo ya magazeti makongwe kabisa nchini Tanzania inanipa kizunguzungu na kwa kiasi kikubwa inanipa simanzi nikizingatia kwamba Uhuru ni gazeti linalomilikiwa na Chama Tawala.(mbona hii kidogo inavutia?) Kwa rasilimali walizonazo, jamaa wa uhuru wanaweza kabisa kuwa na kitu bora.Hivi ni nani mkarabati wa tovuti hii? Tafadhali, itengenezeni jamani.Tunataka tusome sera na ajenda zenu(hata kama zimejaa longolongo za kisiasa) bila kupata maumivu kama ilivyo hivi sasa.Unasemaje msomaji?

Pichani juu ni mimi kutokana na e-mail moja niliyowahi kutumiwa,nikaambiwa nitizame moja kwa moja kwenye monitor yangu kisha nitabasamu ili nipigwe picha.Nilifuata maelekezo na matokeo yake ndio kama hayo hapo juu,nikageuka kuwa mzungu!
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:02 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 2:37:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Simon Kitururu

    Jeff, umependeza hapo pichani!:-)

    Si unajua ni mwiko kuwaambia watu kuwa huriziki na mwonekano wao. Hasa wanawake inasemekana kuwa ukitaka uhusiano wako ufane, wasifie ,kuanzia kuvaa kwao mpaka muonekano kila mara iwezekanapo. Hii ni hata wakikuambia niambie ukweli!Ukiwaambia ukweli hata kama wanakubaliana na wewe inasemekana kuwa huo ni mwanzo wa wao kufikiri kuwa huvutiwi nao kisawasawa. Lakini sijui kama hili jambo limehakikishwa kitaaluma!Pia inasemekana katika kauli mwanaume hutumiazo kumpata mwanadada asilimia kubwa huhusisha kauli za kumuhakikishia uzuri wake wa nje na jinsi unavyo mnasa kuliko uzuri wa roho na tabia.

     
  • Tarehe: 1:03:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger SaHaRa

    Lakini uzuri si lazima uwe wa physical appearance. Kama ulivyosema kuna issue ya pesa. Pia kuna ingine ya power and confidence. Ndio maana unaona kijitu kifupi amekamata ki-mobitel chake kirefu kama Mlima Kilimanjaro. Lakini utakuta kijamaa na limtu fulani hivi.

    Na kwa wengine sisi ni intelligence. Kwa mimi binafsi, yaani sidhani kama kuna kitu kinachovutia (kwa mwanaume) kama ambition, intelligence - na sense of humour. Hata kama una kibiyongo ... ;-)

     
  • Tarehe: 11:27:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Simon,
    Lazima kuna sababu kwanini wenzetu wanawake wanaamini kwamba wote ni wazuri.Je sisi wanaume ndio sababu?

    Sahara,
    Umenena vyema.Nadhani tunaweza kukubalian a kwamba kila mtu anacho chake kinachomvutia kwa mwingine.Na kwa sababu inasemekana hakuna binadamu aliyekamilika au mwenye vyote basi kinachotakiwa kufanyika ni kuchukua yale mazuri na kuachana na mengineyo.Au unasemaje?

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker