VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, February 10, 2007
NJIA YA CHINI KWA CHINI

Ingawa naamini kuna neno toshelezi au tafsiri ya moja kwa moja ya neno "tunnel", kamusi niliyonayo inaniambia kwamba tunnel kwa kiswahili ni "njia ya chini kwa chini". Pichani juu ni "njia ya chini kwa chini" inayoiunganisha majiji ya Windsor,Ontario,Canada na Detroit,Michigan,United States. Njia hii ya chini kwa chini ni ya pekee na kila siku hutumiwa na maelfu ya wakaazi wa Canada wanaovuka mpaka kuingia Marekani na hali kadhalika wakaazi wa marekani wanaovuka kuingia Canada.Inasemekana wapo watu kibao tu wanaishi Canada na kufanya kazi Marekani na pia wamarekani wanaofanya kazi Canada.Kumbuka kwamba nchi hizi zinaruhusu mtu kuwa na uraia wa nchi mbili mchakato ambao Tanzania inaufanyia kazi kwa mwendo wa kinyonga. Michuzi, Maggid na wengineo picha za namna hii mnaziitaje kwenye taaluma yenu?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:33 PM | Permalink |


Maoni: 9


 • Tarehe: 10:36:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger zemarcopolo

  Jeff unasemaje kuhusu mtanzania aliye na uraia wa nchi mbili au zaidi kuwa rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu?

   
 • Tarehe: 10:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger zemarcopolo

  samahani,hapo juu isomeke jamhuri ya muungano.

   
 • Tarehe: 1:06:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Zemarcopolo,
  Swali zuri sana.Binafsi nadhani mtu mwenye uraia wa nchi mbili asiruhusiwe hata kugombea uraisi achilia mbali kuwa raisi.Na sio uraisi tu bali pia vyeo au nafasi za kazi zozote tunazoweza kuziita "nyeti" ziendelee kushikiliwa na raia wa kuzaliwa huku tukihakikisha vigezo kama hicho cha kutokuwa na uraia wa nchi nyingine yeyote vikitiliwa mkazo na kwa makini.Kwa hali hiyo tume ya uchaguzi itakuwa haina budi kuongeza vipengele kama hivyo kama vile ambavyo hivi sasa bila digrii na umri fulani huruhusiwi kugombea uraisi.Nasikia hata ukiwa huna mke inakuwa ni tatizo kugombea achilia mbali kuongoza nchi.Kwa hiyo kwa maoni yangu,marufuku kuwa raia wa nchi mbili kama unatarajia kuongoza nchi au kuhodhi nafasi yoyote nyeti.

   
 • Tarehe: 5:01:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Halifa Mjengwa

  Labda niulize kwa vigezo vipi mtu aliyekuwa na uraia wa nchi mbili mojawapo ikiwa Tanzania asiweze kuwa raisi au kiongozi wowote wa juu katika serikali? Hasa ikizingatiwa huyu mtu uraia wake wa kuzaliwa na makuzi ni Tanzania?

   
 • Tarehe: 7:13:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Halifa,
  Jibu rahisi nadhani ni maslahi ya taifa.

   
 • Tarehe: 12:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Waperu wanaweza kutupa jibu zuri la swali hili kwa sababu wana eksipiriensi ya Rais Alberto Fujimori aliyekuwa na uraia wa nchi mbili; Peru na Japan.

  Wakati mwingine ukiangalia hata hao wazawa wanaongoza nchi zetu utafikiri hawaongozi kwao.

  Masalaamia,

  F MtiMkubwa Tungaraza.

   
 • Tarehe: 1:59:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Mbona kuna watu wenye urais wa nchi moja ambao wanaongoza bila kujali maslahi ya taifa? Hao je?

  Jeff: picha hiyo nimeipenda sana maana iko katika hali ya kisanii zaidi.

   
 • Tarehe: 1:39:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ndesanjo,
  Hao ni wengi na ndio hawa tunaohangaika nao kila kukicha.Hukumu yao inachemka jikoni.

  Shukrani kwa kuifagilia picha.

   
 • Tarehe: 1:24:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Hapo juu nilikosea neno "urais" lilipaswa kuwa "uraia."
  Dawa yao sio utani inachemka. Ngoja tu.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker