
Sifa moja kubwa nchi ya Canada iliyonayo ni kwamba ni nchi yenye baridi sana.Watu wengi wanaoishi jirani na Canada (Marekani) huwa hawataki kuitembelea Canada kwa sababu wameshasikia kwamba kuna baridi kupita mfano. Lakini ukweli ni kwamba Canada sio nchi yenye baridi kushinda zote ulimwenguni.Maeneo mengi ya Canada hususani kusini mwa Canada yana viwango vya baridi karibuni sawa tu na miji mingi ya Marekani.Mahali ambapo pana baridi kushinda sehemu zote duniani ni mahali panapojulikana kama Vostok (kituo cha utafiti cha warusi) na pia Plateau Station huko Antarctica. Olymyakon,Russia pia pana baridi kuliko Snag,Yukon kaskazini mwa Canada ambapo ndipo panapoifanya Canada ikimbiwe na wasiopenda baridi. Kiwango cha baridi cha chini kabisa ambacho kimewahi kurekodiwa huko Snag,Yukon ni Fahrenheit -81.4.
Kama ambavyo picha ya juu inaonyesha,sio kila mtu anayachukia majira ya baridi kali.Wapo wanaofurahia. Tatizo kubwa linakuja kwetu sisi wakuja ambao michezo ya kwenye barafu sio yetu na tunaiogopa kama ukoma (kuvunjika kiuno ukiwa mtu mzima sio mchezo). Hapo ni katikati ya jiji la Toronto ambapo kila mmoja anakaribishwa kufurahi na familia yake kwa michezo ya barafu. Tujifunze?
Duh !Jeff , Unajua ushakuwa mkanada/mmarekani , unajua wengine hatutumii fareniheiti? Sentigredi tu wengine:-) Jeff , Tuwekee picha ulizo anguka wakati una sketi au ku skiii